Askofu Bagonza : Maadili ni Nadharia, UADILIFU ni Vitendo.

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,583
11,659
Sasa sikiliza...

1. Unaweza kutenda haki kwa niaba
2. Unaweza kuomba radhi kwa niaba
3. Unaweza kusaidia kwa niaba
4. Unaweza kuteseka kwa niaba
5. Unaweza kufa kwa niaba

LAKINI
1.Huwezi kutenda dhambi kwa niaba
2. Huwezi kusingizia mtu kwa niaba
3. Huwezi kuua kwa niaba
4. Huwezi kuteka kwa niaba
5. Huwezi kuiba kwa niaba

Kila mtu atawajibika mbele ya Mungu au shetani wake kwa yale aliyotenda LAKINI hayana kwa niaba. Ukitenda dhambi kwa kutii amri halali, dhambi hiyo ni yako mtendaji, si ya aliyetoa amri hata kama naye ana dhambi kwa kipimo kingine tofauti.

Ukiona uovu ukanyamaza, wewe ni mwovu kuliko anayetenda uovu huo, na wewe ni mbaya kuliko aliyeagiza uovu huo utendeke. UADILIFU ni kutenda usemayo si kusema utendayo. Akemeaye uovu ni bora kuliko atamaniye kutenda wema.

Kwa kuwa mamlaka zote zatoka kwa Mungu, imezipasa mamlaka hizo (Wafalme, Makuhani na Manabii) watambulishwe na tabia ya kutenda haki, kukemea uovu na kuchukia damu isiyo na hatia.

...wabariki viongozi wake
...wake kwa waume na watoto
...hekima umoja na amani
...hizi ni ngao zetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wakati kauli kama hizi pasipo kukemea moja kwa moja huwa naona sawa na mtu anayemwambia mtoto anayelia akimuaga akienda kazini "nyamaza nitakuletea pipi" wakati unajua fika ukirudi hutomletea hiyo pipi..!!
 
Huyu askofu ni mwanasiasa au alichukua nadhiri ya kuongoza kondoo wa bwana.?
Amekua mwanasiasa kuliko mchunga kondoo
Naomba nikujibu kutokana na hoja zake

"Ukiona uovu ukanyamaza, wewe ni mwovu kuliko anayetenda uovu huo, na wewe ni mbaya kuliko aliyeagiza uovu huo utendeke"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maandiko yanasema "nyinyi si sehemu ya ulimwengu huu".

Ahubiri ufalme wa milele(wa Mungu). Siasa aachie wanasiasa.
 
Huyu askofu ni mwanasiasa au alichukua nadhiri ya kuongoza kondoo wa bwana.?
Amekua mwanasiasa kuliko mchunga kondoo
mpagani huyo kafunga makanisa yote ya KKKT YALIYO CHINI YAKE WATU WASIENDE KUSALI AKIOGOPA CORANA
HAHUBIRI KANISANI KWANI KAYAFUNGA
 
Anaandika Askofu Bagonza :MAADILI ni nadharia
UADILIFU ni Vitendo.

Sasa sikiliza....

1. Unaweza kutenda haki kwa niaba
2. Unaweza kuomba radhi kwa niaba
3. Unaweza kusaidia kwa niaba
4. Unaweza kuteseka kwa niaba
5. Unaweza kufa kwa niaba

LAKINI

1.Huwezi kutenda dhambi kwa niaba
2. Huwezi kusingizia mtu kwa niaba
3. Huwezi kuua kwa niaba
4. Huwezi kuteka kwa niaba
5. Huwezi kuiba kwa niaba

MWISHO WA SIKU

Kila mtu atawajibika mbele ya Mungu au shetani wake kwa yale aliyotenda LAKINI hayana kwa niaba. Ukitenda dhambi kwa kutii amri halali, dhambi hiyo ni yako mtendaji, si ya aliyetoa amri hata kama naye ana dhambi kwa kipimo kingine tofauti.

Ukiona uovu ukanyamaza, wewe ni mwovu kuliko anayetenda uovu huo, na wewe ni mbaya kuliko aliyeagiza uovu huo utendeke. UADILIFU ni kutenda usemayo si kusema utendayo. Akemeaye uovu ni bora kuliko atamaniye kutenda wema.

Kwa kuwa mamlaka zote zatoka kwa Mungu, imezipasa mamlaka hizo (Wafalme, Makuhani na Manabii), watambulishwe na tabia ya kutenda haki, kukemea uovu na kuchukia damu isiyo na hatia.

...wabariki viongozi wake
...wake kwa waume na watoto
...hekima umoja na amani
...hizi ni ngao zetu.
 
Back
Top Bottom