Askari wafichua ufisadi katika Jeshi la Magereza

Hawa wanabishana kuhusu ubinafsishaji.

Kwa hiyo tuwatilie mashaka watu wanaoandika JF,hawa watu Chadema nadhani,wanasema wanayafahamu matatizo ya TPA,wanayafamu matatizo ya ATCL. Ni kwa sabanu hazijabinafsishwa?
 
Kwa kweli sare za askari magereza zinatia aibu!
 
BAADA ya Rais John Magufuli kulipiga marufuku Jeshi la Magereza na majeshi mengine nchini kuruhusu askari wake kununua sare kwa watu binafsi, askari wa jeshi hilo wameibuka na kudai kuwa wamekuwa wanauziwa sare hizo kwa Sh 45,000.

Pia wamesema kofia na mikanda licha ya kuwa haiuzwi kwenye maduka ya watu binafsi, lakini upatikanaji wake pia ni wa shida, hali ambayo inawalazimu askari kutoa rushwa kwa wahifadhi bohari ili kupatiwa sare hizo.

Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti, askari mbalimbali waliohojiwa na gazeti hili licha ya kumpongeza Rais Magufuli kwa kulikemea suala hilo, walisema ni rahisi kushona kombati uraiani kwa kuwa vitambaa vinapatikana madukani, lakini kofia na mkanda ikichakaa askari analazimika kutoa pesa ili kupata mavazi hayo.

“Hizi kofia na mikanda inatolewa bohari ya jeshi, lakini kuupata huko mkanda au kofia lazima utoe rushwa kwa askari anayefanya kazi pale,” alisema mmoja wa askari aliyehojiwa na gazeti hili.

Wengi wa askari hao walisema kutokana na ugumu wa kupatikana na kofia na mikanda ya jeshi hilo, wengi wao wanaendelea kutumia kofia na mikanda waliyopewa wakati wanamaliza mafunzo.

Walisema kinachotolewa bure na jeshi hilo kwa sasa ni vyeo tu na sio sare nyingine yoyote. “Kofia hii ninayotumia pamoja na mkanda ni ile niliyopewa wakati namaliza depo (mafunzo) mwaka 2001,” alisema askari huyo ambaye ana miaka 15 sasa kazini na kuongeza, “Magereza wanachotoa bure kwa askari wao ni zile alama za cheo tu, vingine vyote vinavyohusu sare lazima askari ajinunulie.”

Wakati askari Magereza wanajinunulia sare, serikali imekuwa inatoa mamilioni ya fedha kwa ajili ya kuwahudumia askari hao.

Mfano, katika bajeti ya mwaka 2015/16 serikali ilitoa Sh bilioni 167.1 kwa jeshi hilo.

Kati ya fedha hizo, Sh bilioni 67.7 zilitolewa kwa jeshi hilo kwa ajili ya matumizi mengineyo, Sh bilioni 97.7 kama mishahara na fedha za maendeleo zilizotolewa kwa polisi ni Sh bilioni 1.6 Askari mmoja ambaye yuko mkoani Simiyu aliyefanya mahojiano na gazeti hili, alisema upatikanaji wa sare za Magereza kwa askari walioko mikoani ni mbaya, kwani wamekuwa wanalazimika kununua suruali na shati kati ya Sh 40,000 na 45,00 na viatu Sh 40,000.

“Juzi nilikuja hapo Dar es Salaam, nikawa na shida ya mkanda na kofia, nililazimika kutoa Sh 30,000 ambayo kofia niliinunua kwa Sh 10,000 na mkanda nilinunua kwa Sh 20,000,” alisema askari huyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini. Alipoulizwa anazipataje sare za jeshi hilo, alifafanua, “Sisi ukitaka sare unaenda kwa fundi unachukuliwa vipimo vya shati na suruali, unamtumia askari mwenzako wa Dar es Salaam anakununulia kitambaa na kukushonea, kisha anakutumia.”

Alisema yeye tangu amalize mafunzo mwaka 2009 hajawahi kupewa sare yoyote. “Sijawahi kupewa mkanda, kofia wala viatu vyote tunajinunulia... mkanda nilio nao na kofia ambayo imeisha nilipewa wakati namaliza mafunzo, hadi juzi nilipokuja huko ndipo nikafanya jitihada za kupata kofia na mkanda mwingine,” alisema.

Askari mwingine wa kike anayefanya kazi jijini Dar es Salaam, alisema wamekuwa wanajinunulia vitambaa katika duka la Khimji na kwenda uraiani kushona sare hizo.

“Unachagua mwenyewe fundi wako, lakini mita ya kitambaa tunanunua kwa Sh 8,000 pale kwa Khimji, mashono yanategemea na fundi utakayempelekea mwenyewe,” alisema askari huyo na kuongeza kuwa wamekuwa wananunua soksi pia kwa Sh 4,000 huko uraiani.

Aliongeza kuwa yeye alimaliza mafunzo mwaka 2001 na tangu wakati huo amekuwa anavaa mkanda na kofia aliopewa akiwa mafunzoni. “Sijawahi pata mgawo wowote wa sare tangu nitoke mafunzoni,” alieleza.

Alifafanua kuwa hata pale askari akihitaji kofia akienda kuomba bohari askari wanaofanya kazi kwenye hizo bohari wanataka wapewe rushwa ndipo waitoe.

“Hivi hivi huwezi pata kofia wala mkanda, lazima utoe kitu kidogo kwa anayefanya kazi bohari, kwa kweli mimi nilienda siku moja nikapata usumbufu sikuwahi tena kurudi huko,” aliongeza.

Kuhusu viatu, alisema wengi wa askari wanaofanya kazi Segerea na Ukonga wamekuwa wananunua viatu kwa mafundi wa uraiani ambao wanachonga viatu vinavyofanana na vya Magereza.

Alisema kwa sasa wananunua duka moja lililoko Mombasa, Ukonga ambako kuna huyo mtu anayevishona viatu vya aina hiyo. Askari mwingine wa kike alisema amekuwa anashona shati kwa Sh 10,000 uraiani na kwenye kiwanda cha Magereza anashona kwa Sh 5,000. Bei hiyo pia ni kwa sketi. Alisema sare kamili lazima igharimu mita 3.

“Pale dukani Kwa Khimji tunanunua kwa bei ya jumla ya shilingi elfu nane kwa meta, lakini ukienda maduka mengine ya rejareja unapigwa hadi shilingi elfu kumi na mbili kwa mita,” alibainisha.

Askari mwingine aliyeko mkoani Mwanza akizungumza na gazeti hili alisema wao kambini kwao walipatiwa mgawo wa mwisho mwaka 2012 na tangu wakati huo hawajapewa mgawo wowote.

Alisema wamekuwa wanaagiza sare Dar es Salaam kwa kutuma fedha Sh 40,000 au Sh 45,000 pamoja na vipimo, askari mwenzako anaenda kukununulia na kukutumia.

“Mimi hapa kofia yangu imetoboka, lakini kuipata kofia ni ngumu zaidi maana hizo hazipatikani kwingine kokote kama ilivyo kwa mkanda ambao nao unakaa nao miaka mingi hadi unabadilika rangi,”alisema askari huyo wa kiume.

Alisema mara nyingi wamekuwa wananunua viatu kwenye mitumba.

Alisema soksi pia wananunua zile zinazofanana na rangi ya magereza uraiani kwa Sh 5,000. Kutokana na jeshi la Magereza kutokuwa na utaratibu wa kuwagawia askari wake sare, wamekuwa hawana uwezo wa kudhibiti sare hizo kuvaliwa uraiani na kampuni zingine za ulinzi au hata mashule.

Kuna baadhi ya shule pia zimekuwa zinawashonea wanafunzi wao vitambaa hivyo vinavyotumiwa pia na askari wa magereza.

Mojawapo ya shule hizo ni Shule ya Sekondari ya Kitunda ambayo wanafunzi wanavaa sketi na suruali zinazofanana na sare ya Jeshi la Magereza. Kamishna Mkuu wa Magereza, John Minja alipotafutwa jana atoe ufafanuzi wa sababu ya askari wake kushona sare uraiani, simu yake iliita bila majibu.

Hata alipoandikiwa ujumbe mfupi wa maneno katika simu yake ya mkononi, alisema yuko kwenye kikao. Juzi Rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza kwenye kambi ya jeshi la Magereza ya Ukonga na kueleza kuwa na taarifa za askari wa jeshi hilo kununua sare kwenye maduka ya watu binafsi.

Alipiga marufuku askari hao kuendelea kununua sare uraiani badala yake akataka jeshi hilo liwape bure hizo sare.

