Askofu amshangaa Mbunge Lema kutotambua mwafaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu amshangaa Mbunge Lema kutotambua mwafaka

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kishongo, Jul 12, 2011.

 1. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Askofu wa Kanisa la Blessing Alter lililopo mkoani Arusha, Isaya Sizya, amesema anashangazwa na hatua ya Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kukataa mwafaka uliofikiwa hivi karibuni na kuondoa chuki na hofu miongoni mwa wakazi wa Arusha.

  Pia askofu alimtaka Mbunge huyo kutimiza ahadi zake alizozitoa wakati wa uchaguzi ambazo alidai kuwalaghai wananchi kuzitekeleza ndani ya miezi sita.
  Alisema Lema alipokuwa kwenye kampeni za uchaguzi aliahidi kwa wananchi kujenga kituo kikuu cha mabasi Ngulelo na Kisongo, jengo la Machinga Complex, hospitali kubwa tatu, mfumo wa majitaka na barabara.

  Alisema tangu alipoingia madarakani hajawahi kuitisha mkutano na wananchi na kuwaeleza ahadi ngapi amezitekeleza badala yake amekuwa akiendesha siasa za majitaka ambazo hazilengi kuleta maendeleo badala yake zinaleta chuki kwa madiwani na wananchi.
  Akizungumza na waandishi wa habari jana, Askofu Sizya alisema viongozi wa dini walikuwa wakifunga na kusali juu ya amani mkoani hapa na kusisitiza kuwa viongozi hao hawataki kuona damu ya wanaArusha ikirudia kumwagika tena.

  Askofu Sizzya alisema Lema anapaswa kuacha siasa za vurugu na vitisho kwa madai ya kutotambua mwafaka wa kumtambua Meya, Gaudence Lyimo na Naibu Meya Estomi Mallah.

  Alisema kupinga mwafaka ni kuendeleza unazi wa kisiasa ambao hauna maana hivyo Lema anapaswa kuheshimu makubaliano ya mwafaka ya viongozi wengine yaliyofuata taratibu zote na moja ya sifa ya kiongoi bora ni kuheshimu watu na viongozi wengine.

  Source: IPP MEDIA
   
 2. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Mbona hasemi kwa nn anamshangaa! Huyu askofu kama haelezi kinagaubaga kwa nini anamshangaa Lema nitamshangaa zaidi yeye. Mwafaka wa 'magumashi' wa kazi gani kwa Lema na wapenda maendeleo na demokrasia ya kweli?
   
 3. t

  tumpale JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 201
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  haya makanisa ya voda fasta uaskofu unapatikanaje, maana mtu anaweza akaamka akajiita askofu, tusifedheheshe tittle ya uaskofu.
   
 4. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu mchungaji namfahamu aliandaa tamasha mziki Wa Injili kuchangia yatima kuna mama mmoja wa UN alimsaidia hela akala alikuwa na kesi ya kula hela huyo njaa inamsumbua tu.QUOTE=Kishongo;2217491]Askofu wa Kanisa la Blessing Alter lililopo mkoani Arusha, Isaya Sizya, amesema anashangazwa na hatua ya Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kukataa mwafaka uliofikiwa hivi karibuni na kuondoa chuki na hofu miongoni mwa wakazi wa Arusha. Pia askofu alimtaka Mbunge huyo kutimiza ahadi zake alizozitoa wakati wa uchaguzi ambazo alidai kuwalaghai wananchi kuzitekeleza ndani ya miezi sita.Alisema Lema alipokuwa kwenye kampeni za uchaguzi aliahidi kwa wananchi kujenga kituo kikuu cha mabasi Ngulelo na Kisongo, jengo la Machinga Complex, hospitali kubwa tatu, mfumo wa majitaka na barabara. Alisema tangu alipoingia madarakani hajawahi kuitisha mkutano na wananchi na kuwaeleza ahadi ngapi amezitekeleza badala yake amekuwa akiendesha siasa za majitaka ambazo hazilengi kuleta maendeleo badala yake zinaleta chuki kwa madiwani na wananchi.Akizungumza na waandishi wa habari jana, Askofu Sizya alisema viongozi wa dini walikuwa wakifunga na kusali juu ya amani mkoani hapa na kusisitiza kuwa viongozi hao hawataki kuona damu ya wanaArusha ikirudia kumwagika tena. Askofu Sizzya alisema Lema anapaswa kuacha siasa za vurugu na vitisho kwa madai ya kutotambua mwafaka wa kumtambua Meya, Gaudence Lyimo na Naibu Meya Estomi Mallah. Alisema kupinga mwafaka ni kuendeleza unazi wa kisiasa ambao hauna maana hivyo Lema anapaswa kuheshimu makubaliano ya mwafaka ya viongozi wengine yaliyofuata taratibu zote na moja ya sifa ya kiongoi bora ni kuheshimu watu na viongozi wengine.Source: IPP MEDIA[/QUOTE]
   
