Kiranja Mkuu
JF-Expert Member
- Feb 18, 2010
- 4,066
- 4,085
Sisi wananchi wa Jimbo la Kawe hatujakutuma kugombana na kutukanana na shemeji yako.
Mambo ya kusema kuwa ndoa mbili za shemeji yako zilivunjika sababu ya tabia zake, na tangu ameingia kwenye familia yenu amekuwa akileta migogoro kila siku.
Hayo ni family matters, hayatuhusu wapiga kura.
Kuhusu chanjo, chanjo ni hiari ya mtu, eidha kuchanjwa ama kuto chanjwa.
Wananchi wa Kawe tunataka uwe upande wetu tunapolia kupanda kwa gharama za maisha.
Tukisema tozo ya miamala ni mzigo, utuelewe licha ya kwamba wewe ni biluonea mwenye madege, mahilikopta na una hela tayari ya kununua treni ya umeme.
Tukisema sisi wananchi hatujabahatika kujenga, lakini tunawalipia matajiri waliojenga Kodi zao za majengo utuelewe na uwe upande wetu.
Tunapolia kupanda kwa mafuta ya kula, Basi lia pamoja nasi, piga kelele dunia nzima isikie.
Sisi tuna maisha magumu yanayosababishwa na CCM halafu wewe unaleta mizaha, mara like mara hiki.
Tunakuomba utimize wajibu wa kututumikia.
Naamini umenielewa.
Kiranja Mkuu wa viranja wote kutoka Mbezi Beach, Kilongawima