Askofu Gwajima na Mbunge wa Kinondoni, wazuiwa kumuona Mufti Mkuu Muhimbili

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,689
55,661
Kwenye gazeti la Tanzania Daima, wameandika kwamba "Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Gwajima na Mbunge wa Kinondoni, Maulid Mtulia(CUF), wazuiwa kumuona Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakary Zubeiry, ambaye kalazwa katika Hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam".

Hii imenisikitisha sana kama siasa zimetufikisha huko. Sioni sababu ya kuzuia Mtu kumtembelea Mgonjwa.

Huu sio Utamaduni wa Mtanzania. Mbona mlisema Uchaguzi Umeisha? Mbona Viongozi wa CCM na UVCCM hawawekewi Vizingiti na Masharti kama Viongozi walionesha kuunga mkono UKAWA? Yaani wewe kama Uliunga mkono UKAWA utaruhusiwa kwa Masharti kibao kumuona Mgonjwa.

Watanzania tujitafakari upya.

Haya sio Mambo ya Kufurahia.

Tunajenga tunabomoa?
gwajima.png
 
Tunajenga na kubomoa simultaneously ,hivyo Zoea tu Mkuu watu ni wanafiki sana
 
Kwenye gazeti la Tanzania Daima, wameandika kwamba "Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Gwajima na Mbunge wa Kinondoni, Maulid Matulia(CUF), wazuiwa kumuona Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakary Zubeiry, ambaye kalazwa katika Hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam".

Hii imenisikitisha sana kama siasa zimetufikisha huko. Sioni sababu ya kuzuia Mtu kumtembelea Mgonjwa.

Huu sio Utamaduni wa Mtanzania. Mbona mlisema Uchaguzi Umeisha? Mbona Viongozi wa CCM na UVCCM hawawekewi Vizingiti na Masharti kama Viongozi walionesha kuunga mkono UKAWA? Yaani wewe kama Uliunga mkono UKAWA utaruhusiwa kwa Masharti kibao kumuona Mgonjwa.

Watanzania tujitafakari upya.

Haya sio Mambo ya Kufurahia.

Tunajenga tunabomoa?

Kuna Mtu Hapo Kwa Aina Za Dhambi Zake Na Unafiki Wake Angeruhusiwa Tu Kuingia Kumwona Mufti Wetu Pengine Asingepona Kabisa au Leo Tungekuwa Tunaomboleza. Akhsanteni Madaktari Na Shikamooni!
 
Kwenye gazeti la Tanzania Daima, wameandika kwamba "Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Gwajima na Mbunge wa Kinondoni, Maulid Matulia(CUF), wazuiwa kumuona Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakary Zubeiry, ambaye kalazwa katika Hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam".

Hii imenisikitisha sana kama siasa zimetufikisha huko. Sioni sababu ya kuzuia Mtu kumtembelea Mgonjwa.

Huu sio Utamaduni wa Mtanzania. Mbona mlisema Uchaguzi Umeisha? Mbona Viongozi wa CCM na UVCCM hawawekewi Vizingiti na Masharti kama Viongozi walionesha kuunga mkono UKAWA? Yaani wewe kama Uliunga mkono UKAWA utaruhusiwa kwa Masharti kibao kumuona Mgonjwa.

Watanzania tujitafakari upya.

Haya sio Mambo ya Kufurahia.

Tunajenga tunabomoa?

Mgonjwa pia ana haki zake.Yuko huru kusema kama kuna mtu anataka kuniona ruksa aje au najisikia leo kuonana na watu wawili tu au sitaki kuonana na mtu yeyote sijisikii vizuri au kila anayetaka kuniona aweke apppointment.

Ukilazwa sio kuwa kila chizi ruksa kukuona wengine waweza kuwa na maradhi ya kuambukiza wakakuambukiza na wengine ni wanga wanaweza kuwa wanakuja sio kukuona bali kukuwangia.Hapo kunawezekana kuna mwanga hapo yule ni sheikh tena sheikh mkuu aweza kujua mwanga yule anakuja kuniwangia.Amruhusu tu?
 
Hoja ya msingi, walikatazwa na nani? Kwa nini walikatazwa?

Kikubwa zaidi, kulikuwa na umuhimu gani wa kueleza media kwa sababu siyo suala la ajabu kwa mtu yoyote kukataliwa kumuona mgonjwa hata kama una uhusiano naye wa damu(ndugu wa karibu)
 
Pengine alikuwa na matibabu ya dharura, lakini hivi hivi siyo kawaida; sie wote ni wa MUNGU mmoja.
 
Bakwata ni miongoni mwa taasisi zinazomilikiwa na CCM. Hawa wanatudhalilisha sana sisi waislam. Might Allah Subhannah take them to Jehanam.
 
dah nimecheaka sana kwa habari hii.Inawezekana,yule askofu mpenda sifa angeenda hapo,na baadaye kutoa taarifa kuwa sheikh wetu ana majini yamekaba,na atamwombea ikiwezekana abadili na dini.
Ni mawazo tu ya kigwajimagwajima.By the way mimi kristo kwahiyo msijenge chuki hapaa.Namwombea heri sheikh wetu na kiongozi wetu apone haraka.
 
Bakwata ni miongoni mwa taasisi zinazomilikiwa na CCM. Hawa wanatudhalilisha sana sisi waislam. Might Allah Subhannah take them to Jehanam.
Hivi kwa nini mnalazimisha kumwona huyo mgonjwa sheikh mkuu?
Hao watu wawili ni lini wameanza kutembelea wagonjwa muhimbili? Wangeanza kwanza kuwa na tabia ya kutembelea wagonjwa wa kawaida.Mbona hatuwaoni wakiwatembelea? Halafu hivi mtu ukienda kumtembelea mgonjwa halafu hata daktari akisema usiingie kumwona au ndugu yake au yeye mwenyewe mgonjwa ni kitu cha kwenda kuwaeleza waandishi wa habari?

Hao wawili walikuwa na lao jambo.Mimi nimeshaenda hospitali ni kawaida kuambiwa huwezi mwona mgonjwa sasa hivi.HUULIZI KWA nini unajiondokea sio kesi.Sasa wao wanafungulia hadi kesi kuwa hatukupewa nafasi ya kumwona kama vile imo kwenye katiba kuwa mtu kama anaumwa atake asitake lazima watu wamwone.

Kitendo cha wao kulipeleka hilo kwenye vyombo vya habari kinaonyesha wazi walikuwa na nia OVU.
 
Mgonjwa yupo Hospitali kwa ajili ya kupatiwa Matibabu sio kutembelewa! Awali Viongozi mbalimbali wakiwemo akina Lowassa na Mgeja waliruhusiwa kumuona lakini kadri ziku zinavyoendelea Idadi ya wagonjwa imeongezeka bila ya kufuata taratibu imepelekea Madakatari kushindwa kuendelea na Matibabu!! Madakatari wana haki ya kuzuia acheni Siasa za Kipumbavu kwenye Afya za Watu!
 
ccm inatoka wapi kwenye ugonjwa wa mufti ??

kama ni uchaguzi mbona lowasa alienda kumwona juzi ??

ukawa ni kama mkemweza haishi maneno
 
Sidhani kama hoja hapa ni siasa. Mbona Mgombea wa CHADEMA na UKAWA, Edward Lowasa alienda kumtembelea huyo Mufti? Tafuteni sababu nyingine
 
Mleta mada huwa ni mzushi sana.Wanajamii muwe makini na nyuzi zake. Kwanza jina la mmbunge amekosea.
Fuatilieni nyuzi zake mtaona 100% ni uzushi.
 
Mgonjwa pia ana haki zake.Yuko huru kusema kama kuna mtu anataka kuniona ruksa aje au najisikia leo kuonana na watu wawili tu au sitaki kuonana na mtu yeyote sijisikii vizuri au kila anayetaka kuniona aweke apppointment.

Ukilazwa sio kuwa kila chizi ruksa kukuona wengine waweza kuwa na maradhi ya kuambukiza wakakuambukiza na wengine ni wanga wanaweza kuwa wanakuja sio kukuona bali kukuwangia.Hapo kunawezekana kuna mwanga hapo yule ni sheikh tena sheikh mkuu aweza kujua mwanga yule anakuja kuniwangia.Amruhusu tu?
Kama ana uwezo wa kujua mwanga au mchawi mbona hakujua Kama ataugua awahi kujikinga? Kama Majini yake yana nguvu mbona yameshindwa kuzuia kombora toka pemba? Hapo alipo anaumwa baada ya CUF kumbeep kidogo tu.
 
Back
Top Bottom