Askofu Dk Stephen Munga wa KKKT, avuliwa Uchungaji, Wachungaji 7 Wasimamishwa

Askofu Munga alishastaafu, sasa wanamfukuza mstaafu hapo ni sawa na kupiga bomu Mochwari.
 
Askofu wa dayosisi ya Kaskazini Mashariki (Tanga) ni Dr. Msafiri Mbilu, alichaguliwa mwaka jana November na kuingizwa kazini April 2021....so Dr Munga sio Askofu wa hiyo dayosisi sijui huo uaskofu amevuliwa vipi, ni Askofu mstaafu kwa sasa.
Ni kweli anatuhuma mbali mbali za ubadhilifu wa pesa na mali za dayosisi lkn alishatoka kwenye hicho kiti tangu April, maybe yeye na wenzake wavuliwe huo uchungaji kama unavyosema ndio atakuwa amepoteza hata hiyo hadhi ya kuwa askofu mstaafu. Mleta taarifa rekebisha taarifa yako...Munga ni Askofu mstaafu
Naona wewe umeyaweka haya mambo Sawa.
 
Bla bla ndio ku-critize au njia mpya ya kufanya argument?
Rwaichi alisema mkachanje au ni watawa tu.
Wewe kama unadai ushawishi wake umeongezeka huku wao wakikili wamepoteza ushawishi
siwezi nkafanya argument na wewe uwe unamfuatilia pope wako basi.
Kwenda kuchanja ndio kipimo cha ushawishi? Kama ndivyo unavyofikiria waumini wa RC wapo hivyo basi haujui lolote kuhusu RC
 
Ndiyo ilikuwapo
Catholic ipi ile iliyo waua gnostic wote walio pinga uhusiano wa bible agano la kale na jipya
Mungu wa agano laa kale ni muuaji, chuki na visasi na wa jipya Mungu wa upendo, mpole na mnyenyekevu
lakini siku ya mwisho tena anageuka kuwa Mungu wa agano la kale mwenye visasi
 
Hawa waliovuliwa uaskofu na uchungaji nadhani waliwekwa kimkakati na mfumo uliopita na Hawa wamewahi kushiriki kuhalalisha Kufungwa ndoa ya mbunge wa Korogwe Kama sikosei ikimhusisha pia mtoto wa Mbunge wa Arumeru...nadhani hii ni karma kwa tunaofuatililia historia na uzi za jf huu mgogoro wa kiuongozi uliwahi kuletwa humu


Naamini KKKT wameshtukia mchezo wa kuwapa watu wenye serikali kwenye damu uongozi.

Uwongo unakusaidia nini wewe? Huo mgogoro mbona upo hata tangu awamu ya nne.Punguza gubu hata kama ulikuwa humpendi JPM.
 
Halmashauri Kuu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Dayosisi ya Kaskazini Mashariki{DKM} imemsimamisha kazi Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Dkt Steven Munga pamoja na Uchungaji saba kupisha uchunguzi kwa tuhuma mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kushindwa kusimamia mali za Dayosisi hiyo pamoja na ubadhilifu mkubwa wa mamilioni ya fedha.

Kwa Mujibu wa taarifa iliyosomwa kanisani jumapili ya Novemba 7 mwaka huu na nakala kugawanywa Kwa waumini,inaeleza hatua zilizochukuliwa baada ya Mkutano Maalumu wa Halmashauri hiyo uliofanyika oktoba 29 mwaka huu.

Hatua hiyo ni pamoja aliyekuwa Askofu wa Dayosisi hiyo kuvuliwa Uchungaji na hivyo kupoteza sifa ya kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo.

Nakala ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Kaimu Katibu Mkuu Dayosisi ya Kaskazini Mashariki,Mchungaji Godfrey Walalaze ilitaja wachungaji wengine waliochukuliwa hatua ni pamoja na Mchungaji Dk Eberhadt Ngugi ambaye alikuwa Msaidizi wa Askofu na Mdhamini wa Mali amesimamishwa Uchungaji ,Mchungaji James Mwinuka aliyekuwa Katibu Mkuu na Mdhamini wa Mali naye amesimamishwa Uchungaji na Mchungaji Dk Anneth Munga aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo-SEKOMU amesimamishwa Uchungaji.

Wengine ni pamoja na Mchungaji Yambazi Mauya aliyekuwa Mkuu wa Jimbo{DINARI} la Tambarare naye amesimamishwa Uchungaji,Mchungaji Paulo Diu aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Kikristo na Elimu naye amesimamishwa Uchungaji ,Mchungaji Yohana Titu aliyekuwa Chaplain wa Hospital ya Bombo naye amesimamishwa Uchungaji na Rodgers Shehumu aliyekuwa Mtunza Hazina wa Jimbo la Tambarare na Hospital ya Lutindi naye amesimamishwa kazi.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Katibu Mkuu Walalaze ilisema kuwa sababu nyingine zilizopelekea kuchukuliwa hatua kwa wachungaji hao na mtunza hazina wa Jimbo ni pamoja na kutumia vibaya Madaraka yao kulikosababisha uvunjaji wa Katiba KKKT-DKM na kufanya mambo yanayosababisha migongano na kuchochea vurugu na ukosefu wa amani miongoni mwa waumini wa watumishi wa Dayosisi kwa ujumla.

