Askofu Bagonza: Ndoa inahitajika...

Askofu Bagonza: Ndoa inahitajika...

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
53,158
Reaction score
104,881
*Kalamu
Baba Askofu Benson Kalikawe Bagonza*

NDOA INAHITAJIKA...

Inahitajika ndoa ya dharula ili maisha yarejee katika hali ya kawaida. Maharusi ni Bwana NGUVU na Bi HEKIMA. Kwa nini ndoa? Jibu ni, ili tuweze kujibu maswali mawili:

1. Kwa nini watu waandamane?
2. Kama wakiandamana, kwa nini
wapigwe?

TUTAFAKARI

1. Mtihani wa Taifa wa darasa la nne ukiwa unaendelea, ikatokea karatasi ya mtihani ikakutwa inafungia vitumbua mtaa wa pili, mtihani unafutwa. Aliyechapa mtihani anakamatwa na kuhojiwa. Muuza vitumbua anakamatwa na kuhojiwa.

Chukulia mtihani wa mwisho wa madaktari na marubani ukivuja au kusingiziwa kuvuja. Utawaacha madaktari hawa waende kupasua wagonjwa au marubani wakarushe ndege?

Karatasi za kura ni nyaraka nyeti. Ni kama risasi. Ikipotea moja toka stoo isijulikane iko wapi, kila kitu kinasimama. Huwezi kujua hiyo risasi itatokezea wapi? Aliyechapa karatasi zetu za kura anaweza kutumiwa kuvuruga nchi. Kwa nini zizagae zagae? Tusikimbilie kuwalaumu wanaoandamana wala kukimbilia kutumia nguvu na mabomu yetu kwa kinachohitaji ndoa kati ya matumizi ya nguvu na matumizi ya hekima.

Nitajibiwa kuwa waandamanaji wanavunja sheria kuandamana kwa amani kudai risasi iliyopotea ipatikane isije ikaingiza nchi katika msiba mkubwa. Wanaonijibu wangetuonyesha risasi iko wapi. Wangetuambia madaktari hawa waliovujishiwa mtihani wanafaa kutibu wagonjwa wetu? Marubani hawa waliofanya mtihani uliovuja watarusha ndege zetu. Tutazipanda ndege hizi? Zitatufikisha?

Mzee Msekwa anasahau tu. Bunge la chama kimoja wakati wa Kambarage wagombea wa ubunge walikuwa wawili kwa alama za NYUMBA na JEMBE. Mijadala ndani ya Bunge ilikuwa mikali na vijijini tulijadili kipi bora kati ya nyumba na JEMBE.

Wanaowatukana mabalozi, wanaokamata wapinzani na kuwaweka ndani wanaongeza msiba kwa Taifa. Kuna mahali tumejikwaa. Wenye hekima wanasema "ukishindwa kuwa mwaminifu basi jitahidi uwe mwangalifu". Haki ya mtu kulia anapoumia haitolewi wala kuondolewa na katiba. Ni takwa la Muumba kwa viumbe wote. Pigeni lakini msizuie watu kulia.

Wengine hatujasahau, Kuna wakati tulikuwa tunabembelezwa kuandamana. Haya ni maoni yangu, nawe una yako. Tujitahidi kuhudhuria harusi ya Be. NGUVU na Bi HEKIMA.
 
Askofu Bagonza ana HEKIMA, na anatumia "CHEO" kutangaza haki kutedeka.

Maandamano ya "AMANI" kesho yanapaswa kuangaliwa na "VIONGOZI WENYE MAMLAKA (Rais Mteule, Rais, NEC, CCM, IGP, MKUU WA MAJESHI, MKUU WA USALAMA WA TAIFA)" kwa jicho la "HAKI", bila kuangalia kwa jicho la "MASLAHI".

Kesho ndio itaamua hatima yao na maisha yao, kama wakitumia jicho la maslahi na kutumia nguvu, badala ya kutumia jicho la haki, basi nchi inaweza kuchafuka na ICC (Mahakama Ya Kimataifa Ya Makosa Ya Jinai) itawaita, na kuna kila dalili ACP Mambosasa akatolewa kama "CHAMBO" kwanza (Wakubwa wote wakajikalia kimya, yeye akaachiwa mpira peke yake uwanjani kwenda kinyume na "WITO/MATAMKO" yanaotolewa na nchi za magharibi na akawakamata viongozi wa upinzani)!!!!

Dunia ya sasa ni kama kijiji, technology ndio imeshika dunia. Kitakacho tokea kesho, basi kabla hakijaisha kitakua kimesambaa dunia nzima.

Kuna "MADIKTETA" wengi sana walitumia nguvu na majeshi makubwa sana, mifano ya kina "ADOLF HITLER, CON. SOLEIMAN, SADDAM HUSSEIN, MOBUTU SSESE SEKO, BOKASSA n.k" leo wako wapi???

Tanzania hatuwezi na hatuna uwezo hata wa kufikia nusu au robo ya "NGUVU Za KIJESHI/PESA" waliokua nayo "MUAMMAR GADAFI au SADDAM HUSSEIN". Leo wako wapi?

*** Its too late, watawala wakubali yaishe. Raia, Mabalozi, NGO, Asasi Za Haki Za Binaadamu, Nchi za Nje n.k hawaukubali utawala huu kuanzia 2015 mpaka sasa. Huwezi ukashindana na dunia nzima peke yako.
 
