Mchungaji Martin Luther King Jr wa Marekani hakukaa kimya katika kutetea watu weusi.
Iweje leo inakuwa nongwa kwa Maaskofu wa Baraza Kuu la Katoliki kutetea Tanzania?
Tanzania hii ni yetu sote, na wao ni sehemu ya Tanzania. Wajibu wa kanisa ni kusaidia jamii katika masuala mbalimbali yakiwemo ya kijamii.
Martin Luther King Jr. Aliwatetea watu wanyonge na impact yake ipo mpaka leo.
Hoja nzito nzito lazima zijibiwe kwa uzito huo huo. Huwezi ukasimama kwa dharau na kuanza kuwakebehi, eti tu kwa sababu wewe umewahi kushika wadhifa fulani sehemu fulani.
Mambo ya dynasty yaliwashinda akina Khan kipindi kile cha ujima je, yanaweza kufanyika leo kipindi cha sayansi na teknolojia?
HOJA NZITO HAZIJIBIWI KWA MATAMSHI MEPESI MEPESI.