Elections 2010 Askofu ampoza Dk. Slaa

Ally Msangi

JF-Expert Member
Jun 29, 2010
609
119
ASKOFU wa Kanisa la Evangelical Brotherhood Church Of Tanzania (EBCT), Rabbi Mwakanani, amempoza mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, kumtaka kuyakubali matokeo ili kuliepusha taifa kuingia kwenye machafuko, kwa kuwa yeye na chama chake wamekuwa na ushawishi mkubwa kwa wananchi.

Akizungumza katika ibada maalumu ya kuwaombea amani viongozi walioteuliwa katika Uchaguzi Mkuu, alisema kitendo chake cha kugomea matokeo hayo ni dalili inayoweza kusababisha chuki miongoni mwa jamii.

Askofu Mwakanani alisema katika hali ya kawaida ya binadamu si rahisi kukabili changamoto zinazojitokeza baada ya kufanya kazi kubwa, lakini kwa kuwa kila jambo linalofanywa na binadamu husimamiwa na Mungu, basi kiongozi huyo anapaswa kumwachia Mungu.

“Hakuna asiyejua kuwa uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa wa kipekee ulioambatana na matukio mengi, huku wananchi wakijenga imani kubwa kwa baadhi ya wagombea, haitoshi kuamini kwa njia ya kawaida kama kweli haki ilitendeka katika mchakato wote, lakini yote hayo yanapaswa kusahaulika, kwani kuendelea kushikilia misimamo ya namna hiyo kunaweza kusababisha madhara makubwa katika jamii,” alisema.

Aidha, alisema viongozi walioshinda na wale walioshindwa wanapaswa kuketi pamoja na kujadili mambo yaliyofungamana na dhamira zao kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi waliowachagua.

Alisema ridhaa waliyopewa viongozi hao na wananchi si utashi wa kibinadamu, bali umetokana na nguvu ya Mwenyezi Mungu, ambapo viongozi wa madhehebu ya dini walikesha kwenye maombi ili apatikane kiongozi mwenye ridhaa ya Mungu.

“Ningepata fursa ya kukutana na Dk. Slaa ningemshauri kuwa Mungu kamuwekea akiba kwa miaka mitano ijayo anapaswa kuwa mvumilivu katika siasa…kwa hali hii anatufanya Watanzania tuishi kwa hofu, ili tuishi kwa amani Dk. Slaa akubali matokeo,” alisema Askofu Mwakanani.
 
Hassan J. Mosoka

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
682
321
Askofu umethubutu!
ingawa kwa kweli maaskofu wangu mnaponishangaza ni pale mnaposhindwa kutoa huduma ya kinabii kuwasaidia viongozi wanaoingia madaraka kwa njia za kutatanisha kama ilivyotokea uchaguzi wa mwakahuu, kuwa ni lazima wakubali nao pia kusoma alama za nyakati badala ya kuwapiga mabomu watanzania wasio hatia.
Kusema si utashi wa kibinadamu sijui umemaaanisha nini? wako viongozi wengi walioingia madarakani kwa utashi wa kibinadamu akiwepo Sauli katika taifa la wayahudi. Huu uchaguzi wa Tanzania unathibitishaje kuwa kuwa watawala hawakuingia kwa utashi wa kibinadamu????? Ikiwa tumeona kila aina ya maigizo kabla hawajaingia!! Wakuu wa dini tumeini madhabahu kwa hofu ya Mungu mwenye nguvu.
Nawasilisha
ASKOFU wa Kanisa la Evangelical Brotherhood Church Of Tanzania (EBCT), Rabbi Mwakanani, amempoza mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, kumtaka kuyakubali matokeo ili kuliepusha taifa kuingia kwenye machafuko, kwa kuwa yeye na chama chake wamekuwa na ushawishi mkubwa kwa wananchi.

Akizungumza katika ibada maalumu ya kuwaombea amani viongozi walioteuliwa katika Uchaguzi Mkuu, alisema kitendo chake cha kugomea matokeo hayo ni dalili inayoweza kusababisha chuki miongoni mwa jamii.

