Askari wafichua ufisadi katika Jeshi la Magereza

Askari wafichua ufisadi katika Jeshi la Magereza

Mbona kuna askari trafiki alilalamika kuwa hata wao wajinunulia sare zao
 
Hawa wajela jela Vepeee.
Eti nao wanataka kwenda Mission za ki Jeshi kama Darfur etc.
Kule hakuna Wafungwa bana wa kuwalinda.
Labda wangeomba kwenda Mission Guantanamo Bay inge Make Sense
 
kila sehemu ni AIBU!!!
Ni kweli kabisa kuwa mambo hayaendi vyema kwenye taasisi nyingi kutokana na mfumo wa kifisadi nchini na inahitajika kazi ya ziada kupiga vita ufisadi wenye unaochukua mbinu, sura na rangi tofauti kutegemea na nyakati na maendeleo ya teknolojia.

Hili la jeshi la magereza linaakisi mambo yalivyo kwenye taasisi za majeshi. Wengi wa skari wa vya vyeo vidogo wanavaa sare zilizochakaa na kupauka. Raia wameaminishwa kuwa kila jambo la majeshi husan la JWTZ ni "nyeti" likiwemo la matumizi ya fedha.

Wakati wa vikao vya bunge vya kila mwaka vya kujadili makadirio ya mapato na matumizi ya fedha (bajeti) ya taifa, wabunge hawajadili na kuhoji kwa kina makadirio ya matumizi ya majeshi. Ni kawaida kupitishwa kama yanavyowasilishwa kwa mazoea. Si rahisi kuhojiwa na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali anapofanya ukaguzi wake wa kisheria (statutory audit).

Ukiacha JWTZ, rushwa na vitendo vya rushwa ni vingi katika majeshi yetu. Baadhi ya askari wa sehemu zilikoshamiri kwa rushwa "wanajituma" zaidi kwa lengo la kunufaika binafsi. Ndiyo maana huo uozo wa magereza umekuwepo kwa muda mrefu bila kufichuka. Inawezekanaje wasimamia sheria na amani wakawa wahanga wa vitendo vya rushwa? Inawezekana kuzibika kwa mirija ya vipato haramu kumewang'ata kimaisha wanufaika na sababu ya haya kuibuka.
 
Duh,
Hii nchi ina mabo mengi!

Kadri mirija ya kifisadi inavyozibwa ndivyo na kelele za mafisadi na wapambe wao zitazidi kusikika.

Ikumbukwe mafisadi ni watu wenye pesa na ushawishi katika jamii na kwa maana hiyo kelele zao zitasikika zaidi kwa wananchi wajinga na wenye mitazamo tofauti kisiasa.

Serikali ya Rais Magufuli inakabiliwa na jukumu la kuelimisha hawa wajinga ili wasikubaliane na kelele za mafisadi na wapambe wao.

Kikubwa zaidi, Serikali iachane na kundi la wenye mitazamo tofauti ya kisiasa kwa sababu hawawezi kubadilika hata kama serikali itatoa huduma zote za kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Hii nchi haitanyooka bila huu mfumo uliojengwa na sisiemu kufa..,Ishu kama ile ya pembe za ndov jamaa kaimalizia kimyakimya maana anajua mkono wa viongoz wa chama. kidumuuu...
 
Hawa wajela jela Vepeee.
Eti nao wanataka kwenda Mission za ki Jeshi kama Darfur etc.
Kule hakuna Wafungwa bana wa kuwalinda.
Labda wangeomba kwenda Mission Guantanamo Bay inge Make Sense
Tulia mambo mengine huyajui mkuu
Mengine yako deep hata uki Google hautapata majibu
 
Nianze kwa kushukuru ziara ya kushtukiza ya Mhe. Rais DKT Magufuli. Ni kweli Askari MAGEREZA wamekuwa wakinunua sare zao ktk uchambuzi wangu nimebaini kwamba mara ya mwisho kupata sare za Askari ilikua mwaka 1998. Kuanzia hapo hadi Leo hawajapewa mgao, wamekuwa wakinunua sare zao kutoka kwenye maduka ya kamishna jenerali John Minja. pia kozi ya Askari MAGEREZA imekuwa ikiendeshwa pasipo na gharama yoyote, hivi kweli makazi ya ASKARI yanafurahisha. Kupata vyeo imekuwa kasheshe, kwa kheri jenerali John MINJA ulichowafanyia Askari MAGEREZA kamwe hawawezi kufurahia kustaafu.
 
