Askofu Bagonza: Kusema inapotakiwa ni bora kuliko kukaa kimya inapotakiwa. Kukemea vibaya ni bora kuliko kupongeza vibaya

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,611
86,305
Anaandika baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
_____
"Utusamehe Makosa Yetu"

Mwezi Machi mwaka 2017 Baba Mtakatifu, Papa Francis, katika ukuu wake na nafasi yake katika Kanisa, alichukua wajibu wa kuomba msamaha kwa ajili ya mauaji ya kimbari (genocide) ya Rwanda yaliyotokea mwaka 1994.

Makosa ya kanisa yalikuwa ya aina nne:

1. Baadhi ya mapadre kugoma kufungua makanisa ili kuwahifadhi waliokuwa wakiwakimbia wauaji.

2. Baadhi ya mapadre kuwahifadhi wakimbizi kisha wakapigia simu wauaji ili waje kuwaua wakimbizi waliojificha ndani ya kanisa.

3. Baadhi ya mapadre na maaskofu kusifu, kupongeza, na kuunga mkono juhudi za Rais Habyarimana kabla ya mauaji ya kimbari.

4. Baadhi ya mapadre na maaskofu kukaa kimya kabla ya mauaji, wakati wa mauaji na baada ya mauaji.

Haya hayakufanywa na Kanisa Katoliki peke yake tu, bali makanisa mengi nchini humo. Kanisa Katoliki linaonekana kwa sababu ya ukubwa wake, lakini viongozi wa makanisa mengine wanapaswa pia kuomba msamaha.

TUNAJIFUNZA NINI?

Kimya kinaua
Kuunga mkono kunaua
Kukaa katikati kunaua

Kwa hiyo, kusema inapotakiwa ni bora kuliko kukaa kimya inapotakiwa. Kukemea vibaya ni bora kuliko kupongeza vibaya.!

1574175490291.png



 
Askofu Boganza amepoteza mwelekeo sasa

Hajui ashike lipi kati ya dini na siasa

Moja ya kazi ya viongozi wa kiroho ni kuonya, pale wanapoona kuna hatarisho la amani.. Hao wanasiasa ndo kutwa nzima wanawaomba viongozi wa dini kuombea amani, sasa anapoombea amani, akiona kuna kinachohatarisha ni wajibu wake kuonya, kushauri na kukemea..

Wale waliokutana jana na Bashite na kutoa controversial opinions, ulitoa comment yeyote kupinga au kushangaa..?
 
Back
Top Bottom