Askofu Mwakanani alisema katika hali ya kawaida ya binadamu si rahisi kukabili changamoto zinazojitokeza baada ya kufanya kazi kubwa, lakini kwa kuwa kila jambo linalofanywa na binadamu husimamiwa na Mungu, basi kiongozi huyo anapaswa kumwachia Mungu.

“Hakuna asiyejua kuwa uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa wa kipekee ulioambatana na matukio mengi, huku wananchi wakijenga imani kubwa kwa baadhi ya wagombea, haitoshi kuamini kwa njia ya kawaida kama kweli haki ilitendeka katika mchakato wote, lakini yote hayo yanapaswa kusahaulika, kwani kuendelea kushikilia misimamo ya namna hiyo kunaweza kusababisha madhara makubwa katika jamii,” alisema.

Aidha, alisema viongozi walioshinda na wale walioshindwa wanapaswa kuketi pamoja na kujadili mambo yaliyofungamana na dhamira zao kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi waliowachagua.

Alisema
ridhaa waliyopewa viongozi hao na wananchi si utashi wa kibinadamu, bali umetokana na nguvu ya Mwenyezi Mungu, ambapo viongozi wa madhehebu ya dini walikesha kwenye maombi ili apatikane kiongozi mwenye ridhaa ya Mungu.

“Ningepata fursa ya kukutana na Dk. Slaa ningemshauri kuwa Mungu kamuwekea akiba kwa miaka mitano ijayo anapaswa kuwa mvumilivu katika siasa…kwa hali hii anatufanya Watanzania tuishi kwa hofu, ili tuishi kwa amani Dk. Slaa akubali matokeo,” alisema Askofu Mwakanani.
 
Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
10,293
5,856
Wizi ni dhambi.
askofu hebu hubiria hao ccm kwanza nikuelewe
 
TzPride

JF-Expert Member
Nov 2, 2006
2,617
1,162
Anataka Slaa awe mnafiki asema nimeyakubali wakati haiakubali?! Kwani lazima aseme, si anaweza kataa tu na mambo yakaendelea kama wezi walivyo panga? Ya nini Dr. Slaa ajifanye mnafiki bwana, ati nimeyakubali. Huku kukubali kubali ndio tunaendeleza dhana ya uchakachuaji.

Go to hell, the so called askofu.
 
Kituko

JF-Expert Member
Jan 12, 2009
9,559
9,251
kwa nini haw viongozi wa Dini wanahubiri upande mmoja tu, kwa nini wasingeanza kwa JK na Genge lake kuwahambia kuwa wizi ni dhambi? na watubu,
hivi nguvu ya CCM na genge jima la mafisadi linaogopwa hata na viongozi wa dini?
Mimi nadha huyo mchungaji kama yeye ni mtu wa Mungu basi angesimama kwenye haki na kumwambia Dr Slaa Haiuridhie haki yake
 
MTWA

JF-Expert Member
Aug 5, 2009
1,155
159
Viongozi wetu wa Dini ni wanafiki wakubwa sana,

kama hawana hoja ni vema wakakaa kimya kama viongozi wa dini zingine si waige? ya nini kujipendekeza kwa wezi! naona hawana lolote zaidi ya kujikomba kwa JK eti nao wanatibu majeraha, Yepi hayo?

Majeraha aliyeleta ni JK na kundi lake na ndiye anayetakiwa kukiri uhalifu, ufisadi na wizi wake pamoja na dhambi kubwa ya uwongo na usingiziaji aliyofanya kuwa wapinzani wanaleta udini, na hali wao CCm ndo wanatutumia msg za udini kila wakati

Hawa maaskofu naona hawana elimu ni kama wananchi tu wanaolalamika hali mbaya lakini wakisema viongozi ni wazuri.
lazima sasa tuwe makini sna na hawa viongozi wa dini. Wapo wanaotegemea sana viongozi hawa Corrupt,
Wapo wanaotegemea kupata vitu fulani kutoka kwao mathalani vibali mbalimbali na misamaha, wapo ambao shughuli zao pia zina utata hivyo lazima waunge mkono waizi huu,
na wengine hawaelewi wanachokitenda ni kama kondoo wa Tambiko tu

Wanapaswa kusema ukweli na kuhimiza maendeleo na mabadiliko tu
 
sensa

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
397
20
Wamwache Slaa aamue anachotaka kufanya wasituletee unafiki hapa,mamluki tu hao.
 
