Askofu Bagonza: Kusema inapotakiwa ni bora kuliko kukaa kimya inapotakiwa. Kukemea vibaya ni bora kuliko kupongeza vibaya

God bless you baba askofu, mungu awe nawe pamoja na jamii yako, mungu aibariki kazi ya mikono yako, akupe afya jema na maisha marefu , endelea kumutumikia mungu na taji yakungoja pale parapanda itakapolia
 
Ameandika Askofu Dr Bagonza (PhD)

"Utusamehe Makosa Yetu"
Baba Mtakatifu, Papa Francis, katika ukuu wake na nafasi yake katika Kanisa, alichukua wajibu wa kuomba Msamaha kwa ajili ya mauaji ya Kimbari (Genocide) ya Rwanda. Ilikuwa mwezi Machi 2017.
Makosa ya Kanisa yalikuwa ya aina nne:

1. Baadhi ya Mapadre kugoma kufungua Makanisa ili kuwahifadhi waliokuwa wakiwakimbia wauaji.

2. Baadhi ya Mapadre kuwahifadhi Wakimbizi kisha wakapigia simu wauaji ili waje kuwaua Wakimbizi waliojificha ndani ya Kanisa.

3. Baadhi ya Mapadre na Maaskofu kusifu, kupongeza, na kuunga Mkono juhudi za Rais Habyalimana kabla ya mauaji ya Kimbari.

4. Baadhi ya Mapadre na Maaskofu kukaa kimya kabla ya mauaji, wakati wa mauaji na baada ya mauaji.

Haya hayakufanywa na Kanisa Katoliki peke yake tu, bali Makanisa mengi Nchini humo. Kanisa Katoliki linaonekana kwa sababu ya ukubwa wake. Viongozi wa Makanisa mengine wanapaswa pia kuomba msamaha.

TUNAJIFUNZA NINI?
- Kimya kinaua
- Kuunga mkono kunaua
- Kukaa katikati kunaua

Kwa hiyo, kusema inapotakiwa ni bora kuliko kukaa kimya inapotakiwa. Kukemea vibaya ni bora kuliko kupongeza vibaya.

61877116_668113893616235_3828212777374187520_n.jpg
 
Kwa makosa ya wenzetu tujifunze.
Kinga ni bora kuliko tiba
Polepole, Bashiru, Magufuli, Kipilimba, Sirro , Makonda, Jerry Muro, Ali Hapi and the rest of the JPM aircrew haviwahusu, wamebarikiwa kuliko watanzania wote na uzao wa matumbo yao umebarikiwa!.
 
Huyu ndie mtu wa Mungu

Sio Pengo na wenzake wanafiki wakubwa
Kwa kweli Pengo hasomeki tena kwa wino wa bluu. Anapunguza morali ya waumini wa RC na kutuweka kwenye danger zone. Hawezi kupongeza vizur bora akae kimya. Ona sasa anavyotukanwa mitandaoni.
 
Back
Top Bottom