“Wakati wa utawala wangu askari wote wapate sare bure, wataenda kununua uraiani nikimali za muda wangu. Na kuanzia leo maduka yote ya raia yaliyoko kwenye kambi za kijeshi yaondolewe na wauza sare hizo wakome kufanya biashara hiyo mara moja,” alisema.

Alisema kuna baadhi ya maofisa wa jeshi hilo la Magereza wamekuwa wanashirikiana na watu binafsi kufanya biashara ikiwemo kuuza sare za jeshi, jambo ambalo alisema ni kinyume kabisa na taratibu za jeshi hilo.

Chanzo:Habarileo.
Mwegulu anashunghulikia mambo ya yanga
Lizaboni Field Marshal
 
Duh,
Hii nchi ina mabo mengi!

Kadri mirija ya kifisadi inavyozibwa ndivyo na kelele za mafisadi na wapambe wao zitazidi kusikika.

Ikumbukwe mafisadi ni watu wenye pesa na ushawishi katika jamii na kwa maana hiyo kelele zao zitasikika zaidi kwa wananchi wajinga na wenye mitazamo tofauti kisiasa.

Serikali ya Rais Magufuli inakabiliwa na jukumu la kuelimisha hawa wajinga ili wasikubaliane na kelele za mafisadi na wapambe wao.

Kikubwa zaidi, Serikali iachane na kundi la wenye mitazamo tofauti ya kisiasa kwa sababu hawawezi kubadilika hata kama serikali itatoa huduma zote za kijamii, kiuchumi na kisiasa.
Uzuri ufisadi huu huletwa na CCM, hata mlipokuwa mnaambiwa ccm ni chama cha mafisadi mlipinga.
Hadi sasa tunawambia hiki chama ni cha kifisadi lkn mtaendelea kupinga hadi pale muone kwa macho yenu kama hili.
Wakati huu ccm inapinga ufisadi kwa mkono wa kulia na kuruhusu kwa mkono wa kushoto kama ilivyofanya ktk kubariki rushwa ya 10m
 
Kumbe mambo yalikuwa hivyo. Sikuiona hii taarifa kwa kweli bora alivyoomba kustaafu
 
Hayo Ni Ya Magereza Tu Unaona Rushwa Na Utata
Je? Police, Immigration, Fire,Tpdf
Naamini Kuna Mengi Sana Na Mazito Yamejificha Vikosini.

Cha Bure Ni Cheo Hivi Hapo Ndani Watu Yale Mapesa Ya Bajeti Huwa Wanakula Tu Na Kufanya Ukokotozi Hewa Wa Bajeti
ingawa sipo majeshin ila polis tpdf wanagawiwa uniform tena na viatu na mabegi kwa upande wa polisi mikanda,makoti na vitu vyote kwa ujumla labda majeshi mengine
 
Uzuri ufisadi huu huletwa na CCM, hata mlipokuwa mnaambiwa ccm ni chama cha mafisadi mlipinga.
Hadi sasa tunawambia hiki chama ni cha kifisadi lkn mtaendelea kupinga hadi pale muone kwa macho yenu kama hili.
Wakati huu ccm inapinga ufisadi kwa mkono wa kulia na kuruhusu kwa mkono wa kushoto kama ilivyofanya ktk kubariki rushwa ya 10m
Hata Lowassa tuliambiwa ni fisadi papa ambaye anatakiwa awe gerezani na tulipinga!
 
Na huo ndio ukweli,umesema vyema lkn cha ajabu alipohamia CDM mmekuwa wakwanza kusema kuwa ni fisadi.Yaani huwa nashangaa kuwa hizi ni akili za namna gani au matope?
 
Ni kweli ana kazi kubwa sana.

Kuziba mianya ya kifisadi kwa nchi kama Tanzania sio kazi ndogo.
Kwani hao wanaoziba mianya ya ufisadi wametoka sayari gani? Je, wao hawajashiriki kabisa vitendo vya ufisadi? Ni hadi hapo tutakapokuwa na mfumo unaowadhibiti hata wale "wanaoziba mianya ya ufisadi" ndipo angalau tutaweza kwenda hatua nyingi katika vita dhidi ya ufisadi, vinginevyo tutaendelea na blah blah zisizo na matokeo chanya!
 