Nianze kwa kushukuru ziara ya kushtukiza ya Mhe. Rais DKT Magufuli. Ni kweli Askari MAGEREZA wamekuwa wakinunua sare zao ktk uchambuzi wangu nimebaini kwamba mara ya mwisho kupata sare za Askari ilikua mwaka 1998. Kuanzia hapo hadi Leo hawajapewa mgao, wamekuwa wakinunua sare zao kutoka kwenye maduka ya kamishna jenerali John Minja. pia kozi ya Askari MAGEREZA imekuwa ikiendeshwa pasipo na gharama yoyote, hivi kweli makazi ya ASKARI yanafurahisha. Kupata vyeo imekuwa kasheshe, kwa kheri jenerali John MINJA ulichowafanyia Askari MAGEREZA kamwe hawawezi kufurahia kustaafu.
Noted!
 
Hayo mambo yanafanyika sehemu nyingi tu ...kama JPM amedhamiria kweli kuwatetea wanyonge afumue huko wizarani na kwenye mahalmashauri yake.Hiyo ni moja tu kati ya midudu kibao iliyoko kwenye serikali yake.
 
Nianze kwa kushukuru ziara ya kushtukiza ya Mhe. Rais DKT Magufuli. Ni kweli Askari MAGEREZA wamekuwa wakinunua sare zao ktk uchambuzi wangu nimebaini kwamba mara ya mwisho kupata sare za Askari ilikua mwaka 1998. Kuanzia hapo hadi Leo hawajapewa mgao, wamekuwa wakinunua sare zao kutoka kwenye maduka ya kamishna jenerali John Minja. pia kozi ya Askari MAGEREZA imekuwa ikiendeshwa pasipo na gharama yoyote, hivi kweli makazi ya ASKARI yanafurahisha. Kupata vyeo imekuwa kasheshe, kwa kheri jenerali John MINJA ulichowafanyia Askari MAGEREZA kamwe hawawezi kufurahia kustaafu.
Aroo, we utakua afande Magereza wewe! Ila poleni sana maana ninyi ni kati ya jeshi linalopata adha nyingi mno.Nafikiri hata salaries zenu zinatakiwa kua juu kidogo kuliko jeshi lolote nchini, mlikua kama mmesahaulika hivi, maana muda wote ni kulinda wafungwa hakuna njia nyingine ya kutafuta kipato isopokua kwa mabosi tu, Wale wenzenu wanaweza kupata za kupigia viatu kiwi barabarani na ninyi mtapatia wapi? Nawaonea huruma sana, huyo Minja sio wa kuachwa tu bali achunguzwe na ikirhibitika alikua fisadi afungwe tu.
 
Mara nyingi Magu huwa anasema "Kazi hii ngumu, niombeeni" nilikuwa simuelewi kabisa ila sasa ndio naelewa. Askari anajinunulia uniform, daaah.
 
BAADA ya Rais John Magufuli kulipiga marufuku Jeshi la Magereza na majeshi mengine nchini kuruhusu askari wake kununua sare kwa watu binafsi, askari wa jeshi hilo wameibuka na kudai kuwa wamekuwa wanauziwa sare hizo kwa Sh 45,000.

Pia wamesema kofia na mikanda licha ya kuwa haiuzwi kwenye maduka ya watu binafsi, lakini upatikanaji wake pia ni wa shida, hali ambayo inawalazimu askari kutoa rushwa kwa wahifadhi bohari ili kupatiwa sare hizo.

Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti, askari mbalimbali waliohojiwa na gazeti hili licha ya kumpongeza Rais Magufuli kwa kulikemea suala hilo, walisema ni rahisi kushona kombati uraiani kwa kuwa vitambaa vinapatikana madukani, lakini kofia na mkanda ikichakaa askari analazimika kutoa pesa ili kupata mavazi hayo.