Mimi Mlutheri ila sasa naelekea kumshangaa Kiongozi wangu wa kiroho yaani yeye ni siasa tuu?

Ninaomba ateuliwe aingie Bungeni ili atimize azma yake bungeni na tumjadili kama mwanasiasa kamili la sivyo ajikite kwenye mambo ya kiroho.

Anyway

Hongera Magufuli,Hongera Mwinyi,Hongera CCM
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
laiti wenye mamlaka wangekuwa na UPEO wa kuelewa BUSARA hizi
Huyo askofu alishakuwa taahila sijui hata upako kama bado anao,
Aligoma kuhusu corona akafunga kanisa na kuzodoa lakini leo hata hana barakoa na hazungumzi kwa nini havai.
 
Baba wa TAIFA alituambia kwamba hakuna umaskini mkubwa Kama umaskini wa akili mm nasema kwa Tanzania ya Sasa wanaounga mkono serikali hii ni wachache Sana ukubali usikubali,Watanzania Wana akili KUBWA KULIKO wanaotuongoza ndio shida ya Sasa huweza kupenda bunge la chama kimoja Wakati wenye Akili kuliko ww waliona umuhimu wa hoja kinzani kwa lengo la kuleta ustawi mzuri wa TAIFA letu lote, Leo mtu Anakuja na technique ya kishamba kuliko kawaida asijue kwamba hata wanaCCM wenye Akili wanamshangaa.
 
Nlimuonya Bagonza mapema kwamba kwa tabia yake hii ya kuchagua upande wa kushabikia huku akiwa kiongozi wa tasisi kama KKKT atakuja kuumia!

Ona sasa anavyoumia
 
NDOA INAHITAJIKA...

Inahitajika ndoa ya dharula ILI maisha yarejee katika hali ya kawaida. Maharusi ni Bwana NGUVU na Bi HEKIMA. Kwa nini ndoa? Jibu ni, ili tuweze kujibu maswali mawili:

1. Kwa nini watu waandamane?
2. Kama wakiandamana, kwa nini
wapigwe?

TUTAFAKARI

1. Mtihani wa Taifa wa darasa la nne ukiwa unaendelea, ikatokea karatasi ya mtihani ikakutwa inafungia vitumbua mtaa wa pili, mtihani unafutwa. Aliyechapa mtihani anakamatwa na kuhojiwa. Muuza vitumbua anakamatwa na kuhojiwa.

Chukulia mtihani wa mwisho wa madaktari na marubani ukivuja au kusingiziwa kuvuja. Utawaacha madaktari hawa waende kupasua wagonjwa au marubani wakarushe ndege?

Karatasi za kura ni nyaraka nyeti. Ni kama risasi. Ikipotea moja toka stoo isijulikane iko wapi, kila kitu kinasimama. Huwezi kujua hiyo risasi itatokezea wapi? Aliyechapa karatasi zetu za kura anaweza kutumiwa kuvuruga nchi. Kwa nini zizagae zagae?

Tusikimbilie kuwalaumu wanaoandamana wala kukimbilia kutumia nguvu na mabomu yetu kwa kinachohitaji ndoa kati ya matumizi ya nguvu na matumizi ya hekima.

Nitajibiwa kuwa waandamanaji wanavunja sheria kuandamana kwa amani kudai risasi iliyopotea ipatikane isije ikaingiza nchi katika msiba mkubwa. Wanaonijibu wangetuonyesha risasi iko wapi. Wangetuambia madaktari hawa waliovujishiwa mtihani wanafaa kutibu wagonjwa wetu? Marubani hawa waliofanya mtihani uliovuja watarusha ndege zetu. Tutazipanda ndege hizi? Zitatufikisha?

Mzee Msekwa anasahau tu. Bunge la chama kimoja wakati wa Kambarage wagombea wa ubunge walikuwa wawili kwa alama za NYUMBA na JEMBE. Mijadala ndani ya Bunge ilikuwa mikali na vijijini tulijadili kipi bora kati ya nyumba na JEMBE.

Wanaowatukana mabalozi, wanaokamata wapinzani na kuwaweka ndani wanaongeza msiba kwa Taifa. Kuna mahali tumejikwaa. Wenye hekima wanasema "ukishindwa kuwa mwaminifu basi jitahidi uwe mwangalifu". Haki ya mtu kulia anapoumia haitolewi wala kuondolewa na katiba.

Ni takwa la Muumba kwa viumbe wote. Pigeni lakini msizuie watu kulia.

Wengine hatujasahau, Kuna wakati tulikuwa tunabembelezwa kuandamana. Haya ni maoni yangu, nawe una yako. Tujitahidi kuhudhuria harusi ya Be. NGUVU na Bi HEKIMA.

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Mimi Mlutheri ila sasa naelekea kumshangaa Kiongozi wangu wa kiroho yaani yeye ni siasa tuu?

Ninaomba ateuliwe aingie Bungeni ili atimize azma yake bungeni na tumjadili kama mwanasiasa kamili la sivyo ajikite kwenye mambo ya kiroho.

Anyway

Hongera Magufuli,Hongera Mwinyi,Hongera CCM
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
Kudai ni siasa tu ni upotoshaji. Labda ungesema na siasa pia.
 
Nasikia eti usipotahiriwa ule uchafu wote unakimbilia kwenye ubongo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom