Askari wa usalama barabarani watumie mashine za EFD

Askari wa usalama barabarani watumie mashine za EFD

Haisaidii dawa ni kufuta kitengo cha trafiki na kuweka kampuni binafsi
 
Jaman mnasemaje?

Napendekeza trafic police wapewe zile mashine za TRA kwa ajili ya kutupigia faini.
Hivi vitabu vyao vinanipa shaka!!
 
Wakati kila kitengo kina kiwango kinachowasilisha kwa RTO kila wiki naye kuwasilisha kiwango flani kila mwezi kwa RPC!

Haiwezekani, mtu akipewa tochi anaambiwa kabisa mwisho wa wiki alete laki 7. Yani kama biashara ya coaster. Unafikiri hao viongozi watakubali mashine za EFD!!

Halafu ili zifanye kazi vizuri wapunguze adhabu kuwa elfu 10, maana wakiacha elfu 30 halafu unganganie kulipa electronic unaweza tafutiwa makosa 7, mpaka gauge ya mafuta kuwa empty itakua kosa la fine ili tu utoe rushwa uachiwe!
 
Hasa zile tochi ziunganishwe na machine za EFD ili akipiga tochi tu isome kule TRA kuongeza mapato ya nchi yetu. POLISI wanatia aibu siku hizi hawana hata aibu wanakula mpaka za wafadhiri.
 
Kwanini hili swali lisiwekwe kwenye yale maswali ya ndio au hapana ITV? hapo wananchi watapiga kura hata wale wasiokuepo humu JF. Hii hoja ina mashiko sana.
 
j smart ndogo tu wanawaibia sana ,hvi kama yule aliyebambwa segerea c alikuwa anawaandikia watu fine wakati kumbe ye mwenyewe ni askari feki atatoa wapi risiti ya ukweli loo watumie kwani hizo daftar wanabebaje?au waweke kituo unapigwa fine unaenda kulipa unapewa rist ya tra

wale tu mshahara mdogo mno
 
Back
Top Bottom