GE2025 Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula, atoa Kauli Kuhusu Mkutano wa Rais Samia na Kadinali Rugambwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Kupitia ukurasa wa Mtandao wa Kijamii Facebook Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula ameandika kuhusiana na Mkutano wa Rais Samia anayemaliza muda wake na pia ni Mgombea Urais Kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) kukutana na Viongozi wa Kanisa Roman Katoliki Muadhama Protase Kadinali Rugambwa na Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo Kuu la Tabora, Paul Ruzoka ambapo picha na video zilisambaa mtandaoni

-----------------

ASKOFU ATOA KAULI KUHUSU MKUTANO WA RAIS SAMIA NA KADINALI RUGAMBWA
Jana, 12 Septemba 2025, Ikulu ilitoa hadharani picha za Rais Samia akiwa pamoja na viongozi wa Kanisa Roman Katoliki, Muadhama Protase Kadinali Rugambwa na Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo Kuu la Tabora, Paul Ruzoka.
Mitandao ya kijamii iliendelea kuzisambaza picha hizo ikitaja maudhui ya kikao hicho kuwa ni kuombewa na wengine wakisema kuwa Rais alikwenda kuombewa. Lakini kwa sababu pia ya mazingira ya sasa nchini watu wanahusisha moja kwa moja na masuala ya uchaguzi

Lakini ni bahati sana mbaya kuwa hata baadhi ya waumini wa Kikristo wanaojua vema wajibu wa askofu kwa jamii na kwa viongozi wa siasa wameingiwa na ukakasi juu ya tukio hilo huku wengine wakijaribiwa kuwafikiria vibaya baadhi ya viongozi wa Kanisa wanaokutana na Rais Samia katika kipindi hiki

Pamoja na mtizamo wangu kuhusu uchaguzi wa mwaka huu ambao unajulikana wazi kuwa tusiingie katika uchaguzi bila ya maridhiano na Reforms kufanyika, siwezi kuwa kipofu kuhusu wajibu wa askofu wa mnyororo kwa viongozi wa Serikali akiwemo Rais wa nchi

Kuhusu mkutano wa jana baina ya Rais Samia na Kadinali Rugambwa, nimebaini ya kuwa siyo kweli kuwa Rais Samia alikwenda kwa Kadinali ili kuombewa hata kama alipata maombi. Lakini ukweli ni kuwa mkutano ule ulifanyika Ikulu ya Tabora. Kwa hiyo, Kadinali Rugambwa pamoja na ujumbe wake ndio waliokwenda Ikulu kwa ajili ya kumuona Rais Samia Suluhu Hassan

Kama huo ndio ukweli, basi jambo moja kati ya haya mawili lilifanyika: Mhe. Rais Samia ndiye aliyetoa mwaliko kwa Kadinali Rugambwa na ujumbe wake kuonana na Rais Ikulu ya Tabora. Ni vigumu kwa Kadinali kukataa mwaliko wa Rais akiwa Tabora na wakati yeye yupo Tabora

Lakini jambo la pili inawezekana kuwa Kadinali Rugambwa ndiye aliyeomba nafasi ya kukutana Rais Samia katika Ikulu ya Tabora kama alijua ya kuwa Rais atakuwa maeneo yale. Ni vigumu kwa Rais kukataa kukutana na Kadinali wakati anatembelea maeneo yale yale

Je, mkutano wao ulikuwa na ajenda gani hasa? Wahusika hawajatoa hadharani kuhusu jambo au mambo waliyoteta. Inawezekana waliongea juu ya uchaguzi; inawezekana walizungumza juu ya masuala ya Kanisa; lakini inawezekana pia walizungumzia juu ya masuala ya nchi na nchi ikizingatiwa kuwa Kadinali Rugambwa ni mshauri wa Papa ambaye ni Mkuu wa Vatican na kama tujuavyo, Vatican ni nchi

Lakini kuhusu kumuombea Rais, jambo moja liko wazi. Liturgia ya Kanisa letu ina kipengele cha kumuombea Rais mara mbili kwa mwezi kila Jumapili. Ninafahamu pia kuwa makanisa yote yenye uaskofu wa mnyororo ikiwemo RC wameweka utaratibu kama huo katika liturgia zao kwani Liturgia zetu zinalingana kwa kiasi kikubwa kwani zote zina asili moja - Kanisa Takatifu Katholiko lililo moja

Katika utaratibu huo wa liturgia, Rais haombi kuombewa, bali ni wajibu wa Kanisa kufanya hivyo. Kila muumini hupata fursa ya kuombea viongozi wa nchi akiwemo Rais kwa njia hiyo

Maudhui ya maombi ni pamoja na kumuomba Mungu ampe hekima ili aongoze na kutawala kwa upendo na haki. Rais akibadilika, mbadala wake ataombewa kwani liturgia haibadilishwi kwa ajili ya mtu. Hata nchi akipinduliwa akaja mtawala wa kijeshi kinyume cha katiba, bado kipengere cha liturgia kitabaki na kuendelea pia kumuombea dikiteta huyo atawale kwa haki!