“Hizi kofia na mikanda inatolewa bohari ya jeshi, lakini kuupata huko mkanda au kofia lazima utoe rushwa kwa askari anayefanya kazi pale,” alisema mmoja wa askari aliyehojiwa na gazeti hili.

Wengi wa askari hao walisema kutokana na ugumu wa kupatikana na kofia na mikanda ya jeshi hilo, wengi wao wanaendelea kutumia kofia na mikanda waliyopewa wakati wanamaliza mafunzo.

Walisema kinachotolewa bure na jeshi hilo kwa sasa ni vyeo tu na sio sare nyingine yoyote. “Kofia hii ninayotumia pamoja na mkanda ni ile niliyopewa wakati namaliza depo (mafunzo) mwaka 2001,” alisema askari huyo ambaye ana miaka 15 sasa kazini na kuongeza, “Magereza wanachotoa bure kwa askari wao ni zile alama za cheo tu, vingine vyote vinavyohusu sare lazima askari ajinunulie.”

Wakati askari Magereza wanajinunulia sare, serikali imekuwa inatoa mamilioni ya fedha kwa ajili ya kuwahudumia askari hao.

Mfano, katika bajeti ya mwaka 2015/16 serikali ilitoa Sh bilioni 167.1 kwa jeshi hilo.

Kati ya fedha hizo, Sh bilioni 67.7 zilitolewa kwa jeshi hilo kwa ajili ya matumizi mengineyo, Sh bilioni 97.7 kama mishahara na fedha za maendeleo zilizotolewa kwa polisi ni Sh bilioni 1.6 Askari mmoja ambaye yuko mkoani Simiyu aliyefanya mahojiano na gazeti hili, alisema upatikanaji wa sare za Magereza kwa askari walioko mikoani ni mbaya, kwani wamekuwa wanalazimika kununua suruali na shati kati ya Sh 40,000 na 45,00 na viatu Sh 40,000.

“Juzi nilikuja hapo Dar es Salaam, nikawa na shida ya mkanda na kofia, nililazimika kutoa Sh 30,000 ambayo kofia niliinunua kwa Sh 10,000 na mkanda nilinunua kwa Sh 20,000,” alisema askari huyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini. Alipoulizwa anazipataje sare za jeshi hilo, alifafanua, “Sisi ukitaka sare unaenda kwa fundi unachukuliwa vipimo vya shati na suruali, unamtumia askari mwenzako wa Dar es Salaam anakununulia kitambaa na kukushonea, kisha anakutumia.”

Alisema yeye tangu amalize mafunzo mwaka 2009 hajawahi kupewa sare yoyote. “Sijawahi kupewa mkanda, kofia wala viatu vyote tunajinunulia... mkanda nilio nao na kofia ambayo imeisha nilipewa wakati namaliza mafunzo, hadi juzi nilipokuja huko ndipo nikafanya jitihada za kupata kofia na mkanda mwingine,” alisema.

Askari mwingine wa kike anayefanya kazi jijini Dar es Salaam, alisema wamekuwa wanajinunulia vitambaa katika duka la Khimji na kwenda uraiani kushona sare hizo.

“Unachagua mwenyewe fundi wako, lakini mita ya kitambaa tunanunua kwa Sh 8,000 pale kwa Khimji, mashono yanategemea na fundi utakayempelekea mwenyewe,” alisema askari huyo na kuongeza kuwa wamekuwa wananunua soksi pia kwa Sh 4,000 huko uraiani.

Aliongeza kuwa yeye alimaliza mafunzo mwaka 2001 na tangu wakati huo amekuwa anavaa mkanda na kofia aliopewa akiwa mafunzoni. “Sijawahi pata mgawo wowote wa sare tangu nitoke mafunzoni,” alieleza.

Alifafanua kuwa hata pale askari akihitaji kofia akienda kuomba bohari askari wanaofanya kazi kwenye hizo bohari wanataka wapewe rushwa ndipo waitoe.

“Hivi hivi huwezi pata kofia wala mkanda, lazima utoe kitu kidogo kwa anayefanya kazi bohari, kwa kweli mimi nilienda siku moja nikapata usumbufu sikuwahi tena kurudi huko,” aliongeza.

Kuhusu viatu, alisema wengi wa askari wanaofanya kazi Segerea na Ukonga wamekuwa wananunua viatu kwa mafundi wa uraiani ambao wanachonga viatu vinavyofanana na vya Magereza.

