Ally Msangi
JF-Expert Member
- Jun 29, 2010
- 608
- 120
ASKOFU wa Kanisa la Evangelical Brotherhood Church Of Tanzania (EBCT), Rabbi Mwakanani, amempoza mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, kumtaka kuyakubali matokeo ili kuliepusha taifa kuingia kwenye machafuko, kwa kuwa yeye na chama chake wamekuwa na ushawishi mkubwa kwa wananchi.
Akizungumza katika ibada maalumu ya kuwaombea amani viongozi walioteuliwa katika Uchaguzi Mkuu, alisema kitendo chake cha kugomea matokeo hayo ni dalili inayoweza kusababisha chuki miongoni mwa jamii.
Askofu Mwakanani alisema katika hali ya kawaida ya binadamu si rahisi kukabili changamoto zinazojitokeza baada ya kufanya kazi kubwa, lakini kwa kuwa kila jambo linalofanywa na binadamu husimamiwa na Mungu, basi kiongozi huyo anapaswa kumwachia Mungu.
Hakuna asiyejua kuwa uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa wa kipekee ulioambatana na matukio mengi, huku wananchi wakijenga imani kubwa kwa baadhi ya wagombea, haitoshi kuamini kwa njia ya kawaida kama kweli haki ilitendeka katika mchakato wote, lakini yote hayo yanapaswa kusahaulika, kwani kuendelea kushikilia misimamo ya namna hiyo kunaweza kusababisha madhara makubwa katika jamii, alisema.
Aidha, alisema viongozi walioshinda na wale walioshindwa wanapaswa kuketi pamoja na kujadili mambo yaliyofungamana na dhamira zao kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi waliowachagua.
Alisema ridhaa waliyopewa viongozi hao na wananchi si utashi wa kibinadamu, bali umetokana na nguvu ya Mwenyezi Mungu, ambapo viongozi wa madhehebu ya dini walikesha kwenye maombi ili apatikane kiongozi mwenye ridhaa ya Mungu.
Ningepata fursa ya kukutana na Dk. Slaa ningemshauri kuwa Mungu kamuwekea akiba kwa miaka mitano ijayo anapaswa kuwa mvumilivu katika siasa kwa hali hii anatufanya Watanzania tuishi kwa hofu, ili tuishi kwa amani Dk. Slaa akubali matokeo, alisema Askofu Mwakanani.

Ni kweli hawa wanojiita watumishi wa Mungu na wenyewe ni wachakachauji wa imani. Huyu "Rabbi" ni myahudi au nini? Jamani hivi kukataa matokeo ya wizi na dhuruma kutaletaje vurugu na machafuko? Ina maana kila mwaka mambo yakijirudia tupuuze tu? Huyo Mungu gani anayehalalisha dhuruma? Basi hakuna haja ya uchaguzi tuwe tunaomba Mungu anatuletea viongozi. Si ameishawapanga tayari. Huyo Mungu mimi namkataa.kwa nini haw viongozi wa Dini wanahubiri upande mmoja tu, kwa nini wasingeanza kwa JK na Genge lake kuwahambia kuwa wizi ni dhambi? na watubu,
hivi nguvu ya CCM na genge jima la mafisadi linaogopwa hata na viongozi wa dini?
Mimi nadha huyo mchungaji kama yeye ni mtu wa Mungu basi angesimama kwenye haki na kumwambia Dr Slaa Haiuridhie haki yake
Wizi ni dhambi.
askofu hebu hubiria hao ccm kwanza nikuelewe
ASKOFU wa Kanisa la Evangelical Brotherhood Church Of Tanzania (EBCT), Rabbi Mwakanani, amempoza mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, kumtaka kuyakubali matokeo ili kuliepusha taifa kuingia kwenye machafuko, kwa kuwa yeye na chama chake wamekuwa na ushawishi mkubwa kwa wananchi.
Akizungumza katika ibada maalumu ya kuwaombea amani viongozi walioteuliwa katika Uchaguzi Mkuu, alisema kitendo chake cha kugomea matokeo hayo ni dalili inayoweza kusababisha chuki miongoni mwa jamii.
Askofu Mwakanani alisema katika hali ya kawaida ya binadamu si rahisi kukabili changamoto zinazojitokeza baada ya kufanya kazi kubwa, lakini kwa kuwa kila jambo linalofanywa na binadamu husimamiwa na Mungu, basi kiongozi huyo anapaswa kumwachia Mungu.
Hakuna asiyejua kuwa uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa wa kipekee ulioambatana na matukio mengi, huku wananchi wakijenga imani kubwa kwa baadhi ya wagombea, haitoshi kuamini kwa njia ya kawaida kama kweli haki ilitendeka katika mchakato wote, lakini yote hayo yanapaswa kusahaulika, kwani kuendelea kushikilia misimamo ya namna hiyo kunaweza kusababisha madhara makubwa katika jamii, alisema.
Aidha, alisema viongozi walioshinda na wale walioshindwa wanapaswa kuketi pamoja na kujadili mambo yaliyofungamana na dhamira zao kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi waliowachagua.
Alisema ridhaa waliyopewa viongozi hao na wananchi si utashi wa kibinadamu, bali umetokana na nguvu ya Mwenyezi Mungu, ambapo viongozi wa madhehebu ya dini walikesha kwenye maombi ili apatikane kiongozi mwenye ridhaa ya Mungu.
Ningepata fursa ya kukutana na Dk. Slaa ningemshauri kuwa Mungu kamuwekea akiba kwa miaka mitano ijayo anapaswa kuwa mvumilivu katika siasa kwa hali hii anatufanya Watanzania tuishi kwa hofu, ili tuishi kwa amani Dk. Slaa akubali matokeo, alisema Askofu Mwakanani.
Tulikueleza padre Slaa huyawezi mambo hayo sasa umekiona.
Ukubali , ukatae bao lipo pale pale. Tumuombe tu Kikwete akupe viti vyake vya Ikulu kama alivyofanya Dr Shein kwa Mzee Juma Duni