Hata hivyo Rais anayo haki ya kumtafuta hata kwenda kwa kiongozi wa Kanisa ili pia kutafuta ushauri kama alivyofanya Nikodemu, aliyekuwa kiongozi mwandamizi au waziri katika Barabara la Uongozi la Sanhedrin la nchi ya Yuda. Mhe. Nikodemu alimuendea Yesu usiku wa manane ili kupata ushauri (Yohana 3:1-15)

Viongozi wa serikali wanaweza kumuendea kwa kificho kiongozi wa dini askofu kulingana na mazingira yao au mazingira ya askofu kama alivyofanya Nikodemu kwa kumuendea Yesu usiku. Wakati wa Rais Magufuli, niliwahi kujiwa katika makazi ya askofu usiku na waziri wake

Wakristo ni watu wanaongozwa kwa maandiko (scripture), mantiki (reasons), Ufunuo kutoka kwa Mungu (Revelations) pamoja na mapokeo (traditions). Hivi ndivyo ambavyo huwaongoza pia maaskofu wa mnyororo katika kutimiza ulio wajibu wao. Maaskofu hawaongozwi na hisia za watu katika jamii au waumini wao. Hii ndiyo sababu maaskofu wanaaminika katika kutenda haki

Kitendo cha Rais Samia kukutana na Kadinali Rugambwa wakati huu hata kama hatujajua ni nini ilikuwa ajenda ya mazungumzo yao, sisi wengine tulio waumini wa masuala ya haki na utetezi wa haki nchini inapasa tufurahi badala ya kununa. Je, ni nani ajuaye kuwa hiyo ndiyo sehemu ya majibu ya maombi yetu?

Watu wanahimizwa kuomba na wajibu wao ni kuomba. Lakini ni kwa namna gani maombi yao yatajibiwa na Mungu hilo halikukirumiwa katika mikono yetu na uelewa wetu. Tusivuke mipaka!

Nilitamani sana kujua katika mkutano wao wa siku 14 baina ya Mtume Paulo na Mtume Kefa (Petro) walizungumza nini mjini Yerusalemu, lakini sijawahi kufahamu zaidi ya Mtume Paulo kutueleza tu kuwa walikutana (Wagalatia 1:18)

Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 13 Septemba 2025; Saa 2:50 asubuhi

Soma pia

1757832874495.png

1757833190329.png

1757833269804.png

1757833348476.png
 
Binafsi, nimekuelewa vyema kabisa Askofu Mwamakula...

Tupo ktk kipindi kigumu mno kama jamii. Kipindi cha gepu kubwa la uhasama na kutoaminiana kati ya viongozi wa serikali na wananchi au jamii...

Hakuna kiongozi yeyote wa serikali kwa sasa anayeweza kutenda jambo fulani kwa nia njema kisha jamii ikamwelewa na kumuamini. Honestly, hii si situation njema na ya kujigamba nayo au kuifurshia. Hiki ni kiashiria cha hatari huko tuendako iwapo hatutarekebisha kwa toba mbele ya Mungu wetu...

Wengi wanaamini kuwa, kitendo cha Rais kuonana na maaskofu wetu hawa, tafsiri ya kimantiki ya mkutano huo inayogonga kwenye vichwa vya watu haraka haraka ni "amekwenda kuhonga mapesa maaskofu wetu ili wanyamaze, wasimkosoe na kubariki zoezi la uchaguzi haramu linaoendelea sasa..."

Nyakati na mazingira zinalazimisha watu wafikiri hivi. Sio kosa lao hawa watu. Ni mazingira ya hali halisi. Tunapaswa kutubu, kuomba neema na rehema kwa Baba Mungu wetu wa mbinguni ili atuepushe na mkono wa hukumu yake kama taifa....

