Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 752
- 1,810
Wanakijiji wanne wamepigwa risasi na kufa jana na wengine wanne kujeruhiwa vibaya wakiwemo watoto wa shule baada ya askari hao wa doria katika msitu wa oldonyosambu, wilaya ya Arumeru kuwakuta wanakijiji hao wameingiza mifugo yao kwenye hifadhi ya msitu huo na kuanza kuwamiminia risasi ovyo, majeruhi wamelazwa hospital ya Mt Meru, na maiti wapo Moshwale mt. Meru, diwani wa kata hiyo amethibitisha.