Askofu Gwajima amtetea Lowassa

Askofu Gwajima amtetea Lowassa

gumegume

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2011
Posts
1,063
Reaction score
620
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, kwa mara ya kwanza amejitosa kwenye harakati za Urais kwa kutoa kauli za ukosoaji zinazowalenga baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaoutaka Urais.

Katika mazungumzo yake na RAI, Gwajima alisema kauli zilizotolewa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Naibu Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano, Januari Makamba na Waziri Mkuu wa zamani Cleopa Msuya dhidi ya wanasiasa wenzao zina dhamira ovu ya kupakana matope.

Akizungumzia kauli hizo, Askofu Gwajima alisema wanasiasa wanaodai kuchukizwa na mafisadi na kusema kwamba Watanzania wasiwachague wagombea urais wanaotumia fedha, hawana hoja badala yake wanaendesha vita ya Urais.

"Kwani mtu yeyote mwenye akili timamu anajua kwamba bila fedha huwezi kujenga mtandao wa Urais, ili ufanikiwe unahitaji kutumia fedha kujenga mtandao, kwa mfano unahitaji usaidizi wa watu wa Rukwa, Mwanza n.k; lazima uwe na watu huko Rukwa na Mwanza na lazima utoe fedha ili watu hao waweze kusafiri, kula na kulala."

"Bila fedha huwezi kuwaza suala la Urais, maneno yao yanalenga kupotosha watu kwamba wako watu fulani wasiotumia fedha, huku wakijua ukweli kwamba kila mtu anatumia fedha, kwa mfano fomu ya kuwania Urais ni shilingi milioni tano, sasa wao hizo fedha watakuwa wamezipata wapi? Kiujumla, hatua kubwa kama ya Urais inahitaji fedha," alisema.

SOURCE: GAZETI LA RAI ALHAMISI JANUARI 8-14, 2015
 
Gwajima tapeli kama matapeli wengine tu naye ni miongoni mwa watu waliogawiwa hela na mafisadi lakini zitamtokea puani.
 
bila fedha huwezi kuwa rais huo ndio ukweli kumbuka obama alivyovunja rekodi ya kukusanya pesa

hata mapinduzi ya kumwaga damu au ya amani huhitaji pesa pia
 
kashapewa mlungula huyo, pesa inaweza kumfanya mtu akawa taahira kabisa
 
Lakini siyo hizi mafisadi kama Lowasa anakera sana.

Pesa alizo zungumzia hapa sidhani kama ni za kuwa nunua watu, bali ni za kufanya shughuli za kisiasa. Kama amezungumzia za kununua watu na yey Gwajima akasapoti na asikemee kama kiongozi wa kiroho, nitakuwa na walakini nae zaidi
 
Jamaa kaongea ukweli mbona bila fedha halifanyiki jambo, wanaosem hawatumii hela wanafki tu

Mkuu,

Hoja ya msingi ni kuwa, hizo pesa wanazotumia wamezipata wapi na kama wamezipata katika njia inayokubalika kiutaratibu na kisheria, basi hoja ya pili itakuwa, hizo pesa wanazitumia katika msingi ulio ndani ya taratibu na kanuni walizojiwekea na vyama vyao vya siasa?

Lakini vile vile ukiaangalia hoja ya Gwajima, inavyoonekana anataka kuharalisha makosa ili kutetea makosa mengine
 
Yeye angesubiri apitishwe na chama chake kisha chama kingemsaidia,nafikiri lawama zisingekuwepo,then baada ya kupitishwa na chama na endapo chama kitakuwa hakina pesa za kampeni ndipo angeonesha ukereketwa wake kwa chama kwa kutoa pesa yake mfukoni...lakini hili la kuanza kutoa toa vichochoroni inaashiria 1:HAJIAMINI
2:NI FISADI KWELI
3:ANAHISI AMECHOKWA NA CHAMA AMA WANANCHI
Sasa kama yote hapo juu ni sahihi na bado anagawa pesa kuomba msaada kuingia ikulu lazima tujiulize!!!
 
yah ukweli utabaki kuwa ukweli, mimi ninachoelewa mtu anahitaji fedha ili kutimiza dhamila yake gwajima yupo sahihi kabisa lakini cha msingi ni kujua hizo fehda zinatumikaje katika kutimiza hiyo dhamila. kama zitatumika vibaya kweli lakini kama ni kuwa weka pamoja watu wa dini mbalimbali, wasomi, wakulima na makundi mengine naona yupo sahihi
 
Mkuu,

Hoja ya msingi ni kuwa, hizo pesa wanazotumia wamezipata wapi na kama wamezipata katika njia inayokubalika kiutaratibu na kisheria, basi hoja ya pili itakuwa, hizo pesa wanazitumia katika msingi ulio ndani ya taratibu na kanuni walizojiwekea na vyama vyao vya siasa?

Yeah, ndio maana nkasem kama ni kwa lengo la kuwanunua watu, wote ni washenz hao then
 
Sijui kashamwacha yule mwimbaji wa nyimbo za Injili.Halafu kuna ile scandal ya kuzaa na mke wa mtu Dr fulani sijui kesi imemalizika au imechinjiwa baharini.
 
wote wenye chuki na lowassa mtahaha sana mwaka huu. nani msafi ccm wa kusema anafaa kuwa raisi? hata kama lowassa ni fisadi hategemei hizo pesa. na angekuwa anategemea ufisadi siku nyingi hizo pesa zingeshaisha. acheni unoko maana lowassa ni raisi na itawauma sana.
 
Hivi gwajima ndiyo anayetembea na wake za watu kama ndiye kesha laaniwa hata anayozungumza siyo yeye ni shetani aliyemwingia.
 
Back
Top Bottom