Mkuu Punguza Unazi
Kwahiyo Rais Alipomhoji Waziri/Kamishna General Alikosea ? Kwenye Maovu Lolote Linaweza Kuzungumzwa Bila Hofu.

Huoni Askari Wamefunguka Kutaja Kero Ambazo Kwa Mujibu Wa Taratibu Za Majeshi Uniforms Zao Hupewa Bure Na Inapokwisha Tena Yaani Kiatu,Soksi,Suruali,Sketi,Mkanda,Shati,Kofia Hutolewa Bure.

Umeona Tsh 40000/- Wanazolipa Askari Ni Sawa
Kununua Vitambaa Na Kujishonea
najeshi yote yamepigwa upande wa kushoto ili kuyanusulu laazima yajenge ngazi kulia sababu majeshi yote yameingiliwa na siasa wakati jeshi na siasa ni vitu viwili tofauti .jeshi lina misingi yake ya utendaji .kwa sasa kila askari hana morali na kwa sababu ya siasa majeshin .zaman jeshi lilikuwa ni jeshi la command na sio kubembelezana kama sasaivi wala kuhojihoji mambo ya jeshi .mkikumbuka zaman Askali wa majeshi yote walikuwa wanalipwa pesa kidogo San mshahala but kazi walikuwa wanafanya kwa morali sio sasaivi askali wanalalamika Mara waongezewe pesa mala nini inafika hatua mpaka raia anahoji mambo ya majeshi ndio maana kaka yangu ameona aendelee kufanya mambo yake tu coz now majeshi yote ovyoooo
 
Na huo ndio ukweli,umesema vyema lkn cha ajabu alipohamia CDM mmekuwa wakwanza kusema kuwa ni fisadi.Yaani huwa nashangaa kuwa hizi ni akili za namna gani au matope?
Akili zipi?

Hizi akili za kumfanya mgombea Urais fisadi anayetakiwa kuwa gerezani!
 
BAADA ya Rais John Magufuli kulipiga marufuku Jeshi la Magereza na majeshi mengine nchini kuruhusu askari wake kununua sare kwa watu binafsi, askari wa jeshi hilo wameibuka na kudai kuwa wamekuwa wanauziwa sare hizo kwa Sh 45,000.

Pia wamesema kofia na mikanda licha ya kuwa haiuzwi kwenye maduka ya watu binafsi, lakini upatikanaji wake pia ni wa shida, hali ambayo inawalazimu askari kutoa rushwa kwa wahifadhi bohari ili kupatiwa sare hizo.

Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti, askari mbalimbali waliohojiwa na gazeti hili licha ya kumpongeza Rais Magufuli kwa kulikemea suala hilo, walisema ni rahisi kushona kombati uraiani kwa kuwa vitambaa vinapatikana madukani, lakini kofia na mkanda ikichakaa askari analazimika kutoa pesa ili kupata mavazi hayo.

“Hizi kofia na mikanda inatolewa bohari ya jeshi, lakini kuupata huko mkanda au kofia lazima utoe rushwa kwa askari anayefanya kazi pale,” alisema mmoja wa askari aliyehojiwa na gazeti hili.

Wengi wa askari hao walisema kutokana na ugumu wa kupatikana na kofia na mikanda ya jeshi hilo, wengi wao wanaendelea kutumia kofia na mikanda waliyopewa wakati wanamaliza mafunzo.

Walisema kinachotolewa bure na jeshi hilo kwa sasa ni vyeo tu na sio sare nyingine yoyote. “Kofia hii ninayotumia pamoja na mkanda ni ile niliyopewa wakati namaliza depo (mafunzo) mwaka 2001,” alisema askari huyo ambaye ana miaka 15 sasa kazini na kuongeza, “Magereza wanachotoa bure kwa askari wao ni zile alama za cheo tu, vingine vyote vinavyohusu sare lazima askari ajinunulie.”

Wakati askari Magereza wanajinunulia sare, serikali imekuwa inatoa mamilioni ya fedha kwa ajili ya kuwahudumia askari hao.

Mfano, katika bajeti ya mwaka 2015/16 serikali ilitoa Sh bilioni 167.1 kwa jeshi hilo.

