USSR
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 11,718
- 27,812
Na Askofu Benson Kalikawe Bagonza
KWA WEMA au KWA UBAYA, TUSIMSAHAU MAGUFULI
Miaka minne imepita tangu tangazo la kifo cha Rais wa awamu ya tano, hayati JPM litolewe. Kama kilivyo kitendawili cha umri wa mwanadamu unaanza kuhesabiwa lini (anapoingia tumboni au anapotoka), ndivyo kilivyo kitendawili cha kifo cha JPM (Alikufa siku walipotangaza au alikufa siku aliyokufa). Ukweli ni kuwa hatunaye.
Kwa wema au kwa ubaya, TUSIROGWE tukamsahau Rais Magufuli. Kwa nini?
1. Alipendwa sana kama alivyochukiwa sana. Watu wasio na upande hawakuwa wengi. Hili ni darasa.
2. Alijibebesha mizigo mingi kwa ajili ya taifa. Ikamlemea na kufupisha maisha yake.
3. Alibebeshwa mizigo mingi. Aliwatetea watendaji wasiomtetea na kuwaumiza waliomtetea. Marais wetu wajue, kazi ya rais ni kuwatetea wateule wake waadilifu. Kazi ya wateule ni kumtetea rais (hata kama si mwadilifu).
4. Aliwatisha wala rushwa bila kuitisha rushwa. Alipoondoka wala rushwa uwakalipiza kisasi kwa kubugia rushwa waliyoikosa wakati wa Magufuli.
5. Aliwatisha maaskari wenzake katika vita ya rushwa (media, civil society, opposition, mitandao na wasomi). Maaskari wenzake wakaufyata. Akabaki peke yake. Rushwa ikamshambulia mpaka nyumbani. Alikosa mtetezi.
6. Alimtanguliza Mungu bila kupatana naye. Mungu akampa vyote (madaraka na mamlaka), lakini akamnyima kimoja: Urefu wa maisha. Lakini urefu na ufupi wa maisha si neno. Umeacha nini? Vitu vinasahaulika. Tunu zinadumu.
7. Urais ulimtafuta. Aliponogewa akautafuta. Wapambe wakaushabikia kuliko rais mwenyewe. Sasa wanaimba, eti aliyepo hajawahi kutokea. Ninajua aliyepo anawa-zoom na anajua siku akiondoka watamtukuza ajaye wakisahau asali ya sasa. Mnenepeshe mbuzi-katoliki utamla, lakini mwanadamu ni namba nyingine!
8.JPM kifoni amefanya muujiza mmoja: Waliomchukia hawana furaha na waliompenda hawana furaha. Mwanadamu kiumbe wa ajabu, anayemjua ni muumbaji wake.
8. Kwa kutii kauli yake, “uchaguzi wa 2019 na 2020 ulivurugwa”. Waliochaguliwa na walioshindwa wakakosa furaha milele. Wezi hawakuiba kura, waliiba mfumo. Wataalamu wa TEHAMA ndio wanatuchagulia viongozi. Hata yeye aliondoka bila kujua kama alichaguliwa au la?
9. JPM amelala kaburini. Anaishi mioyoni mwa watu. Mkewe na mtoto watawasha mwenge 2025. Chato na Sengerema kaeni chonjo. Asiye na mwana abebe paka shume!
10. Mambo aliyokosea JPM yanahitaji kurekebishwa (demokrasia). Tusipoyarekebisha, tuna la kujibu mbele za Mungu. Tukiyarekebisha, JPM ana la kujibu mbele za Mungu. Tuchague kwa busara nini cha kufanya. Kwa hakika, MUNGU analipenda hili taifa. Huamini? Lichezee uone. Sitamani kusimama aliposimama mrithi wa JPM.
Raha ya Milele Umwangazie JPM.