Askofu amkaanga Makinda

Askofu amkaanga Makinda

Ili gazeti toka liandike Tyson kawa mwanamke siku nalinunua nafunguia pweza au ngisi.

Kumbe mara moja moja unakuwa na akili. Hapa nakupongeza kwa kuchangia kuliongezea mauzo gazeti makini Tanzania. Wakati unakula pweza unasoma na habari muda huo huo.
 
Askofu anayeficha jina lake anawachafua Maskofu wenzake
 


Huwezi kutumia cheo cha Uaskofu kusema jambo la kitaifa kisha ukaliomba gazeti kuficha UASKOFU WAKO. Cheo ni dhamana

Unapoongea jambo la kitaifa kama mtu binafsi unaweza kuficha ID yako.
 
Atakuwa Askofu kanjanja huyo..

Kanjanja haswaaaaaaaaaaaaaa.

Atakuwa hatoki kwenye madhehebu makubwa kama KKKT au Katoriki huko hakuna kujisemea hovyo hovyo.

Bado tunambuka Askofu Kilaeni alikuwa msaidizi wa Cadinal Pengo akaaanza kusema hovyo hovyo akahamishwa.

Makanisa mengine yana Askofu mmoja tu aliyejipachika Uaskofu. Uaskofu unakuwa wa mtu mmoja hadi atakapokufa.
 
Kwa kuogopa kutaja jina lake, Aksofu amehidhihirisha kuwa mnafiki hasa ukizingatia nafasi yake katika jamii.

Njia bora ya kuepusha malumbano ni kukaa kimya...

Askofu gani huyo????!!!!!!!!Roho yake ya unabii iko wapi??????????

Kama hata askofu anaomba jina lihifadhiwe basi ujue hajiamii, maana yake hana tofauti na wanasiasa

keleb...


Lakini yeye akiwa kama Mtanzania ana haki ya kutoa maoni yake. Hapo aliongea kama mtanzania na siyo kama Askofu kwani hajawakilisha kanisa lake bali ni maoni yake.

Na pia anaogopa Serikali yaweza kumfanyia mambo kama waliyomfanyia Dr. Ulimboka.

Bado tunampenda Askofu wetu huyu.


MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Naye askofu wa kanisa moja kubwa nchini ambaye aliomba kuhifadhiwa jina ili kuepusha malumbano, alisema kuwa Spika Makinda na Naibu wake, Job Ndugai, wanayumba na wanaliyumbisha Bunge.
Akizungumza na gazeti hili kwa simu, askofu huyo alisema kuwa viongozi hao wawili wametumwa na wanatumika. Na kwamba wale waliowatuma wanaona kuwa wanafanya vizuri kwani ndilo hasa lengo.
Alisema ni juhudi za wabunge pekee, tena wenye maono ya kizalendo, ndizo zinaweza kuwaondoa madarakani kwani ni vibaraka.
“Ukimlinganisha huyu Spika na wenzake waliowahi kuongoza Bunge, huyu ni balaa. Amevaa itikadi zaidi. Lakini tunatafsiri kuwa anatumika na Rais.
“Huwezi kuwa na Bunge imara kama una serikali dhaifu. Ndiyo maana katika nchi yetu sasa, mtu hawezi kuwa Spika kama Rais hajamkubali,” alisema.
Alisema hayo tunaweza kujifunza kutokana na kauli ya Makinda ya hivi karibuni alipotoa maoni yake kwenye tume ya kukusanya maoni ya Katiba, pale aliposema kwamba anapendekeza Spika asitokane na chama cha siasa.
Hiyo ina maana anashinikizwa na chama chake kufanya mengi ambayo kama si shinikizo, asingeyafanya. Hata haya yanayotokea ni shinikizo la chama chake.
“Hali ni hiyohiyo hata katika mahakama. Serikali inaingilia sana uhuru wa mahakama. Ndiyo maana hata Jaji Mkuu alipotoa maoni yake katika Tume ya Marekebisho ya Katiba alisema angependa mahakama iwe huru.
“Maana yake anajua kuwa kwa sasa kuna shinikizo kutoka serikalini au chamani katika uendeshaji wa maamuzi ya mahakama nchini. Hii ni hatari,” alisema.
Askofu alibainisha kuwa Makinda ni tofauti na Spika aliyepita Samuel Sitta; kwamba Sitta alikuwa na mwelekeo, alisimamia ukweli, japo mwelekeo wake haukupendwa na watawala.
Aliongeza kuwa Sitta alikuwa mpigania haki, mpenda mabadiliko na aliweza kuonyesha kuwa anawajali wanyonge. Hakuliyumbisha Bunge na aliweza kusimamia maamuzi.
“Bunge haliongozwi kitaasisi, bali linaongozwa kwa matashi ya mtu binafsi au kikundi cha watu.
“Sisi tunapaswa kuwa makini katika kuchagua watu wa aina hii na tunapaswa kuwaelimisha Watanzania ili wapambane kuondoa mfumo wa aina hii,” alisema.

source: Tanzania daima

Hatuna tatizo na ujumbe wake,tatizo ni pale mchunga kondoo wa bwana anapojificha na kukemea akiwa kichakani hapo ndiyo shida.Hata hao kondoo watadhani ni masikhara.

Pili nilishawahi kusema ni bora kama ikishindikana wabunge wazalendo waamue kujiuzuru wao na kuliacha bunge liwe la Makinda na Ndugai japokuwa kwenye msafara wa mamba na kenge nao wamo.
 
Hapa kosa sio la askofu ni upumbavu wa mwandishi na mhariri wake, kama mtu hataka kutaja jina kwa nini umpe prominence? inamaana hii ni habari ya kutungwa na wakina Ansbert ili kutengeneza story kwanza ni askofu gani Tanzania anayemuogopa rais na hivyo kuogopa kusema ukweli? maaskofu wanamuogopa mungu tu na ndio maana walitoa waraka na kumuuliza huyu bwana juu ya mfumo kristo kwenye serikali yenye asilimia 95 ya viongozi wakiwa waislamu na mpaka leo amefyawa mkia hajajibu, Tanzania Daima acheni usanii wenu mnaboa acheni uvivu nakufanya kazi zenu binafsi wakati na sehemu yakazi

Na mimi Naitwa Askofu KAZIMOTO naomba JF mfiche jina langu..... Ha ha ha haaaaaaa
 
Danganya toto UZI umeanza na Askofu, members wengi wamekimbilia kuusoma wanakutana na Askofu asiye na jina!!!!!!!!!!!!!!!!!! ha ha ha haaaaaaaaa

Hana roho ya Unabiii Ha ha ha haaaaaa

Anamwogopa Shetani Ha ha ahaaaa

Hukuna jambo la Hatari katika dini kama Uoga ha ha haaaa
 
Kwa kuogopa kutaja jina lake, Aksofu amehidhihirisha kuwa mnafiki hasa ukizingatia nafasi yake katika jamii.

Viongozi wa dini wa nchi hii ndio wanafiki namba moja. Ukiona ametoa hata hizo comments za kinafiki ujue ni kwa sababu kuna mambo fulani kapishana na watawala. Mara nyingi huamishia hasira zao za kupishana na watawala kwenye kuchochea wananchi. All in all hii serikali haina muelekeo na kila mtu anajua kinachoendelea hata kama askofu asingeongea kitu
 
Askofu anatoa hoja yake huku hataki kujulikana kama yeye ndiye mwenye hoja hiyo. Askofu bwana tehe! tehe! tehe!
 
wakuu lakini mbona wengi wetu humu jamvin tunaandika majina yasiyo halisi..tuna tofauti gan na huyo askof kama kwel tunahitaji mabadiliko ...usimnyoshee mtu kidole kimoja huku vinne vinakurudia

Kwanza nakugongea LIKE. Wengi wamelaumu askofu na kujizolea laana wakati wao wenyewe wanatumia majina feki kwa woga wa kutambulika. Jifanye jasiri kwenye serikali jasiri kama hii uone. Mmesahau Jasiri aliyepelekwa mabwepande na aliporudi akawa kimya kama vile hayupo???? Mmesahau jasiri wa nyololo. Acheni kumwona mwenzenu mwoga, wakati wenyewe uoga umewajaa. "Toa kwanza boriti kwenye jicho lako, ndipo uone kibanzi kwenye jicho la mwenzako"
 
Tatizo watu wanatokea kusikojulikana wanajitangazia Uaskofu Mkuu kanisa hilo hilo halina cha askofu msaidizi au maaskofu wengine....yaani hat thamani ya jina lenyewe wanaishusha.

.
Kama kweli watu tunawaza vizuri na kama huo ujumbe sii wa kulishwa ni mawazo ya huyo askofu kweli, basi hicho ni kichwa kilichoenda shule na kuiva. Mnapomhusisha na wale askofu wa kujitangaza nawashangaa. Lakini maneno yake yanayoweza kuwa Mada ya kujadiliwa hata katika vyuo vyetu vikuu, hayawezi kumwacha nyoka pangoni mwake ni lazma atoke kujitetea. Ndio maana hapa unaona Tiss wote waliomo jf wametoka kuokoa jahazi.
Askofu ametaja jina ama hakutaja lakini ukweli na uhalisia aliotoa unajitosheleza.
.
 
Jomba naona umeamua kula sumu kwa sababu tu umesikia harufu ya ARKI!
Hivi wewe na hao Maaskofu wako munaposema zaidi ya 95 Viongozi wa Serikali ni Waislamu hua munakusudia nini? Mimi ninavyofahamu Serikali haikamiliki kwa Raisi, Spika, Makamo wa Raisi, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu, Mwanasheria Mkuu, IGP na au Mkuu wa Majeshi peke yao bali uongozi wa Serikali unajumuisha Mawaziri, Manaibu Waziri, Makatibu Wakuu, Wakurugenzi, Gavana wa Benki kuu, Wakuu wa Mikoa na Wilaya na wengineo.
Ili wewe na Maaskofu wako muniridhishe hemu nambieni katika hao Waislamu ni wangapi na wasiokua Waislamu ni wangapi?? Musiishie kutoa takwimu za 95% bali mungetenda haki zaidi iwapo mutatupa orodha ya uwiano wa idadi katika kila taasisi ya serikali! Binafsi TAMKO lile la Maaskofu limeliona ni KITUKO cha mwaka.

Acha Longo longo, hizo nafasi wakristu wanaozipata ni wale wenye sifa na siyo kwamba wanapewa. Washauri wenzako msomeshe watoto wenu na siyo kulalamika kila kukicha, hii approach haitawasaidia.
 
Huyu Askofu atafutwe na akamatwe kwani anataka kuchanganya dini na Siasa! amesahau ya Kaisari ampe kaisari?...
 
Back
Top Bottom