mr mkiki
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 5,583
- 11,659
Sasa sikiliza...
1. Unaweza kutenda haki kwa niaba
2. Unaweza kuomba radhi kwa niaba
3. Unaweza kusaidia kwa niaba
4. Unaweza kuteseka kwa niaba
5. Unaweza kufa kwa niaba
LAKINI
1.Huwezi kutenda dhambi kwa niaba
2. Huwezi kusingizia mtu kwa niaba
3. Huwezi kuua kwa niaba
4. Huwezi kuteka kwa niaba
5. Huwezi kuiba kwa niaba
Kila mtu atawajibika mbele ya Mungu au shetani wake kwa yale aliyotenda LAKINI hayana kwa niaba. Ukitenda dhambi kwa kutii amri halali, dhambi hiyo ni yako mtendaji, si ya aliyetoa amri hata kama naye ana dhambi kwa kipimo kingine tofauti.
Ukiona uovu ukanyamaza, wewe ni mwovu kuliko anayetenda uovu huo, na wewe ni mbaya kuliko aliyeagiza uovu huo utendeke. UADILIFU ni kutenda usemayo si kusema utendayo. Akemeaye uovu ni bora kuliko atamaniye kutenda wema.
Kwa kuwa mamlaka zote zatoka kwa Mungu, imezipasa mamlaka hizo (Wafalme, Makuhani na Manabii) watambulishwe na tabia ya kutenda haki, kukemea uovu na kuchukia damu isiyo na hatia.
...wabariki viongozi wake
...wake kwa waume na watoto
...hekima umoja na amani
...hizi ni ngao zetu.
Sent using Jamii Forums mobile app