Askari wakamatwa kwa kuuza risasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askari wakamatwa kwa kuuza risasi

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Pdidy, Oct 28, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,168
  Likes Received: 5,594
  Trophy Points: 280
  Askari wakamatwa kwa kuuza risasi
  Anna Makange, Tanga
  Daily News; Tuesday,October 28, 2008 @00:02  Polisi mkoani hapa inawashikilia askari wawili wa Gereza Kuu la Mkoa wa Tanga, Maweni, kwa tuhuma za kumiliki risasi 19 za bastola kinyume cha sheria. Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Simon Sirro alisema watuhumiwa hao kwa pamoja walikamatwa Oktoba 20, mwaka huu saa 4:30 asubuhi katika Barabara ya Kwanza jijini hapa.

  Aliwataja askari hao kuwa ni Koplo Dickson Michael (37) ambaye ni mtunza ghala la silaha la Gereza la Maweni pamoja na mwenzake Zuberi Mhando (29), ambao alidai walikuwa wakijaza risasi zilizotumika kwenye maboksi ya risasi mpya mara baada ya kuziiba.

  Kamanda huyo alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na taarifa ya raia wema ambao walilieleza jeshi hilo kuwa mara kwa mara askari hao wamekuwa wakiwauzia risasi wahalifu, hatua iliyolifanya jeshi hilo kuandaa mtego uliofanikiwa kuwanasa.

  "Raia wema walitueleza kwamba mara kwa mara wamekuwa wakiwaona askari hao wakiuza risasi kwa majambazi ambapo bei ni shilingi elfu sita kwa kila moja. Ndio tukaamua kuweka mtego kwa kuwapa dili la kuuza risasi mia kwa kila moja shilingi elfu nane, nao wakachangamkia, lakini hawakuweza kufanikisha kiasi chote walichoagizwa, kwani siku ya tukio walifika katika eneo la biashara na risasi kumi na tisa tu, ndio tukawakamata,” alifafanua Kamanda Sirro.

  Alisema katika uchunguzi wa awali, Koplo Michael na mwenzake Mhando walikiri kuiba risasi 70 kwa nyakati tofauti kutoka kwenye ghala la silaha la gereza hilo na kusema walikuwa wakiziuza kwa watu mbalimbali ambao sio waadilifu na walikuwa wakizitumia katika uhalifu ndani na nje ya Mkoa wa Tanga.

  Hata hivyo, Sirro alibainisha kuwa tayari watuhumiwa hao wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Tanga na kwamba Polisi inaendelea kuwasaka watuhumiwa wengine ambao wametajwa kuhusika kununua risasi hizo 70 zilizoibwa kwa nyakati tofauti.
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Yale yale ya mkulima kula mbegu..
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,168
  Likes Received: 5,594
  Trophy Points: 280
  hapo wamekamatwa wakiwahi wewe utapona jibu
  analo
  mh mwema!!!!!!
   
Loading...