Askari wa SMZ adaiwa kunaswa akisafirisha dawa za kulevya

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Askari wa moja ya vikosi vya Ulinzi na usalama vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Juma Abdalla Khamis (34) amekamatwa akiwa na vifuko 31 vikiwa na kete 3,198 zinazodhaniwa kuwa dawa za kulevya aina ya Heroin.
Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu jana, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Zanzibar, Kanali Burhan Zuberi Nassor amethibitisha kukamatwa askari huyo.

Kanali Zuberi Nassor alisema tukio hilo lilitokea Aprili 11, 2023 katika uwanja wa ndege wa Pemba. Bila kutaja askari huyo ni mtumishi wa kikosi gani kutokana na upelelezi unaoendelea, alisema alikamatwa na maofisa wa mamlaka hiyo saa 10:30 jioni katika uwanja wa ndege Pemba.

"Mtuhumiwa ni mkazi wa Kibanda Maiti Unguja, hizi ni taarifa za awali, bado uchunguzi unaendelea, taarifa zaidi zitatolewa baada ya uchunguzi kukamilika," alisema Nassor.

Hali ilivyo
Septemba mwaka jana, Athumani Akida Juma (32), mkazi wa Nungwi alikamatwa na pakiti 20 zenye kete 2,401 zinazodaiwa ni dawa za kulevya aina ya heroin.

Pia, Februari mwaka huohuo Jeshi la polisi liliwakamata wanawake wawili wakiwa na unga unaodhaniwa ni wa dawa za kulevya aina ya heroin wenye uzito wa wastani wa kilo 5.62 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa AbeidAman Karume.

Kijana huyo alikamatwa katika operesheni na doria za ukamataji wahalifu wanaojihusisha kuuza na kusambaza dawa za kulevya nchini. Katika operesheni hiyo walikamata mzigo kisiwani Pemba ulio-elekezwa ukiwa na kete 4,000 za bangi, huku upelelezi wa kuwatafuta wahusika ukiendelea.

Kwa twakimu za mamlaka hiyo zilizotolewa Septemba mwaka jana, kesi 215 zinazohusu dawa hizo zilikuwa katika hatua mbalimbali katika vyombo vya sheria.

Hatua hiyo ilikuja baada ya mamlaka hiyo kuanza kufanya kazi Machi mwaka jana ikiwa na nguvu zote za kukamata, kupeleleza na kushtaki baada ya kufanyiwa marekebisho ya sheria ambapo awali ilionekana kutokuwa na meno ya kufanya hivyo.

Mmoja wa vijana ambaye alidai alikuwa mtumiaji wa dawa hizo baadaye akaacha, Issa Muhdin
Issa alisema mtandao wa dawa za kulevya ni mkubwa na iwapo mamlaka itataka kufanikiwa haina budi kuwashirikisha vijana hao.
 
Zenji kunatrend sana aisee
 
Back
Top Bottom