Kati ya fedha hizo, Sh bilioni 67.7 zilitolewa kwa jeshi hilo kwa ajili ya matumizi mengineyo, Sh bilioni 97.7 kama mishahara na fedha za maendeleo zilizotolewa kwa polisi ni Sh bilioni 1.6 Askari mmoja ambaye yuko mkoani Simiyu aliyefanya mahojiano na gazeti hili, alisema upatikanaji wa sare za Magereza kwa askari walioko mikoani ni mbaya, kwani wamekuwa wanalazimika kununua suruali na shati kati ya Sh 40,000 na 45,00 na viatu Sh 40,000.

“Juzi nilikuja hapo Dar es Salaam, nikawa na shida ya mkanda na kofia, nililazimika kutoa Sh 30,000 ambayo kofia niliinunua kwa Sh 10,000 na mkanda nilinunua kwa Sh 20,000,” alisema askari huyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini. Alipoulizwa anazipataje sare za jeshi hilo, alifafanua, “Sisi ukitaka sare unaenda kwa fundi unachukuliwa vipimo vya shati na suruali, unamtumia askari mwenzako wa Dar es Salaam anakununulia kitambaa na kukushonea, kisha anakutumia.”

Alisema yeye tangu amalize mafunzo mwaka 2009 hajawahi kupewa sare yoyote. “Sijawahi kupewa mkanda, kofia wala viatu vyote tunajinunulia... mkanda nilio nao na kofia ambayo imeisha nilipewa wakati namaliza mafunzo, hadi juzi nilipokuja huko ndipo nikafanya jitihada za kupata kofia na mkanda mwingine,” alisema.

Askari mwingine wa kike anayefanya kazi jijini Dar es Salaam, alisema wamekuwa wanajinunulia vitambaa katika duka la Khimji na kwenda uraiani kushona sare hizo.

“Unachagua mwenyewe fundi wako, lakini mita ya kitambaa tunanunua kwa Sh 8,000 pale kwa Khimji, mashono yanategemea na fundi utakayempelekea mwenyewe,” alisema askari huyo na kuongeza kuwa wamekuwa wananunua soksi pia kwa Sh 4,000 huko uraiani.

Aliongeza kuwa yeye alimaliza mafunzo mwaka 2001 na tangu wakati huo amekuwa anavaa mkanda na kofia aliopewa akiwa mafunzoni. “Sijawahi pata mgawo wowote wa sare tangu nitoke mafunzoni,” alieleza.

Alifafanua kuwa hata pale askari akihitaji kofia akienda kuomba bohari askari wanaofanya kazi kwenye hizo bohari wanataka wapewe rushwa ndipo waitoe.

“Hivi hivi huwezi pata kofia wala mkanda, lazima utoe kitu kidogo kwa anayefanya kazi bohari, kwa kweli mimi nilienda siku moja nikapata usumbufu sikuwahi tena kurudi huko,” aliongeza.

Kuhusu viatu, alisema wengi wa askari wanaofanya kazi Segerea na Ukonga wamekuwa wananunua viatu kwa mafundi wa uraiani ambao wanachonga viatu vinavyofanana na vya Magereza.

Alisema kwa sasa wananunua duka moja lililoko Mombasa, Ukonga ambako kuna huyo mtu anayevishona viatu vya aina hiyo. Askari mwingine wa kike alisema amekuwa anashona shati kwa Sh 10,000 uraiani na kwenye kiwanda cha Magereza anashona kwa Sh 5,000. Bei hiyo pia ni kwa sketi. Alisema sare kamili lazima igharimu mita 3.

“Pale dukani Kwa Khimji tunanunua kwa bei ya jumla ya shilingi elfu nane kwa meta, lakini ukienda maduka mengine ya rejareja unapigwa hadi shilingi elfu kumi na mbili kwa mita,” alibainisha.

Askari mwingine aliyeko mkoani Mwanza akizungumza na gazeti hili alisema wao kambini kwao walipatiwa mgawo wa mwisho mwaka 2012 na tangu wakati huo hawajapewa mgawo wowote.

Alisema wamekuwa wanaagiza sare Dar es Salaam kwa kutuma fedha Sh 40,000 au Sh 45,000 pamoja na vipimo, askari mwenzako anaenda kukununulia na kukutumia.

“Mimi hapa kofia yangu imetoboka, lakini kuipata kofia ni ngumu zaidi maana hizo hazipatikani kwingine kokote kama ilivyo kwa mkanda ambao nao unakaa nao miaka mingi hadi unabadilika rangi,”alisema askari huyo wa kiume.