Mfamaji

JF-Expert Member
Nov 6, 2007
6,631
1,903
Kwani wa kuhubiriwa aache dhambi ni nani. Msafi au mwenye dhambi?

Maaskofu acheni unafiki , wengine ni maaskofu wa kujipa tu hamna lolote .Wahubirieni CCM waache uovu Tanzania ni sio Chedema . You can go to hell
 
3D.

JF-Expert Member
Sep 7, 2010
1,013
279
ASKOFU wa Kanisa la Evangelical Brotherhood Church Of Tanzania (EBCT), Rabbi Mwakanani, amempoza mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, kumtaka kuyakubali matokeo ili kuliepusha taifa kuingia kwenye machafuko, kwa kuwa yeye na chama chake wamekuwa na ushawishi mkubwa kwa wananchi.

Akizungumza katika ibada maalumu ya kuwaombea amani viongozi walioteuliwa katika Uchaguzi Mkuu, alisema kitendo chake cha kugomea matokeo hayo ni dalili inayoweza kusababisha chuki miongoni mwa jamii.

Askofu Mwakanani alisema katika hali ya kawaida ya binadamu si rahisi kukabili changamoto zinazojitokeza baada ya kufanya kazi kubwa, lakini kwa kuwa kila jambo linalofanywa na binadamu husimamiwa na Mungu, basi kiongozi huyo anapaswa kumwachia Mungu.

“Hakuna asiyejua kuwa uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa wa kipekee ulioambatana na matukio mengi, huku wananchi wakijenga imani kubwa kwa baadhi ya wagombea, haitoshi kuamini kwa njia ya kawaida kama kweli haki ilitendeka katika mchakato wote, lakini yote hayo yanapaswa kusahaulika, kwani kuendelea kushikilia misimamo ya namna hiyo kunaweza kusababisha madhara makubwa katika jamii,” alisema.

Aidha, alisema viongozi walioshinda na wale walioshindwa wanapaswa kuketi pamoja na kujadili mambo yaliyofungamana na dhamira zao kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi waliowachagua.

Alisema ridhaa waliyopewa viongozi hao na wananchi si utashi wa kibinadamu, bali umetokana na nguvu ya Mwenyezi Mungu, ambapo viongozi wa madhehebu ya dini walikesha kwenye maombi ili apatikane kiongozi mwenye ridhaa ya Mungu.

“Ningepata fursa ya kukutana na Dk. Slaa ningemshauri kuwa Mungu kamuwekea akiba kwa miaka mitano ijayo anapaswa kuwa mvumilivu katika siasa…kwa hali hii anatufanya Watanzania tuishi kwa hofu, ili tuishi kwa amani Dk. Slaa akubali matokeo,” alisema Askofu Mwakanani.

Viongozi wa dini kama wanavyofanya wengi wa wanasiasa (wa CCM) hutumia ujinga wa Watanzania kula nchi yetu. Viongozi wa dini hawatoi shinikizo lolote ili uchaguzi uwe wa haki, kazi yao ni kutaka amani. Tuwakatae watu kama hawa na tusisahau kuwapa mashinikizo kutoa misimamao yao kabla ya uchaguzi ili tujue kama wameamua kuungana na mafisadi au la.
 
Ruge Opinion

JF-Expert Member
Mar 22, 2006
1,838
698
kwa nini haw viongozi wa Dini wanahubiri upande mmoja tu, kwa nini wasingeanza kwa JK na Genge lake kuwahambia kuwa wizi ni dhambi? na watubu,
hivi nguvu ya CCM na genge jima la mafisadi linaogopwa hata na viongozi wa dini?
Mimi nadha huyo mchungaji kama yeye ni mtu wa Mungu basi angesimama kwenye haki na kumwambia Dr Slaa Haiuridhie haki yake
Ni kweli hawa wanojiita watumishi wa Mungu na wenyewe ni wachakachauji wa imani. Huyu "Rabbi" ni myahudi au nini? Jamani hivi kukataa matokeo ya wizi na dhuruma kutaletaje vurugu na machafuko? Ina maana kila mwaka mambo yakijirudia tupuuze tu? Huyo Mungu gani anayehalalisha dhuruma? Basi hakuna haja ya uchaguzi tuwe tunaomba Mungu anatuletea viongozi. Si ameishawapanga tayari. Huyo Mungu mimi namkataa.
 
