Askofu Bagonza atoa pongezi na ujumbe mzito kwa CHADEMA

Sanyambila

JF-Expert Member
Jan 24, 2018
339
457
Ujumbe kutoka kwa Baba Askofu Dr Benson Bagonza PhD..

HONGERA CHADEMA, lakini...

Nawapongeza wana Chadema kwa kumaliza uchaguzi. Nawapongeza viongozi wote walioshiriki, wakashindwa na kushinda. Mlichokozwa, hamkuchokozeka. Waleteeni watanzania fikra mpya, hoja mpya na siyo Tanzania mpya.
Tanzania ni moja isiyo na mipaka mipya na kwa hiyo Tanzania siyo mpya.

Mnapoanza awamu mpya zingatieni haya:

1. Taifa imara linahitaji Chama tawala imara.

2. Chama tawala imara kinahitaji chama mbadala/Pinzani imara.

3. Serikali imara inahitaji chama tawala na chama pinzani imara.

4. Bunge imara linahitaji chama tawala imara, serikali imara na kambi ya upinzani imara. Nje ya haya, hakuna spika imara.

5. LAKINI, uimara wa chama cha upinzani hautokani na uimara wa chama tawala. Msibweteke.

6. Mkutano wenu umeonyesha haya:

- Chadema ina mashabiki wengi kuliko wanachama. CCM ina wanachama wengi kuliko mashabiki.

- Kazi ya Chadema ni kubadili mashabiki kuwa wanachama, na ya CCM ni ya kuongeza mashabiki bila kupoteza wanachama. Msichukiane, msipendane, msimalizane bali mjifunze kuishi na hali msiyoweza kuibadilisha.

- Wanachama wanapenda kuchagua viongozi wao. Hujuma kutoka wapinzani wenu zina nguvu sawa hujuma za kutengeneza wenyewe. Jilindeni na chachu ya ubaguzi, ukanda, U-wenyewe na ubabe. Haya ni mabaya kwa watani wenu, hayawezi kuwa mazuri ndani yenu.

7. Kubalini bila uchungu kuwa, hakuna chama cha siasa Tanzania chenye uwezo wa kushinda uchaguzi kwa kutegemea kura za wanachama wake tu. Kazi ya kushawishi haiepukiki. Kulazimishana ni kubaka demokrasia. Hakuna anayezaliwa akiwa mzalendo au msaliti. Kuna wakati Yuda anahitajika ili kuujua uimara wako. Bila ushirikiano, kuna chama pinzani cha milele na chama tawala cha milele.

8. Haja ya kuwa na taasisi imara kuliko kuwa na viongozi/watawala imara ni kubwa sasa kuliko huko nyuma. Hakuna taasisi imara nje ya KATIBA MPYA inayolipatia taifa tume huru ya uchaguzi, bunge huru, mahakama huru, asasi huru za kiraia, media huru na wananchi walio huru. Hofu ni adui wa maendeleo.
Amani endelevu imo ndani ya tumbo la katiba mpya.

Tanzania yenye amani ni tunda la mshikamano wenye haki ndani yake. Msichoke kutafuta maridhiano ndani na nje yenu.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Ni confused bishop.wa KKKT nadhani Ni mental case kanisa lim
mchukukie serious asje siku moja akatupa majoho akatembea uchi madhabahuni.

Anahitaji treatment na counselling ya kiroho na kisaikolojia kuna tatizo
Mkuu, umetupa mawe container nzima, ngoja Baba Askofu au wapambe wake waje kujibu hoja.
 
Ni chama gani huyo askofu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Bagonza Ni Chadema alikuwa team Lowasa.Lowasa aliwaingiza pori viongozi wengi wa dini kwa kuwagawagawia pesa .Huyo nimmmoja wa waliokula pesa za Lowasa

Kabla Lowasa kujitosa na kurubuni viongozi wa dini ,viongozi wengi wa dini walikuwa mbali na siasa ilikuwa wao na dini dini na wao .Lowasa aliharibu Sana baadhi ya viongozi wa dini .Wengi maskini ushiriki wao kwenye siasa ulikuwa kwa Mara ya kwanza tokea Wawe viongozi wa dini.Maburungutu ya pesa na misaada laghai ikawapofusha

Nakumbuka askofu mmoja Yuko kinondoni alitangaza kanisani kuwa hili.kanisa sisi Ni UKAWA tuko na Lowasa asiyetaka aondoke kanisani

Lowasa kugawa hela kwa baadhi ya viongozi wa dini wengine wakakengeuka wakaona ohh kumbe kushabikia siasa kunalipa.Wengine wamejirudi Bagonza kabaki huko huko akitarajia siku za mgao wa pesa zaweza Rudi kaacha kusubiria kurudi kwa Yesu Mara ya pili anasubiria kurudi kwa mgao wa pesa Mara ya pili
 
"Ushauri Mzuri ila pia mimi namshauri kama anaona anaweza siasa aje kwenye siasa kama Dr Slaa alivyofanya kipindi kile."

Mkuu sijapata ushauri wako, unataka aje kwenye siasa aache kazi yake ya kuhubiri neno, au ahubiri neno akiwa kwenye siasa pia? Slaa aliacha upadri ili aingie kwenye siasa? Weka vizuri hilo.
 
Askofu Bagonza ni mwiba kwa watawala watemi, sio kama viongozi wengine wa dini wanaolinda ugali na matumbo yao (Kufikia hatua wapo radhi wapindishe maandiko), na kujitia "UPOFU" kwa haya yanaoendelea nchini.

 
Back
Top Bottom