Kwanza nilivyomuna tu Changonja nikajua hapa movie. Kuna watu wawili nikiwaona tu hao kwenye issue yoyote najua akina Kanumba cha mtoto hao ni Chagonja na mwenziwe Kova mtoto wa Dar, hao wazee wa karata 3. Wazee waongo hao hata macho hawapepesi. Huwa wanachomekewa huko kusiko na jina bali wenyewe huwa wanaita ngazi za juu. Wanakujaga na hekaya za kizamani sana bila kujua huko wanakolala ndio sisi tumeamkia. Bado wanaishi dunia ya gazezi la mzalendo na vichekesho vya kina chakubanga, bila kujua siku hizi dunia ni digital. Wanaongea mambo mpaka unajiuliza hawa wazee wako sawa kweli. Ukikutana na vijana wao wa jeshi la polisi mpaka wanapata hasira jinsi wazee wanavyowapeleka kizamani. Ila ndio hivyo huko jeshini wanasema hakuna kuhoji ni kutekeleza kwanza longolongo baadae. Wenyewe wanajua mambo mawili tu nchi hii chadema na magaidi mwisho wa habari. Haya mambo mengine sijui mbinu za kisasa unawachanganya maana hata kugoogle kwenye internet kwao ni janga.
Kwa hiyo usishangae ukiona wanaleta mambo ya namna hiyo, ila ni sisi wenyewe ndio tumeruhusu viongozi wasanii wakakaa madarakani hivyo hawataki weledi bali mazoea ili wapige deal, na huwa wanaamini sisi waafrika hatujui kitu bali wazungu. Ngoja wamuone mzungu hata kama hajui kusoma na kuandika nakwambia kwenye kiti watampisha. Na wazungu si unajua wanatujua kwamba tunawatetemekea wanapiga deal wanavyopenda nchi hii. Ole wako sasa umguse mzungu akipiga simu tu wanamuuliza nani anakusumbua, akikohoa tu utaona PT zimeshehena maaskari tayari kwa kipigo.