 5. by default

  by default JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
   
 6. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Mpaka viongozi wa dini wanawashangaa CDM, Baba Askofu endelea kuhubiri Amani ili nchi yetu isingie kwenye vita
   
 7. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  kishongo@ work.
  ndugu mmiliki wa "bold" unaabudu mungu wa wapi? muafaka haukubaliki.. tunchokitaka ni haki ifuatwe na tuone "sauti ya wengi sauti ya mungu" na mamlaka iliyowekwa na mungu na yenye baraka zote
   
 8. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Unanikumbusha mbali sana mkuu!mwaka 2005 viongozi wa dini ya kikristu waliposema JK ni chaguo la mungu waislamu na wana CCM walifurahi sana na ilipofika 2010 waliposema JK hafai wakaitwa wadini!!kichekesho!na wewe unarudia yale yale maaskofu wanakuwa wazuri tu pale wanapoikosoa CHADEMA,wakiisifu mnawaita wadini!!kichekesho kingine!
   
 9. m

  matawi JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  watu wa dini kutaneni mweke vigezo vya mtu kuitwa askofu maana mtu akiamka anaanza kujiita askofu tayari anajua magazeti yatamwandika
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  nchi hii kila mtu anashangaa tu!!! bado mimi
   
 11. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  duh! Huyo Askofu nina mashaka nae...
   
 12. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #12
  Jul 12, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wana Arusha kweli waliingia mkenge kwa Lema, kumbe aliwapa ahadi zote hizo ? kwa kweli hana uwezo hata wakutekeleza 1%, jamaa itabidi aililie serikali ili imtekelezee hayo anayo yataka, la sivyo imekula kwake na kwa wana arusha
   
 13. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Wakiristo mkachukia?
   
 14. k

  kindondechi New Member

  #14
  Jul 12, 2011
  Joined: May 11, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nani kamvalisha Dr.Hilo shati?naomba amvue haraka
   
 15. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #15
  Jul 12, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Leo nilikuwa sijacheka..ila imebidi. Nashukuru mkuu, you made my day!!
   
 16. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #16
  Jul 12, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  huyu askofu hili ni tamko la pili anatoa la kwanza alilipwa na Chatanda akawakemea maaskofu wa arusha kwa kupinga muafaka leo kapewa fedha na madiwani wa cdm naibu meya mala na katibu wa madiwani wa cdm kujaribu kuzuia hukumu yao inayosubiriwa isiwe ngumu
  Mungu atakuathibu kwa kutumia madhabau yake kuganga njaa badala ya kueneza injili
   
 17. i

  in and out Member

  #17
  Jul 12, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  big up, askofu. kwenye siasa wameingia wahuni na wendawazimu tuwe macho taifa letu lisiangamie.
   
 18. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #18
  Jul 12, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hivi ili swala la Arusha mwisho wake sijui itakuaje
   
 19. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #19
  Jul 12, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Huyu Askofu sasa anataka watu tumkosee Mungu bure. Watu wetu wameuawa kwa risasi, wengine vilema, huku madiwani wanagawana vyeo then Askofu Isaya anasema eti muafaka umepatikana. Watumishi wa Mungu kuweni makini kama kweli mnawachunga kondoo wa Bwana.
   
 20. D

  Derimto JF-Expert Member

  #20
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ngoja nimchane huyu bishop feki namfahamu vizuri sana isaya aliyeoa mwanamke aliyemzidi umri ambaye alifiwa na wazazi wake akaachiwa mali kidogo ambazo isaya alitumia vibaya na kuwafanya waishi kimasikini zaidi na kuahamia dhehebu la EAGT kama mchungaji na baada ya kuona vurugu zake zimezidi wakamchoka na ndipo akaachia kanisa alilokuwa analichunga la EAGT sanawari kwa kuwaambia washirika kila moja aende anakotaka yeye anavunja kanisa na kuendeleza tabia ya kuomba omba na kuwatapeli watu mbalimbali hapa mjini na hata kukopa na kutolipa madeni yake na hivyo kutafauta wadhili wa kujikingiliza na tabia zake hizo mpaka sasa anajiita askofu kwa kifupi ni mtu wa tamaa sana na huwa hakatai mwaliko wa harusi yoyote anapenda sana kujulikana hana lolote na kama ndiyo askofu wa kishongo hata sishangai maana nadhani akili zao zinafanana
   
Loading...