Askari wa Voda fasta

Askari wa Voda fasta

Everyday

Member
Joined
May 6, 2014
Posts
11
Reaction score
2
Jamani naomba ufafanuzi. Hivi ni kweli kuwa jukumu, lengo na madhumuni makubwa kabisa ya polisi hawa maarufu kama voda fasta ni kukamata na kukimbizana na pikipiki?

Inaniwia vigumu kuamini hivyo kwani kwa nikionacho katika mji wa Morogoro bila kujua kinachoendelea ndani ya miji mingine kinanitia simanzi na kero kwa kuona jinsi nguvu kazi hii inavyotumika kinyume na matarajio ya raia.

Kutwa nzima polisi hawa wako busy katika highways za Iringa, Dar, Dodoma na mitaa ya mjini Morogoro na kila ukiwakuta lazima utawakuta kwenye matukio ya kuwakamata waendesha pikipiki tu.

Ninafahamu kuwa wana majukumu mengine zaidi ya kufanya na ambayo ni mazito na muhimu kuliko hayo badala ya kuvaa kikomandoo na kubebelea silaha iliyosheheni risasi kwa minajili ya kukimbizana na waendesha pikipiki.

Hivi taarifa ya kazi ya siku wanaiandikaje watu hawa? Na huko CCP ni kweli kuwa mafunzo yao yalikuw maalumu kwa ajili hii tu?

Ningependa kufahamishwa.
 
voda fasta ni askari wa opareshen wa kila tukio lakini kwa morogoro wamezidi kupita kiasi kufukuzana na bodaboda na ndio maana ajali kila mara zinatokea
 
Hivyo? Hebu kuwa raia mwema kwaripoti hili kwa RPC wa Morogoro..utakuwa umetusaidia sana mkuu!
 
Jamani naomba ufafanuzi. Hivi ni kweli kuwa jukumu, lengo na madhumuni makubwa kabisa ya polisi hawa maarufu kama voda fasta ni kukamata na kukimbizana na pikipiki?

Inaniwia vigumu kuamini hivyo kwani kwa nikionacho katika mji wa Morogoro bila kujua kinachoendelea ndani ya miji mingine kinanitia simanzi na kero kwa kuona jinsi nguvu kazi hii inavyotumika kinyume na matarajio ya raia.

Kutwa nzima polisi hawa wako busy katika highways za Iringa, Dar, Dodoma na mitaa ya mjini Morogoro na kila ukiwakuta lazima utawakuta kwenye matukio ya kuwakamata waendesha pikipiki tu.

Ninafahamu kuwa wana majukumu mengine zaidi ya kufanya na ambayo ni mazito na muhimu kuliko hayo badala ya kuvaa kikomandoo na kubebelea silaha iliyosheheni risasi kwa minajili ya kukimbizana na waendesha pikipiki.

Hivi taarifa ya kazi ya siku wanaiandikaje watu hawa? Na huko CCP ni kweli kuwa mafunzo yao yalikuw maalumu kwa ajili hii tu?

Ningependa kufahamishwa.

Ufahamishwe nini sasa mbona unaelewa tu.
 
Back
Top Bottom