Alisema mara nyingi wamekuwa wananunua viatu kwenye mitumba.

Alisema soksi pia wananunua zile zinazofanana na rangi ya magereza uraiani kwa Sh 5,000. Kutokana na jeshi la Magereza kutokuwa na utaratibu wa kuwagawia askari wake sare, wamekuwa hawana uwezo wa kudhibiti sare hizo kuvaliwa uraiani na kampuni zingine za ulinzi au hata mashule.

Kuna baadhi ya shule pia zimekuwa zinawashonea wanafunzi wao vitambaa hivyo vinavyotumiwa pia na askari wa magereza.

Mojawapo ya shule hizo ni Shule ya Sekondari ya Kitunda ambayo wanafunzi wanavaa sketi na suruali zinazofanana na sare ya Jeshi la Magereza. Kamishna Mkuu wa Magereza, John Minja alipotafutwa jana atoe ufafanuzi wa sababu ya askari wake kushona sare uraiani, simu yake iliita bila majibu.

Hata alipoandikiwa ujumbe mfupi wa maneno katika simu yake ya mkononi, alisema yuko kwenye kikao. Juzi Rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza kwenye kambi ya jeshi la Magereza ya Ukonga na kueleza kuwa na taarifa za askari wa jeshi hilo kununua sare kwenye maduka ya watu binafsi.

Alipiga marufuku askari hao kuendelea kununua sare uraiani badala yake akataka jeshi hilo liwape bure hizo sare.

“Wakati wa utawala wangu askari wote wapate sare bure, wataenda kununua uraiani nikimaliza muda wangu. Na kuanzia leo maduka yote ya raia yaliyoko kwenye kambi za kijeshi yaondolewe na wauza sare hizo wakome kufanya biashara hiyo mara moja,” alisema.

Alisema kuna baadhi ya maofisa wa jeshi hilo la Magereza wamekuwa wanashirikiana na watu binafsi kufanya biashara ikiwemo kuuza sare za jeshi, jambo ambalo alisema ni kinyume kabisa na taratibu za jeshi hilo.

Chanzo:Habarileo.

ili haya mambo yaishe hasa upande wa combat dawa ni kubadiri aina na muonekano wa sare za hawa maaskari...itafutwe combat ambayo haiendani na matumizi yoyote ndani ya jamii..kama.ile ya JWTZ..sasa hizi za polis na magereza kuanzia chekechea mpka makondakta wanazivaa..

alafu hizi combat zao za zamani mno toka mkoroni ameondoka hadi sasa anataka.kurudi bado wanazivaa tu.
 
Askari magereza wanafiki sana na wamezoea kuchungulia minduku ya wafungwa/mahabusu.
Bonge la laana.
 
Mkoroni?
Ndio nani huyu! Alikuwa Luteni Usu au?
 
Askari magereza wanafiki sana na wamezoea kuchungulia minduku ya wafungwa/mahabusu.
Bonge la laana.
Unafiki wao nini au baba yako ndo katemeshwa mzigo mkuu maana naona povu sana baada ya kuona taarifa ya Minja kusepa kwao uchagani
 
Askari anaomba rushwa kwa askari mwenzie ili ampatie mkanda au kofia. Ndio maana askari na rushwa ni kama uji na mgonjwa
 
BAADA ya Rais John Magufuli kulipiga marufuku Jeshi la Magereza na majeshi mengine nchini kuruhusu askari wake kununua sare kwa watu binafsi, askari wa jeshi hilo wameibuka na kudai kuwa wamekuwa wanauziwa sare hizo kwa Sh 45,000.

Pia wamesema kofia na mikanda licha ya kuwa haiuzwi kwenye maduka ya watu binafsi, lakini upatikanaji wake pia ni wa shida, hali ambayo inawalazimu askari kutoa rushwa kwa wahifadhi bohari ili kupatiwa sare hizo.

Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti, askari mbalimbali waliohojiwa na gazeti hili licha ya kumpongeza Rais Magufuli kwa kulikemea suala hilo, walisema ni rahisi kushona kombati uraiani kwa kuwa vitambaa vinapatikana madukani, lakini kofia na mkanda ikichakaa askari analazimika kutoa pesa ili kupata mavazi hayo.

“Hizi kofia na mikanda inatolewa bohari ya jeshi, lakini kuupata huko mkanda au kofia lazima utoe rushwa kwa askari anayefanya kazi pale,” alisema mmoja wa askari aliyehojiwa na gazeti hili.

