Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Karagwe, Dkt. Benson Bagonza, amesema hali ya sasa ya kisiasa nchini, baada ya kuenguliwa kwa Mgombea Urais wa ACT Wazalendo Luhaga Mpina, inathibitisha hitaji kubwa la wadau wa siasa kurudi mezani kujadiliana.
Akizungumza na SAUT DIGITAL, saa chache baada ya Mpina kuzuiwa kuingia katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kurejesha fomu Agosti 27, 2025, Bagonza amesema mfumo wa sasa unaonesha dalili za kuvuruga misingi ya demokrasia na uhuru wa vyombo vya uchaguzi.
“Mambo yote ni magumu sana haya, yanasisitiza kitu kimoja tu ambacho nimekuwa nikikisema- tunahitaji kurudi mezani. Kwa mfano hili la kuengua mgombea, mimi nilitegemea anakwenda kurejesha fomu halafu kama kuna sababu basi Msajili aweke pingamizi huko, siyo Msajili amuengue mgombea. Kazi ya kuengua mgombea siyo ya Msajili ni ya Tume, lakini cha ajabu zaidi pia nikaona Tume ikatoa barua ya kumzuia kabla hata hajaenda, kana kwamba kulikuwa na mawasiliano kati ya Tume na Msajili,” amesema Askofu Bagonza.
Askofu huyo ameongeza kuwa kitendo cha vyombo vinavyotakiwa kuwa huru na vinavyojitegemea kuonekana kushirikiana katika kumzuia mgombea ni ishara ya hatari kwa mustakabali wa uchaguzi.
“Hatutakuwa na uchaguzi ila tutakuwa na siku ya uchaguzi, kwahiyo uchaguzi ni kama umekwisha, tunawashukuru sana WanaCCM wameteua wamemaliza, tusonge mbele lakini uchaguzi ni kama umekwisha. Matokea yake hapo baadaye ni kwamba hakuna mzigo mimi ninaoufahamu hapa duniani kwa kiongozi kama kuongoza watu ambao una mashaka kama walikuchagua, ni mzigo sana”, amesisitiza.
Bagonza amehimiza kuwepo kwa chombo cha maelewano kitakachokutanisha vyama vyote na wadau wa siasa kujadili namna ya kusonga mbele, akibainisha kuwa kutumia nguvu kufanikisha maendeleo badala ya ushawishi ni mzigo mkubwa kwa serikali yoyote.
“Sasa Bunge lilikwishavunjwa kwahiyo hatuna wabunge, lakini bado tuna Mawaziri na hili ni jambo jema kwasababu huwezi kuiacha serikali hewani. Kwahiyo hata sasa tuna wagombea Urais lakini bado tunaye Rais, huwezi kuiacha nchi bila Rais, ni Rais na wakati huohuo ni wagombea, ninadhani ipo haja ya kuitana mezani na kutengeneza mazungumzo