Elections 2010 Askofu ampoza Dk. Slaa

Kwa hiyo ukiibiwa uache tu, coz utasababisha machafuko, hii askofu HAIJAKAA POA KABISA
 
Askofu umethubutu!
ingawa kwa kweli maaskofu wangu mnaponishangaza ni pale mnaposhindwa kutoa huduma ya kinabii kuwasaidia viongozi wanaoingia madaraka kwa njia za kutatanisha kama ilivyotokea uchaguzi wa mwakahuu, kuwa ni lazima wakubali nao pia kusoma alama za nyakati badala ya kuwapiga mabomu watanzania wasio hatia.
Kusema si utashi wa kibinadamu sijui umemaaanisha nini? wako viongozi wengi walioingia madarakani kwa utashi wa kibinadamu akiwepo Sauli katika taifa la wayahudi. Huu uchaguzi wa Tanzania unathibitishaje kuwa kuwa watawala hawakuingia kwa utashi wa kibinadamu????? Ikiwa tumeona kila aina ya maigizo kabla hawajaingia!! Wakuu wa dini tumeini madhabahu kwa hofu ya Mungu mwenye nguvu.
Nawasilisha
Yesu Kristo wakati anaeneza dini alifanyiwa dhihaka sana kama vile badili mawe yawe mkate ili akabiliane na njaa, akatae yeye si Mungu ili ayakwepe mateso lakini alikataa ili akamilishe kazi yake ya utume. Mandela aliahidiwa vitu vingi sana na Makaburu iwapo ataacha kujihusisha na siasa na leo ni mtu anayeheshimika sana duniani . Ni mambo ya kusikitisha sana kuona mtumishi wa Mungu(askofu) anamshauri Slaa aache kusimamia ukweli ahamie kwenye uongo. Kwa nini askofu ana roho nyepesi namna hii? Bila shaka ametumwa au anajikomba huenda CCM wakatoa bahasha kwa wanaotetea uongo. Askofu hakuna watanzania watakaopigana kwa ajili ya matokeo lakini mwaje Slaa asimame kwenye ukweli kama anaamini hivyo. Kama unaiogopea nafsi yako jikalie kimya
 
Back
Top Bottom