Contrary to this, tunakuja ktk hoja ya Askofu Mwamakula, kuwa, possibly Rais Samia labda alikwenda kupata ushauri. Inawezekana pia alikwenda kutubu na kujutia mambo na matendo yake...

Mungu kwa kweli ana njia na namna yake ya kujibu maombi ya watu wake. Mara nyingi huwa ni kinyume na jinsi sisi wanadamu tunavyowaza, huwa ni kinyume na njia na mipango yetu wanadamu...

Mungu wa mbinguni awe nawe daima Baba Askofu Mwamakula...
 
maaskofu wa katoliki la mitume huwa hawahongeki.hawana price yeyote ile
 
Kupitia ukurasa wa Mtandao wa Kijamii Facebook Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula ameandika kuhusiana na Mkutano wa Rais Samia anayemaliza muda wake na pia ni Mgombea Urais Kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) kukutana na Viongozi wa Kanisa Roman Katoliki Muadhama Protase Kadinali Rugambwa na Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo Kuu la Tabora, Paul Ruzoka ambapo picha na video zilisambaa mtandaoni

-----------------

ASKOFU ATOA KAULI KUHUSU MKUTANO WA RAIS SAMIA NA KADINALI RUGAMBWA
Jana, 12 Septemba 2025, Ikulu ilitoa hadharani picha za Rais Samia akiwa pamoja na viongozi wa Kanisa Roman Katoliki, Muadhama Protase Kadinali Rugambwa na Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo Kuu la Tabora, Paul Ruzoka.
Mitandao ya kijamii iliendelea kuzisambaza picha hizo ikitaja maudhui ya kikao hicho kuwa ni kuombewa na wengine wakisema kuwa Rais alikwenda kuombewa. Lakini kwa sababu pia ya mazingira ya sasa nchini watu wanahusisha moja kwa moja na masuala ya uchaguzi

Lakini ni bahati sana mbaya kuwa hata baadhi ya waumini wa Kikristo wanaojua vema wajibu wa askofu kwa jamii na kwa viongozi wa siasa wameingiwa na ukakasi juu ya tukio hilo huku wengine wakijaribiwa kuwafikiria vibaya baadhi ya viongozi wa Kanisa wanaokutana na Rais Samia katika kipindi hiki

Pamoja na mtizamo wangu kuhusu uchaguzi wa mwaka huu ambao unajulikana wazi kuwa tusiingie katika uchaguzi bila ya maridhiano na Reforms kufanyika, siwezi kuwa kipofu kuhusu wajibu wa askofu wa mnyororo kwa viongozi wa Serikali akiwemo Rais wa nchi

Kuhusu mkutano wa jana baina ya Rais Samia na Kadinali Rugambwa, nimebaini ya kuwa siyo kweli kuwa Rais Samia alikwenda kwa Kadinali ili kuombewa hata kama alipata maombi. Lakini ukweli ni kuwa mkutano ule ulifanyika Ikulu ya Tabora. Kwa hiyo, Kadinali Rugambwa pamoja na ujumbe wake ndio waliokwenda Ikulu kwa ajili ya kumuona Rais Samia Suluhu Hassan

Kama huo ndio ukweli, basi jambo moja kati ya haya mawili lilifanyika: Mhe. Rais Samia ndiye aliyetoa mwaliko kwa Kadinali Rugambwa na ujumbe wake kuonana na Rais Ikulu ya Tabora. Ni vigumu kwa Kadinali kukataa mwaliko wa Rais akiwa Tabora na wakati yeye yupo Tabora

Lakini jambo la pili inawezekana kuwa Kadinali Rugambwa ndiye aliyeomba nafasi ya kukutana Rais Samia katika Ikulu ya Tabora kama alijua ya kuwa Rais atakuwa maeneo yale. Ni vigumu kwa Rais kukataa kukutana na Kadinali wakati anatembelea maeneo yale yale

Je, mkutano wao ulikuwa na ajenda gani hasa? Wahusika hawajatoa hadharani kuhusu jambo au mambo waliyoteta. Inawezekana waliongea juu ya uchaguzi; inawezekana walizungumza juu ya masuala ya Kanisa; lakini inawezekana pia walizungumzia juu ya masuala ya nchi na nchi ikizingatiwa kuwa Kadinali Rugambwa ni mshauri wa Papa ambaye ni Mkuu wa Vatican na kama tujuavyo, Vatican ni nchi