mamtaresi

Member
Oct 13, 2010
53
0
haijakaa vizuri hata kidogo huu ni wizi na mungu hapendi wizi na amri yake ya saba inasema usiibe kwanini watu waibe halafu ushauri aliyeibiwa akubali tu kuwa ameibiwa asifanye chochote? dawa ya mwizi jela au anawekewa tairi tunamaliza kazi yake .dr slaa msimamo wako naupenda usiwe kigeugeu maana mungu anasema kama moto na uwe moto na kama baridi ni baridi ukiwa vuguvugu atakutapika keep it dr .slaa and go forward not backward.
 
Mwalimu

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
1,559
1,032
1SAMWELI 15:23 - "Kwa maana kuasi ni kama dhambi ya uchawi, na chukizo nikama uovu wa kuabudu sanamu. Kwa sababu umelikataa neno la Bwana, yeye amekukataa kama mfalme"

Nimeanza na nukuu ya neno hili kuonyesha ni jinsi gani watumishi wa Mungu wanatakiwa kusimama katika nafasi yao kama kiunganishi kati ya Mungu na viongozi wa kisiasa....
 
carmsigwa

Member
Nov 4, 2010
21
1
Wana JF naanza kwakushanga! halafu najiuliza hivi nikweli kiongozi mkuu wadini anaweza akateta na waumini akimtetea shetani? hakika shetani anaweza akawa amemtetea makuu mtu huyu hadi akamsahau mungu! Je waweza kuahidiwa mkuu na wezi na ukawasaliti watu wako kwakufichama chini ya mwavuli unao itwa amani na utulivu? je Watanzania wanafurahia amani nautulivu baada ya kuprwa kilakitu? kama wakuu wadini wanakuwa wanafiki namnahii tutakimbilia wapi?

Tuliwaona wakati wakampeni mkaenda chadema kuwasihi wawe tayari kuyapokea matokeo hamkuenda kwenye chama kingine leo tena mnarudi chadema mkiwasihii wakubali matokeo, kwakigezo kilekile cha utulivu naamani.Kwanini hamkuenda tume ya uchaguzi, sisiem,UWT ambao wame chafua uchaguzi kwa makusudi? hakika jibu sipati nanikipata litakuwa tusi
 
Kamakabuzi

JF-Expert Member
Dec 3, 2007
2,604
1,065
Kuna madhambi makubwa sana hapa Tz yamejificha katika gunia la amani.
Wakiiba hela zetu tukilalamika - eti Amani itavunjika
Wakiiba kura zetu tukilalamika - eti amani itavunjika
Wakikwepa kodi kwa njia ya misamaha ya kidini tukiwaeleza -eti amani itavunjika
Ama kweli Amani ya TZ umeficha uozo mwingi sana. Tunamshukuru Dr. Slaa kwa kweka wazi uozo huo, navyi wachungaji msiwe wanafiki - wakemeeni, kama ni misamaha ya kodi bora muikose kwa manufaa ya wananchi wote.
 
Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
8,200
3,528
Wizi ni dhambi.
askofu hebu hubiria hao ccm kwanza nikuelewe

Yaani askofu anawaombea na kuwabariki wezi??? hapo ndipo ninashindwa kutofautisha kati ya Mafarisayo, Masadukayo, Anasi na Kayafa Makuhani wakuu nyakati za Yesu na viongozi wa dini wa leo. Huyo askofu asingeendesha hata ibada hiyo.

Hakika Yesu angekuwapo TZ leo, tungeona vituko.
 
HM Hafif

JF-Expert Member
Aug 16, 2009
1,359
19
ASKOFU wa Kanisa la Evangelical Brotherhood Church Of Tanzania (EBCT), Rabbi Mwakanani, amempoza mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa, kumtaka kuyakubali matokeo ili kuliepusha taifa kuingia kwenye machafuko, kwa kuwa yeye na chama chake wamekuwa na ushawishi mkubwa kwa wananchi.

