Torch
JF-Expert Member
- Aug 11, 2013
- 1,200
- 1,116
KUZUIA TAHARUKI KUNALETA TAHARUKI
Kuwazuia watu kutoogopa kitu kinachoogopesha ni kuwakosea haki watu hao. Binadamu kamili huogopa. Kutoogopa kinachoogopesha ni kasoro ya kimaumbile hata kama si dhambi.
Hatari huogopesha. Hatari isiyoogopesha si hatari tena. Hatari inayoogopesha imekamilika, siyo feki.
Mwenyezi Mungu anapoagiza TUSIOGOPE haina maana kuwa hakuna hatari. Anasema MSIOGOPE kwa sababu anajua iko hatari.
Kuzuia watu wasiwe na taharuki kwa jambo lenye taharuki ni kusababisha taharuki. Kwa mfano:
1. Kutovaa barakoa katikati ya waliovaa barakoa ni kuzua taharuki.
2. Kutovaa barakoa katika mazishi ya mtu aliyekufa kwa Corona ni kuleta taharuki zaidi.
3. Kuwakejeli wanaotahadharisha juu ya uwepo wa Corona ni kustawisha taharuki.
4. Kuzuia matangazo ya taarifa za Corona au kumilikisha taarifa hizo ni kustawisha taharuki.
5. Kusema hakuna taharuki ni kuchochea taharuki.
6. Kukemea matamko, mahubiri na nyaraka za kuelimisha kuhusu Corona ni kuchochea taharuki.
7. Kuona majeneza mengi airport, misururu ya Coaster na ibada za mazishi kunazua taharuki hata pasipo kutangaza chanzo cha kifo.
8. Kuona hospitali zinatangaza nafasi za kazi za watunza Mortuary kunaleta taharuki.
9. Kuona mafundi majeneza wakitafuta mbao kwa wingi kunaongeza taharuki.
10. Ongezeko la bei ya malimao, tangawizi, vitunguu na asali kunaongeza taharuki.
KWA hiyo taharuki ni sehemu muhimu ya ugonjwa wa Corona. Bila taharuki, Corona haiwi Corona na Elimu haitolewi kikamilifu. Corona bila taharuki haiwezekani. Jitihada za kuondoa taharuki, zinaongeza taharuki. Wanaoshtakiwa kwa kusababisha taharuki ni mashujaa wa vita hii, watastahili nishani ushindi ukipatikana. Zingatia, chukua hatua.