Lakini kuhusu kumuombea Rais, jambo moja liko wazi. Liturgia ya Kanisa letu ina kipengele cha kumuombea Rais mara mbili kwa mwezi kila Jumapili. Ninafahamu pia kuwa makanisa yote yenye uaskofu wa mnyororo ikiwemo RC wameweka utaratibu kama huo katika liturgia zao kwani Liturgia zetu zinalingana kwa kiasi kikubwa kwani zote zina asili moja - Kanisa Takatifu Katholiko lililo moja

Katika utaratibu huo wa liturgia, Rais haombi kuombewa, bali ni wajibu wa Kanisa kufanya hivyo. Kila muumini hupata fursa ya kuombea viongozi wa nchi akiwemo Rais kwa njia hiyo

Maudhui ya maombi ni pamoja na kumuomba Mungu ampe hekima ili aongoze na kutawala kwa upendo na haki. Rais akibadilika, mbadala wake ataombewa kwani liturgia haibadilishwi kwa ajili ya mtu. Hata nchi akipinduliwa akaja mtawala wa kijeshi kinyume cha katiba, bado kipengere cha liturgia kitabaki na kuendelea pia kumuombea dikiteta huyo atawale kwa haki!

Hata hivyo Rais anayo haki ya kumtafuta hata kwenda kwa kiongozi wa Kanisa ili pia kutafuta ushauri kama alivyofanya Nikodemu, aliyekuwa kiongozi mwandamizi au waziri katika Barabara la Uongozi la Sanhedrin la nchi ya Yuda. Mhe. Nikodemu alimuendea Yesu usiku wa manane ili kupata ushauri (Yohana 3:1-15)

Viongozi wa serikali wanaweza kumuendea kwa kificho kiongozi wa dini askofu kulingana na mazingira yao au mazingira ya askofu kama alivyofanya Nikodemu kwa kumuendea Yesu usiku. Wakati wa Rais Magufuli, niliwahi kujiwa katika makazi ya askofu usiku na waziri wake

Wakristo ni watu wanaongozwa kwa maandiko (scripture), mantiki (reasons), Ufunuo kutoka kwa Mungu (Revelations) pamoja na mapokeo (traditions). Hivi ndivyo ambavyo huwaongoza pia maaskofu wa mnyororo katika kutimiza ulio wajibu wao. Maaskofu hawaongozwi na hisia za watu katika jamii au waumini wao. Hii ndiyo sababu maaskofu wanaaminika katika kutenda haki

Kitendo cha Rais Samia kukutana na Kadinali Rugambwa wakati huu hata kama hatujajua ni nini ilikuwa ajenda ya mazungumzo yao, sisi wengine tulio waumini wa masuala ya haki na utetezi wa haki nchini inapasa tufurahi badala ya kununa. Je, ni nani ajuaye kuwa hiyo ndiyo sehemu ya majibu ya maombi yetu?

Watu wanahimizwa kuomba na wajibu wao ni kuomba. Lakini ni kwa namna gani maombi yao yatajibiwa na Mungu hilo halikukirumiwa katika mikono yetu na uelewa wetu. Tusivuke mipaka!

Nilitamani sana kujua katika mkutano wao wa siku 14 baina ya Mtume Paulo na Mtume Kefa (Petro) walizungumza nini mjini Yerusalemu, lakini sijawahi kufahamu zaidi ya Mtume Paulo kutueleza tu kuwa walikutana (Wagalatia 1:18)

Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 13 Septemba 2025; Saa 2:50 asubuhi

Soma pia

Askofu asipate tabu kujieleza wakati huu! Baba Askofu Rugambwa amekutana na Rais mara mbili wakati huu wa uchaguzi ktk ikulu tofauti! Ni wazi mikutano hio si ya bahati mbaya! Je ingelikuwa ni Baba Askofu Malasusa amefanya hayo angekuja na busara hizo? Anyway tuache hayo hayana faida sana pengine...ninachotaka sema, Hao viongozi wakubwa wa nafasi hizo wana wajibu wa kuwa juu ya matabaka yao na kutazama maslah ya nchi! Kama alivyo chambua leo akumbuke tu siku nyingine viongoizi wa matabaka mengine yawe ya kisiasa, kijamii au dini kama hivyo wakifanya kama hayo aliyofanya Baba Askofu Rugambwa watunze ndimi zao ktk kuwabagaza pengine kwa malengo ya kuwaondolea imani wanayopata toka kwa jamii!
 
Askofu Mwamakula siku ya maandamano aandamane akiwa amevaa ile kofia yake kama ganda la chungwa anayoivaaga kisogoni
 
Back
Top Bottom