Rashda Zunde
Senior Member
- May 28, 2022
- 199
- 231
Rais Samia amewaonya askari wa uhamiaji wasio waaadilifu, wanaohujumu fedha za vibali vya makazi na viza na kutaka hatua zichukuliwe kwa wote wanaofanya uhujumu huo.
Rais Samia amesema kupitia utafiti mdogo uliofanyika kwenye mkoa wa Dar es Salaam na Zanzibar wamebaini upotevu mkubwa wa fedha unaofanywa na maafisa uhamiaji na kutaka vitendo hivyo vikomeshwe.
“Wale wote waliohusika na mambo yale washughulikiwe,” ameongeza Rais.
Ili kukomesha vitendo vya vya rushwa na unyanyasaji wa raia wa kigeni unaofanywa kwa maafisa wahamiaji, Rais Samia amesema kuwa kuna haja maafisa hao wanaofanya vitendo hivyo kurudi tena kwenye mafunzo ili wakumbushwe wajibu wao.
Aidha Rais Samia amesema Serikali imetoa fedha ili maafisa wa vikosi vyote vya Tanzania wapate mafunzo yatakayo wawezesha kuongeza ufanisi kwenye vituo vyao vya kazi.