Nakala ya Taarifa hiyo ilisema kuwa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya KKKT-DKM kilichokaa octoba 29 mwaka huu Utondolo, Loshoto kilipitia kwa kina taarifa ukaguzi wa hesabu za Dayosisi kwa kipindi cha mwaka 2019 na mwaka 2020 na kubaini upotevu mkubwa wa fedha umefanyika katika kipindi Cha uongozi wa Askofu Munga.

Hivyo Halmashauri Kuu ilifikia uamuzi wa kumvua Uchungaji na kuwasimamisha kazi watumishi hao kutokana na sababu hizo.

View attachment 2004736View attachment 2004737
Inasikitisha.
Sasa hivi migogoro ndani ya KKKT imekithiri.
 
Hili kanisa linashida mahali

Kule mbeya Kuna askofu alifukuzwa na waumin baada ya kuhamisha makao makuu ya dayosisi yaan mtu mmoja anajiamulia tu

Leo dayisisi ya kaskazin wanavuana uaskofu na uchungaji ukiangalia kiundan mijitu yenye PhD ndio imekuwa mipigaji

Waumin wa hili dhehebu hebu fungeni kumuomba Mungu awaoneshe imani ya kweli ipo wapi

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Umesema neno mkuu.
Huku kwetu Tukuyu, Mbeya, Askofu kasepa na Makao Makuu na kulowea Mbeya.
Na ni kwa faida binafsi.
KKKT imeanza kukosa watumishi wa enzi za baba zetu, watumishi wa wito.
Sasa tuna wafanyakazi waliosomea theolojia.
 
Si wangemuombea toba aendelee na kazi ya kuhubiri neno la mungu?

Hawa wachungaji kumbe fix tu, sisi tukiwa na changamoto kama hizi tukiwaelezea wanatukataza tusichukue uamuzi kama huo badala yake wanatusisitizia kua hilo ni pepo inabidi likemewe

Sasa dayosis nzima imeona kwa msala huu maombi sio suluhu, na usikute wametimuliwa afu kuna mali zimezuiliwa ili kufidia hasara. Au pengine kikao cha dayosis kimeenda mbali kabisa kwa kufungua jalada mahakamani.

Real problems cant be solved by imaginary solution
 
Kanisa la Kinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki (DKMS) limewachukulia hatua mbalimbali viongozi nane kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo kushindwa kusimamia mali za Dayosisi katika uongozi wao.

Sababu nyingine zilizopelekea viongozi hao kusimamishwa ua kuvuliwa uchungaji ni kutumia vibaya madaraka yao kulikosababisha uvunjwaji wa katiba ya kanisa. Aidha, viongozi hao wamedaiwa kufanya mambo yanayosababisha migongano na hivyo kuchochea vurugu na ukosefu wa amani miongoni mwa waumini na watumishi wa dayosisi kwa ujumla.

Waliochukuliwa hatua mbalimbali ni:

1. Dkt. Stephen lsmail Munga, aliyekuwa Askofu wa Dayosisi na Mdhamini wa mali amevuliwa uchungaji na hivyo kupoteza sifa ya kuwa Askofu Mstaafu wa DKMS

2. Mchungaji Dkt. Ebert Hardt Ngugi, aliyekuwa Msaidizi wa Askofu na Madhamini wa mali. amesimamishwa uchungaji

3. Mchungaji James Mwinuka, aliyekuwa Katibu Mkuu na Mdhamini wa mali amesimamishwa uchungaji

4. Mchungaji Dkt. Anneth Munga, aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo- SEKOMU, amesimamishwa uchungaji

5. Mchungaji Yambazi Mauya, Aliyekuwa Mkuu wa Jimbo (Dinari) la Tambarare amesimamishwa uchungaji

6. Mchungaji Paulo Diu, aliyekuwa Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Kikristo na Elimu amesimamishwa uchungaji

7. Mchungaji Yona Titu, aliyekuwa Chaplain wa Hospitali ya Bombo, amesimamishwa uchungaji

8. Rodgers Shehumu, aliyekuwa Mtunza Hazina wa Jimbo la Tambarare na Hosoitali va Lutindi. amesimamishwa kazi.

Katibu Mkuu wa DKMS, Mchungaji Godfrey Walalaze amewasihi waumini kuwa watulivu na kuendelea kuombea amani ya kanisani na dayosisi kwa ujumla.
bishop.jpg


Sent from my itel A16 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom