Askofu Gwajima, mahubiri yako ya jana tarehe 7 Machi, 2021 yana walakini

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,883
155,856

Ukihubiri kanisani kwako kwenye ibada umewashawishi waumini wako waungane na Rais Dk. John Pombe Magufuli kwenye kutoamini chanjo ya korona na badala yake tutegee maombi pekee.

Naomba nikukumbushe machache, hamna ugonjwa mkubwa ulitokomezwa duniani kwa maombi peke yake. Mungu aliweka karama MBALIMBALI kwa mwanadamu ili zikafanyike msaada kwa watu wote.

Hatukuitokomeza ndui kwa maombi, ila kwa chanjo za kisayansi.

Maombi hayakuondoa surua, ila chanjo za kisayansi ziliweza kuitokomeza.

Polio ugonjwa hatari, ulitokomezwa na chanjo za kisayansi. Ni kweli Yesu aliponya mwenye kupooza, lakini hakuondoa polio duniani.
Pepopunda na magonjwa lukuki hayajaondolewa na maombi wala kujifukiza ila ni kwa tiba za kisayansi.

Swala la afya ni swala la mtu BINAFSI, sijui kama hata hao waumini wako wana bima za afya, au bima zao ndio maji, chumvi na mafuta ya upako. Basi waache waumini wako wajiamulie ni tiba gani sahihi kwao kwenye kukabiliana na janga korona.

Kama ambavyo wewe BINAFSI hujawahi kutumia maombi kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine, na badala yake umenunua magari, helicopter na ndege, ambazo zimetengenezwa na wanasayansi, Basi heshimu mchango wa wanasayansi wa tiba.

Naamini umenialewa Baba Askofu, maisha yetu yana thamani kubwa na tunaishi mara moja tu hapa ulimwenguni, usiyageuze kuwa mtaji wako wa siasa na kumfurahisha mkubwa wako huku ukiangamiza roho za watu ambao huenda tiba za kisayansi zingewanusuru.
 
Nikweli kama ndivyo mabunduki na majeshi kwenye misafara yenu mpaka makanis
Kama kufa kupo, ahubiri neno la Mungu liletalo toba, aachane na propaganda.

Mathayo : Mlango 28​

19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
Wewe umeona andiko ni hilo tu kwenye biblia.
Kama kufa kupo, ahubiri neno la Mungu liletalo toba, aachane na propaganda.

Mathayo : Mlango 28​

19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
Unataka ahubiri injili moja kila siku, hujui kuwa kuna injili kama hizi

Ebr 9:27
"Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu"

Zab 104:30
"Waipeleka roho yako, wanaumbwa, Nawe waufanya upya uso wa nchi"
 
Back
Top Bottom