Akizungumza katika ibada maalumu ya kuwaombea amani viongozi walioteuliwa katika Uchaguzi Mkuu, alisema kitendo chake cha kugomea matokeo hayo ni dalili inayoweza kusababisha chuki miongoni mwa jamii.

Askofu Mwakanani alisema katika hali ya kawaida ya binadamu si rahisi kukabili changamoto zinazojitokeza baada ya kufanya kazi kubwa, lakini kwa kuwa kila jambo linalofanywa na binadamu husimamiwa na Mungu, basi kiongozi huyo anapaswa kumwachia Mungu.

“Hakuna asiyejua kuwa uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa wa kipekee ulioambatana na matukio mengi, huku wananchi wakijenga imani kubwa kwa baadhi ya wagombea, haitoshi kuamini kwa njia ya kawaida kama kweli haki ilitendeka katika mchakato wote, lakini yote hayo yanapaswa kusahaulika, kwani kuendelea kushikilia misimamo ya namna hiyo kunaweza kusababisha madhara makubwa katika jamii,” alisema.

Aidha, alisema viongozi walioshinda na wale walioshindwa wanapaswa kuketi pamoja na kujadili mambo yaliyofungamana na dhamira zao kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi waliowachagua.

Alisema ridhaa waliyopewa viongozi hao na wananchi si utashi wa kibinadamu, bali umetokana na nguvu ya Mwenyezi Mungu, ambapo viongozi wa madhehebu ya dini walikesha kwenye maombi ili apatikane kiongozi mwenye ridhaa ya Mungu.

“Ningepata fursa ya kukutana na Dk. Slaa ningemshauri kuwa Mungu kamuwekea akiba kwa miaka mitano ijayo anapaswa kuwa mvumilivu katika siasa…kwa hali hii anatufanya Watanzania tuishi kwa hofu, ili tuishi kwa amani Dk. Slaa akubali matokeo,” alisema Askofu Mwakanani.

Tulikueleza padre Slaa huyawezi mambo hayo sasa umekiona.

Ukubali , ukatae bao lipo pale pale. Tumuombe tu Kikwete akupe viti vyake vya Ikulu kama alivyofanya Dr Shein kwa Mzee Juma Duni
 
Omuregi Wasu

JF-Expert Member
May 21, 2009
749
141
Ni aibu kwa Askofu, kanisa na mwili wa Kristo kwa mtumishi wa Mungu kutetea dhambi.
Bwana mrehemu kwa kuwa hajui afanyalo. Msaidie Dr. Slaa awe na Moyo Mkuu wa Kusimamia Haki, Kweli na Upendo wako ili dunia nzima ijue kuwa WEWE ndiye Mungu wa haki... uwateteaye Wajane,Wanyonge na Yatima!! Wewe ndiye MUNGU uwateteao walioDHURUMIWA Haki zao..... BWana Yesu Utamaraki eehh Bwana!!!
 
SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
33,266
37,471
Tulikueleza padre Slaa huyawezi mambo hayo sasa umekiona.

Ukubali , ukatae bao lipo pale pale. Tumuombe tu Kikwete akupe viti vyake vya Ikulu kama alivyofanya Dr Shein kwa Mzee Juma Duni

Case ya Duni wa CUF ni tofauti case ya Dr Slaa, CCM na CUF wamefunga ndoa sasa kilichofuatia hapo ni maelewano yao, lakini Dr Slaa hana maeleano na kamwe hatakuwa na maelewano na wezi na mafisadi.
 
fauster

New Member
Nov 5, 2010
4
0
Tunashukuru askofu kwa ushauri wako kuhusu makasheshe ya uchaguzi na matokeo yaliyojili. Tunachotaka sasa nii kuona mabadiliko katika jamii yetu ambayo imeteseka kwa muda mrefu. Hao viongozi inabidi wabadilike na wamwogope MUNGU kwani jamii yetu inategemea kuona matunda ya uchaguzi na si maslahi ya watu wachache.
 
Jeremiah

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
644
126
Hawawezi kubadrika hao. Nyerere alikwisha sema . ''Ukishakula nyama ya mtu huwezi kuacha ''. Utaendelea kula tu . Hiyo dhambi itakutafuna hadi kabulini. Dawa ni kuwasafisha kwenye system. Mwenye ujasiri huo ni Dr Slaa basi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom