Askari wanyapori wafanya mauaji ya kutisha!

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,195
Reaction score
27,810
Askari 12 wanaodhaniwa kuwa kikosi kinachopambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi ya taifa ya Tarangire Wilayani Babati mkoani Manyara wanadaiwa kufanya mauaji ya kutisha baada ya kumteka nyara mkulima mmoja mkazi wa mji mdogo wa Galapo ambaye hajulikani alipo na kisha kumtesa na kumshambulia kwa kipigo mke wa mkulima huyo na kusababisha kifo chake kutokana na kile kinachodaiwa kuhusika katika vitendo vya ujangili.

Akizungumza na mamia ya wananchi waliokuwa na hasira huku baadhi yao wakiwa wamepoteza fahamu kwenye nyumba ya msiba katika Kitongoji cha Olongadida mwenyekiti wa kitongoji hicho Bw Rashidi Kajogoo amesema anashangazwa na askari wa hifadhi hiyo kumteka Nyara Bw Eliasi Kibuga Oktoba 14 kinyemela bila ya uongozi kufahamu aidha baada ya mke wake Bi Evaline Gaspa kufuatilia nae Alikamatwa na kisha kufa katikamzingira ya kutatanisha na mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya mrara mjini babati.

Wakati jitihada za kumtafuta mkuu wa hifadhi hiyo bw stephen qoolzikiendelea kufanyika ili kuzungumzia tukio hilo,nae kamanda wa Polisi mkoani hapa afande Akili Mpwapwa akizungumza kwa njia ya simu amekiri kukamatwa kwa mwanamke huyo ambaye amedai baada ya upekuzi alikutwa na mkia wa twiga lakini kifo chake akidai kimetokana na mshtuko wa mahojiano na kufariki na timu ya polisi Imefuatilia kubaini mume wa marehemu mahali alipo,kauli ambayo imepingwa na watoto wa familia hiyo walioshuhudia kipigo cha mama yao huku baba yao akiwa hajulikani alipo.

Hata hivyo kufuatia kuwepo kwa tukio hilo la mauaji liliamsha hasiramamia ya wanawake kupinga mauaji hayo dhidi ya mwanamke mwenzao Bi. Evaline Gaspa huku wakidai kifo chake kimetokana na unyanyasaji ambao haukushirikisha askari wa kike na kutishia kumfungulia mashtaka mkuu wa hifadhi hiyo.

SOURCE: ITV
 
habari imekaa kiudaku daku
Ndugu habari hii ni ya ukweli hivyo comment yako ni maumivu zaidi kwa wafiwa
Hizi operesheni za ujangili na hata Kimbunga..city nk zimejaa watendaji wabovu na wasio na ufahamu wa kutosha juu ya wanachokifanya hatimae kupelekea madhara makubwa kama hili kwa kutumia mabavu kuliko weledi
Taarifa za kipolisi nazo zibatia shaka hivyo kujenga hasira kwa wananchi.
Wanaharakati waliangalie hili kwa jicho la tatu ili ukweli ufahamike na hatua za haki kisheria zifuatwe
 
Hawa polisi ni wauaji wakubwa. Hawawezi kukwepa kuwajibishwa kwa mauaji ya raia asiyekuwa na hatia.
 
Jamani waziri mwenye dhamana inabidi aliangalie hili vizuri maana hizi operation hazina kichwa wala mguu wakikusanya data baani dk 5 unashangaa mtu kashikwa.
 
yaani huko Mtwara hadi wawindaji wa panya-samaki nchanga wamekamatwa..hatari!!
 
Askari 12 wanaodhaniwa kuwa kikosi kinachopambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi ya taifa ya Tarangire Wilayani Babati mkoani Manyara wanadaiwa kufanya mauaji ya kutisha baada ya kumteka nyara mkulima mmoja mkazi wa mji mdogo wa Galapo ambaye hajulikani alipo na kisha kumtesa na kumshambulia kwa kipigo mke wa mkulima huyo na kusababisha kifo chake kutokana na kile kinachodaiwa kuhusika katika vitendo vya ujangili.

Akizungumza na mamia ya wananchi waliokuwa na hasira huku baadhi yao wakiwa wamepoteza fahamu kwenye nyumba ya msiba katika Kitongoji cha Olongadida mwenyekiti wa kitongoji hicho Bw Rashidi Kajogoo amesema anashangazwa na askari wa hifadhi hiyo kumteka Nyara Bw Eliasi Kibuga Oktoba 14 kinyemela bila ya uongozi kufahamu aidha baada ya mke wake Bi Evaline Gaspa kufuatilia nae Alikamatwa na kisha kufa katikamzingira ya kutatanisha na mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya mrara mjini babati.

Wakati jitihada za kumtafuta mkuu wa hifadhi hiyo bw stephen qoolzikiendelea kufanyika ili kuzungumzia tukio hilo,nae kamanda wa Polisi mkoani hapa afande Akili Mpwapwa akizungumza kwa njia ya simu amekiri kukamatwa kwa mwanamke huyo ambaye amedai baada ya upekuzi alikutwa na mkia wa twiga lakini kifo chake akidai kimetokana na mshtuko wa mahojiano na kufariki na timu ya polisi Imefuatilia kubaini mume wa marehemu mahali alipo,kauli ambayo imepingwa na watoto wa familia hiyo walioshuhudia kipigo cha mama yao huku baba yao akiwa hajulikani alipo.

Hata hivyo kufuatia kuwepo kwa tukio hilo la mauaji liliamsha hasiramamia ya wanawake kupinga mauaji hayo dhidi ya mwanamke mwenzao Bi. Evaline Gaspa huku wakidai kifo chake kimetokana na unyanyasaji ambao haukushirikisha askari wa kike na kutishia kumfungulia mashtaka mkuu wa hifadhi hiyo.

SOURCE: ITV

Askar wanyaporiiiiiiiiiii??hawa itakuw ni wageni??au ulimaanisha askar wanyama pori?
 
yaleyale ya "wapigwe tu",hawa askal wa wanyama poli wameadopt tabia za wanyama wamekxa wakatil zaid ya hata wanyama.
 
Jamani hebu tufunguke macho. Baadhi yetu tunafanya makosa kuwalaumu askari kwa mauaji hayo na mauji mengine yanayofanywa na maaskari nchini. Tusiwalaumu polisi. Hao ni kama mbwa tu wanaotimiza amri ya kuuma kwani wanatii tu viapo vyao!

Mwenye mbwa ndiye anapaswa kulaumiwa hapa. Mkuu wa nchi ambaye ni amiri jeshi mkuu anajua fika kinachoendelea. Yeye ndiye mratibu mkuu wa mauaji yote ya kiholela yanayofanywa na maaskari. Hayo ni maagizo kutoka kwake! Lawama zote zimwendee yeye! Huu ni utawala mbovu kabisa kupata kutokea katka historia ya Tanzania!
 
No comments
 
Ndugu habari hii ni ya ukweli hivyo comment yako ni maumivu zaidi kwa wafiwa
Hizi operesheni za ujangili na hata Kimbunga..city nk zimejaa watendaji wabovu na wasio na ufahamu wa kutosha juu ya wanachokifanya hatimae kupelekea madhara makubwa kama hili kwa kutumia mabavu kuliko weledi
Taarifa za kipolisi nazo zibatia shaka hivyo kujenga hasira kwa wananchi.
Wanaharakati waliangalie hili kwa jicho la tatu ili ukweli ufahamike na hatua za haki kisheria zifuatwe

unafiki na uchochezi huo. Bandiko la muda nreefu,unalirudia kwa sababu mawaziri wametimuliwa! Umbea huo.
 
Hawa polisi ni wauaji wakubwa. Hawawezi kukwepa kuwajibishwa kwa mauaji ya raia asiyekuwa na hatia.

we bwabwaa nini? Umeambiwa ni mawaziri wa wizara nne, we unakomaa na polisi tu, we criminal or?
 
habari imekaa kiudaku daku

Kama nawewe umeshiriki kwenye mauaji damu yake iko juu yako. Yaani pamoja na kujitosheleza kwa taarifa baxo unasema imekaa kiudaku udaku?
 
unafiki na uchochezi huo. Bandiko la muda nreefu,unalirudia kwa sababu mawaziri wametimuliwa! Umbea huo.
Sikuzuii kufikiri hivyo..
Tulioona maovu haya tulishayalalamikia muda mrefu
Siamini maneno haya kutoka kwako ndugu.je umeona wameonewa?
 
Back
Top Bottom