Wengi wa askari hao walisema kutokana na ugumu wa kupatikana na kofia na mikanda ya jeshi hilo, wengi wao wanaendelea kutumia kofia na mikanda waliyopewa wakati wanamaliza mafunzo.

Walisema kinachotolewa bure na jeshi hilo kwa sasa ni vyeo tu na sio sare nyingine yoyote. “Kofia hii ninayotumia pamoja na mkanda ni ile niliyopewa wakati namaliza depo (mafunzo) mwaka 2001,” alisema askari huyo ambaye ana miaka 15 sasa kazini na kuongeza, “Magereza wanachotoa bure kwa askari wao ni zile alama za cheo tu, vingine vyote vinavyohusu sare lazima askari ajinunulie.”

Wakati askari Magereza wanajinunulia sare, serikali imekuwa inatoa mamilioni ya fedha kwa ajili ya kuwahudumia askari hao.

Mfano, katika bajeti ya mwaka 2015/16 serikali ilitoa Sh bilioni 167.1 kwa jeshi hilo.

Kati ya fedha hizo, Sh bilioni 67.7 zilitolewa kwa jeshi hilo kwa ajili ya matumizi mengineyo, Sh bilioni 97.7 kama mishahara na fedha za maendeleo zilizotolewa kwa polisi ni Sh bilioni 1.6 Askari mmoja ambaye yuko mkoani Simiyu aliyefanya mahojiano na gazeti hili, alisema upatikanaji wa sare za Magereza kwa askari walioko mikoani ni mbaya, kwani wamekuwa wanalazimika kununua suruali na shati kati ya Sh 40,000 na 45,00 na viatu Sh 40,000.

“Juzi nilikuja hapo Dar es Salaam, nikawa na shida ya mkanda na kofia, nililazimika kutoa Sh 30,000 ambayo kofia niliinunua kwa Sh 10,000 na mkanda nilinunua kwa Sh 20,000,” alisema askari huyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini. Alipoulizwa anazipataje sare za jeshi hilo, alifafanua, “Sisi ukitaka sare unaenda kwa fundi unachukuliwa vipimo vya shati na suruali, unamtumia askari mwenzako wa Dar es Salaam anakununulia kitambaa na kukushonea, kisha anakutumia.”

Alisema yeye tangu amalize mafunzo mwaka 2009 hajawahi kupewa sare yoyote. “Sijawahi kupewa mkanda, kofia wala viatu vyote tunajinunulia... mkanda nilio nao na kofia ambayo imeisha nilipewa wakati namaliza mafunzo, hadi juzi nilipokuja huko ndipo nikafanya jitihada za kupata kofia na mkanda mwingine,” alisema.

Askari mwingine wa kike anayefanya kazi jijini Dar es Salaam, alisema wamekuwa wanajinunulia vitambaa katika duka la Khimji na kwenda uraiani kushona sare hizo.

“Unachagua mwenyewe fundi wako, lakini mita ya kitambaa tunanunua kwa Sh 8,000 pale kwa Khimji, mashono yanategemea na fundi utakayempelekea mwenyewe,” alisema askari huyo na kuongeza kuwa wamekuwa wananunua soksi pia kwa Sh 4,000 huko uraiani.

Aliongeza kuwa yeye alimaliza mafunzo mwaka 2001 na tangu wakati huo amekuwa anavaa mkanda na kofia aliopewa akiwa mafunzoni. “Sijawahi pata mgawo wowote wa sare tangu nitoke mafunzoni,” alieleza.

Alifafanua kuwa hata pale askari akihitaji kofia akienda kuomba bohari askari wanaofanya kazi kwenye hizo bohari wanataka wapewe rushwa ndipo waitoe.

“Hivi hivi huwezi pata kofia wala mkanda, lazima utoe kitu kidogo kwa anayefanya kazi bohari, kwa kweli mimi nilienda siku moja nikapata usumbufu sikuwahi tena kurudi huko,” aliongeza.

Kuhusu viatu, alisema wengi wa askari wanaofanya kazi Segerea na Ukonga wamekuwa wananunua viatu kwa mafundi wa uraiani ambao wanachonga viatu vinavyofanana na vya Magereza.

