Ringo Malisa
Member
- Nov 3, 2019
- 25
- 13
Nawazungumzia Askofu Emmanuel Bandekile Mwamakula na Askofu Dr. Benson Bagonza. Nimekuwa nikitafakari sana kuhusu watumishi hawa wapakwa mafuta wa kanisa hapa nchini. Nashindwa niwaweke kundi lipi lakini naona niwaite watumishi wa kanisa.
Wakati Taifa lilipopitia wakati mgumu wa maambukizi dhidi ya corona, sikubahatika kuwasikia wakisema tufanye nini kama wafuasi wao makanisani zaidi ya kubeza juhudi za Mhe. Rais wa Nchi Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pale aliposema tufunge kwa muda wa siku tatu na kumlilia Mungu aiponye Nchi yetu dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa corona.
Swali langu ni je! kama kwa namna moja ama nyingine mnatumwa na baadhi ya watu wasioupenda Utawala wa awamu hii ya tano, ni kiasi gani cha pesa mnacholipwa ili kuhakikisha watanzania wanaingiwa upofu wa kutoyaona mambo mengi na mazuri ambayo serikali ya Rais Magufuli imewafanyia watanzania? Na je! mnatolea fungu la kumi kiasi hicho cha pesa mnacholipwa? Inatesa sana akili yangu.
Kwa kuwa ninyi ni waandishi wazuri sana mlioona uandishi haulipi mkachagua usaliti wa Nchi pengine unalipa vizuri, naomba mje na makala za kutosha kuiridhisha akili yangu. Wakati huo mfahamu kuwa endapo adhima yenu itafanikiwa na nchi ikaingia kwenye machafuko (VITA), hakika hamtaweza kuabudu na hata sadaka hamtazipata tena. Tupone katika hili. Asanteni sana