Alisema kwa sasa wananunua duka moja lililoko Mombasa, Ukonga ambako kuna huyo mtu anayevishona viatu vya aina hiyo. Askari mwingine wa kike alisema amekuwa anashona shati kwa Sh 10,000 uraiani na kwenye kiwanda cha Magereza anashona kwa Sh 5,000. Bei hiyo pia ni kwa sketi. Alisema sare kamili lazima igharimu mita 3.

“Pale dukani Kwa Khimji tunanunua kwa bei ya jumla ya shilingi elfu nane kwa meta, lakini ukienda maduka mengine ya rejareja unapigwa hadi shilingi elfu kumi na mbili kwa mita,” alibainisha.

Askari mwingine aliyeko mkoani Mwanza akizungumza na gazeti hili alisema wao kambini kwao walipatiwa mgawo wa mwisho mwaka 2012 na tangu wakati huo hawajapewa mgawo wowote.

Alisema wamekuwa wanaagiza sare Dar es Salaam kwa kutuma fedha Sh 40,000 au Sh 45,000 pamoja na vipimo, askari mwenzako anaenda kukununulia na kukutumia.

“Mimi hapa kofia yangu imetoboka, lakini kuipata kofia ni ngumu zaidi maana hizo hazipatikani kwingine kokote kama ilivyo kwa mkanda ambao nao unakaa nao miaka mingi hadi unabadilika rangi,”alisema askari huyo wa kiume.

Alisema mara nyingi wamekuwa wananunua viatu kwenye mitumba.

Alisema soksi pia wananunua zile zinazofanana na rangi ya magereza uraiani kwa Sh 5,000. Kutokana na jeshi la Magereza kutokuwa na utaratibu wa kuwagawia askari wake sare, wamekuwa hawana uwezo wa kudhibiti sare hizo kuvaliwa uraiani na kampuni zingine za ulinzi au hata mashule.

Kuna baadhi ya shule pia zimekuwa zinawashonea wanafunzi wao vitambaa hivyo vinavyotumiwa pia na askari wa magereza.

Mojawapo ya shule hizo ni Shule ya Sekondari ya Kitunda ambayo wanafunzi wanavaa sketi na suruali zinazofanana na sare ya Jeshi la Magereza. Kamishna Mkuu wa Magereza, John Minja alipotafutwa jana atoe ufafanuzi wa sababu ya askari wake kushona sare uraiani, simu yake iliita bila majibu.

Hata alipoandikiwa ujumbe mfupi wa maneno katika simu yake ya mkononi, alisema yuko kwenye kikao. Juzi Rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza kwenye kambi ya jeshi la Magereza ya Ukonga na kueleza kuwa na taarifa za askari wa jeshi hilo kununua sare kwenye maduka ya watu binafsi.

Alipiga marufuku askari hao kuendelea kununua sare uraiani badala yake akataka jeshi hilo liwape bure hizo sare.

“Wakati wa utawala wangu askari wote wapate sare bure, wataenda kununua uraiani nikimaliza muda wangu. Na kuanzia leo maduka yote ya raia yaliyoko kwenye kambi za kijeshi yaondolewe na wauza sare hizo wakome kufanya biashara hiyo mara moja,” alisema.

Alisema kuna baadhi ya maofisa wa jeshi hilo la Magereza wamekuwa wanashirikiana na watu binafsi kufanya biashara ikiwemo kuuza sare za jeshi, jambo ambalo alisema ni kinyume kabisa na taratibu za jeshi hilo.
Chanzo:Habarileo.

Video ya Rais Magufuli alipotembelea gereza la Ukonga na kuambiwa ufisadi wa Magereza.

Ok
 
Nchi hii kila alipo mchagga kuna wizi, hawa watu wa hovyo sana, hivi mbowe alishalipa pesa yetu?

Mkuu hebu chunguza na nyumba palipo ubalozi wa afrika ya kusini, nasikia kilikuwa kiwanja cha mashirika yetu kikauzwa kinyemela.
 
Kwa hali hii tusishangae kupigiwa simu na majambazi yakiwa magereza.
 
Back
Top Bottom