Pamoja na leo kipande cha sauti kusambaa kuwa Gwajima angejisalimisha Jumatatu kwa kuwa kwa sasa yupo Arusha na kuwataka waumini wake kufika polisi Jumatatu bila kufanya vurugu.
Kwa sababu ambazo hazijatolewa bado, askofu Gwajima amejisalimisha kituo cha Polisi tayari leo Ijumaa ili kuhojiwa juu ya kutoa lugha chafu dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Audio: Askofu Gwajima awajibu Polisi Kuhusu kuitwa aende kujieleza
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amejisalimisha katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, kwa ajili ya kuhojiwa kutokana na tuhuma za kutoa lugha chafu dhidi ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Akizungumza nje ya kituo hicho kabla ya kuanza kuhojiwa, Gwajima amekaririwa na FikraPevu akisema kwamba alichofanya yeye ni kutumia fursa ya kumuonya kiongozi mwenzake wa kiroho kutokana na kuwageuka wenzake juu ya makubaliano waliyofikia katika tamko lao linalowahamasisha waumini wao kupiga kura ya hapana kwa Katiba Inayopendekezwa.
Gwajima, anasema mbali na hilo la Katiba Inayopendekezwa, tamko husika lililotolewa na Jukwaa la Wakristo Tanzania, lilipinga kutungwa kwa sheria ya Bunge, chini ya uratibu wa Serikali, inayoruhusu kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi.
"Mimi kama kiongozi wa kiroho niliona nimkemee (Kardinali Pengo) kwa sababu mimi ni Askofu wa Kanisa, na yeye pia ni Askofu wa Kanisa. Ilibidi nimkemee kwamba aache kufanya vile alivyofanya, kuwageuka Maaskofu wenzake," amekaririwa Gwajima akisema na kuongeza, "Lakini cha msingi ambacho ndicho cha kuwaza niliyemkemea ni Kardinali Pengo au Polisi?"
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, alimtaka Gwajima kujisalimisha kuhojiwa kufuatia kusambaa mitandaoni sauti na picha za video zinazomuonyesha akimshambulia kwa maneno makali Kardinali Pengo.
Soma zaidi => Gwajima mikononi mwa Kamanda Kova kwa tuhuma za Kumkashifu Kardinali Pengo