Alisema kwa sasa wananunua duka moja lililoko Mombasa, Ukonga ambako kuna huyo mtu anayevishona viatu vya aina hiyo. Askari mwingine wa kike alisema amekuwa anashona shati kwa Sh 10,000 uraiani na kwenye kiwanda cha Magereza anashona kwa Sh 5,000. Bei hiyo pia ni kwa sketi. Alisema sare kamili lazima igharimu mita 3.

“Pale dukani Kwa Khimji tunanunua kwa bei ya jumla ya shilingi elfu nane kwa meta, lakini ukienda maduka mengine ya rejareja unapigwa hadi shilingi elfu kumi na mbili kwa mita,” alibainisha.

Askari mwingine aliyeko mkoani Mwanza akizungumza na gazeti hili alisema wao kambini kwao walipatiwa mgawo wa mwisho mwaka 2012 na tangu wakati huo hawajapewa mgawo wowote.

Alisema wamekuwa wanaagiza sare Dar es Salaam kwa kutuma fedha Sh 40,000 au Sh 45,000 pamoja na vipimo, askari mwenzako anaenda kukununulia na kukutumia.

“Mimi hapa kofia yangu imetoboka, lakini kuipata kofia ni ngumu zaidi maana hizo hazipatikani kwingine kokote kama ilivyo kwa mkanda ambao nao unakaa nao miaka mingi hadi unabadilika rangi,”alisema askari huyo wa kiume.

Alisema mara nyingi wamekuwa wananunua viatu kwenye mitumba.

Alisema soksi pia wananunua zile zinazofanana na rangi ya magereza uraiani kwa Sh 5,000. Kutokana na jeshi la Magereza kutokuwa na utaratibu wa kuwagawia askari wake sare, wamekuwa hawana uwezo wa kudhibiti sare hizo kuvaliwa uraiani na kampuni zingine za ulinzi au hata mashule.

Kuna baadhi ya shule pia zimekuwa zinawashonea wanafunzi wao vitambaa hivyo vinavyotumiwa pia na askari wa magereza.

Mojawapo ya shule hizo ni Shule ya Sekondari ya Kitunda ambayo wanafunzi wanavaa sketi na suruali zinazofanana na sare ya Jeshi la Magereza. Kamishna Mkuu wa Magereza, John Minja alipotafutwa jana atoe ufafanuzi wa sababu ya askari wake kushona sare uraiani, simu yake iliita bila majibu.

Hata alipoandikiwa ujumbe mfupi wa maneno katika simu yake ya mkononi, alisema yuko kwenye kikao. Juzi Rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza kwenye kambi ya jeshi la Magereza ya Ukonga na kueleza kuwa na taarifa za askari wa jeshi hilo kununua sare kwenye maduka ya watu binafsi.

Alipiga marufuku askari hao kuendelea kununua sare uraiani badala yake akataka jeshi hilo liwape bure hizo sare.

“Wakati wa utawala wangu askari wote wapate sare bure, wataenda kununua uraiani nikimaliza muda wangu. Na kuanzia leo maduka yote ya raia yaliyoko kwenye kambi za kijeshi yaondolewe na wauza sare hizo wakome kufanya biashara hiyo mara moja,” alisema.

Alisema kuna baadhi ya maofisa wa jeshi hilo la Magereza wamekuwa wanashirikiana na watu binafsi kufanya biashara ikiwemo kuuza sare za jeshi, jambo ambalo alisema ni kinyume kabisa na taratibu za jeshi hilo.

Chanzo:Habarileo.
Wanajamvi hivi hamjamuelewa mleta mada?

Habari hii si mpya ni siku nyingi tu.
Mleta mada kainukuu akiwa na lengo moja kuwaondoa katika mada zinazogusa masilahi yenu

Kama mnakumbuka, kuna hili la Dangote ambalo ukiliangalia kwa undani kuna tatizo kubwa
Waziri kasema alidanganya, waziri mwingine akiongelea makaa, mwingine gesi n.k.

Mada hii imeletwa ili kuwaondoa katika hili la kiwanda cha Dangote kilicholetwa na serikali ya CCM ya JK na ambacho kimefungwa kwasababu hapakazi wameamua kuelekeza wawezekezaji wafanye nini

Hii mada ni kufunika nyuso zenu, kuwaondoa katika issue na kujadili kauli ya askari Magereza ambaye hakutaka kutajwa jina lake!!!!
 
Back
Top Bottom