Askofu Gwajima aidanganya mahakama

Askofu Gwajima aidanganya mahakama

10000

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2013
Posts
837
Reaction score
781
Katika uchambuzi wa mageziti asubui ya leo nimesikia gazeti moja likiandika kwamba;

Askofu wa kanisa la ufufuo na uzima Gwajima amekanusha mashtaka aliyoshtakiwa kwayo na JMT kufuatia kumtukana Askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo.

Uongo aliousema askofu Gwajima ni kukataa mbele ya hakimu kwamba hakumuita askofu Pengo mtoto, mpuuzi. Maneno ambayo yanaweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Kukataa kwake kusema ukweli inadhihirishia umma wa Tanzania kwamba Askofu Gwajima ni mtu muongo.
Gwajima akana kortini kumtusi Kardinali Pengo

gwajima_askofu.jpg

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima

KWA UFUPI
Akisomewa maelezo na Wakili wa Serikali, Joseph Maugo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilfred Dyansobera, Gwajima alikana kutoa lugha chafu ila alikubali kuwa yeye ni askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, majina yake na kwamba aliitwa polisi Machi 27, 2015 kwa ajili ya kuhojiwa

Dar es Salaam
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amekana kumtolea lugha chafu Askofu wa Kanisa Katoliki, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo wakati akisomewa maelezo ya awali katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam jana.

Akisomewa maelezo na Wakili wa Serikali, Joseph Maugo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilfred Dyansobera, Gwajima alikana kutoa lugha chafu ila alikubali kuwa yeye ni askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, majina yake na kwamba aliitwa polisi Machi 27, 2015 kwa ajili ya kuhojiwa .

Maugo alidai upande wa mashtaka utawaita mashahidi saba kutoa ushahidi dhidi ya Gwajima pamoja na kuwasilisha vielelezo vitano.

Wakili wa Gwajima, Peter Kibatala aliomba kupewa maelezo ya mlalamikaji katika kesi hiyo.

Hakimu Dyansobera aliuagiza upande wa mashtaka kuwapatia maelezo ya mlalamikaji na kwamba kesi itaanza kusikilizwa kwa mashahidi upande wa mashtaka kutoa maelezo yao Agosti 10, mwaka huu.

Ilidaiwa kuwa kati ya Machi 16 na 25, mwaka huu kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, Gwajima alitoa lugha chafu dhidi ya Pengo.

Akisoma maelezo ya awali, Maugo alidai kati ya Machi 16 na 25, Gwajima alitoa maneno machafu kwa Pengo.

Hata hivyo, Gwajima aliyakana maelezo hayo na kukubali maelezo yake binafsi ya kuitwa polisi.

Katika kesi inayomkabili Askofu Gwajima na wenzake watatu, Maugo alisema nayo ilikuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali, lakini mshtakiwa mmoja hakuwapo mahakamani kutokana na kusumbuliwa na maradhi.

Alidai kwa mujibu wa sheria, mshtakiwa anatakiwa kuwapo mahakamani, hivyo aliomba ipangwe tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea maelezo ya awali, ambapo itasikilizwa Oktoba 8, mwaka huu.

Katika kesi hiyo, Gwajima anakabiliwa na shtaka la kushindwa kuhifadhi silaha na risasi anazomiliki kihalali.

Kwa upande wa washtakiwa wenzake, akiwamo mlinzi wake, George Mzava, Yekonia Bihagaze na Mchungaji Georgey Milulu, wao wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa wakimiliki bastola aina ya Berretta pamoja na risasi 20 kinyume cha sheria.

Wanadaiwa kuwa Machi 29, mwaka huu katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni A walikutwa wakimiliki bastola hiyo yenye namba CAT 5802 bila ya kuwa na kibali kutoka mamlaka husika.

Pia wanadaiwa kuwa siku hiyo, washtakiwa hao pia walikutwa wakimiliki isivyo halali risasi tatu za bastola pamoja na risasi 17 za bunduki aina ya Shotgun. Washtakiwa wako nje kwa dhamana.


CHANZO:
MWANANCHI

 
huenda tafsiri ya neno mtoto na mpuuzi inamaanisha kitu kingine kwa gwajima na sio hakimu anavyofikiria, atakapoulizwa maana tutamsikia akitoa ufafanuz
 
10000

mkuu tulia usikurupuke kiasi hicho sheria ni noma unaweza ukasema kaidanganya mahakama lakin ktk utetezi wake akawa na point za kutosha na kuwabwaga mbaya
 
Last edited by a moderator:
Hakuna kesi hapo ni uhuni tu nna upotevu wa pesa za umma kuiendesha kesi za kipuuzi na kipumbavu. Kesi ziko nyingi serikali inakomalia kesi zisizo na tija,, ilikua presha ya pinda kwa kutukanwa mfipa mwezake sasa amekatwa awe mpole.

Gwajima atashinda hiyo kesi.
 
10000

hivi kuna watu bado wamfuata gwajima...jamani wandugu fungukeni ata macho bac...ni nyakati za mwisho...
 
Last edited by a moderator:
10000

Tena uongo wa mtu ambaye waumini wake wanaamini maneno yake halafu leo anakanusha huo ni uhuni ambao ni mbaya sana hakuna tofauti na ibilisi mwenyewe. Tena katika clip anasikika akisema Askofu Mkuu Pengo ni sawa na mtoto anayevaa pampas. Inashangaza leo anakana hayo, kama kiongozi wa dini ilifaa sana awe mkweli kwani ingekuwa ni ushuhuda na mfano bora kwake nabkwa kanisa lake.
 
Last edited by a moderator:
Wewe nenda ukawe hakimu/jaji kama unadhani mahakama imedanganywa...
 
Kesi kazi hizi huwa zinajifia zenyewe kimya kimya
 
Ndiyo nimesikia leo kwamba neno "MTOTO" ni tusi linaloweza kupelekea uvunjifu wa amani. Na ni nani mlalamikaji katika hili shauri?
 
kesi ambayo mlalamikaji ni jamhuri mara nyingi jamhuri huwa anapigwa chini

Jamhuri bila shahidi anayethibitisha athari za neno mtoto kwake?

Hivi mtoto ni tusi?

Hapa naona hata shetani anasingiziwa! Shetani ni cha mtoto!
 
Pengo alishamsamehe Gwajima sasa kesi mlalamikaji ni nani?siasa za mpaka mahakamani
 
10000

Tena uongo wa mtu ambaye waumini wake wanaamini maneno yake halafu leo anakanusha huo ni uhuni ambao ni mbaya sana hakuna tofauti na ibilisi mwenyewe. Tena katika clip anasikika akisema Askofu Mkuu Pengo ni sawa na mtoto anayevaa pampas. Inashangaza leo anakana hayo, kama kiongozi wa dini ilifaa sana awe mkweli kwani ingekuwa ni ushuhuda na mfano bora kwake nabkwa kanisa lake.

Awe mkweli mbele ya nani. Sheria haiendi hivyo, lazima ukatae ili kesi iendelee upate muda wa kujieleza/ utetezi. Ukisema ndio kesi inaisha unapangiwa siku ya hukumu.
 
Last edited by a moderator:
sasa mtu anayesema anafufua watu anaachaje kuwa muongo..
 
Back
Top Bottom