Askari wa JWTZ aliyefariki Tanga Azikwa

Ta Muganyizi

R I P
Oct 19, 2010
5,361
2,734
Aliyeuawa azikwa

Mwili wa askari wa JWTZ, Said Kajembe aliyefariki dunia katika Hospitali ya Bombo baada ya kujeruhiwa katika mapambano hayo uliagwa jana katika kikosi cha JWTZ Pande na baadaye kusafirishwa kwenda kijijini kwake, Kwashemshi, Korogwe kwa mazishi.
==========

Dar/Tanga. Ni dhahiri kwamba sasa hali si shwari nchini kutokana na mfululizo wa matukio ya uhalifu ikiwamo kuvamiwa vituo vya polisi, kuuawa kwa polisi na jingine kubwa la juzi la mapigano baina ya polisi wakisaidiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) dhidi ya makundi yanayodhaniwa kuwa ni ya ama ujambazi au kigaidi.

Matukio hayo yanayoliweka Taifa katika wasiwasi zaidi hasa wakati huu wa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, yamekuwa gumzo kila kona ya nchi kutokana na utata wake.

Tukio la Tanga

Katika mfululizo wa matukio hayo, juzi risasi zilirindima mkoani Tanga kwa zaidi ya saa 48 wakati Polisi na askari wa JWTZ waliposhirikiana kupambana na wahalifu hao.

Katika mapambano hayo, askari mmoja wa JWTZ alipoteza maisha na wapiganaji wengine zaidi ya sita kujeruhiwa.

Jana, askari hao waliendelea na operesheni ya kuwasaka watuhumiwa na hadi tunakwenda mitamboni hakukuwa na taarifa zozote za kukamatwa kwao.

Mbali na kutokamatwa watu hao ambao hawajajulikana ni wahalifu wa aina gani, pia silaha zilizokuwa zinasakwa hazikukutwa kwenye Mapango ya Amboni kama ilivyokuwa ikihisiwa, zaidi ya pikipiki moja mbovu na baiskeli tatu. Habari zilizopatikana jana zimedokeza kuwa vikosi vilivyopo katika operesheni hiyo vimebadili mbinu za kuwasaka majambazi hao.

Vilevile, wakazi wa kitongoji cha Karasha Amboni ambao walihama kukimbia mapigano, hadi jana walikuwa hawajarejea majumbani mwao.

Majeruhi

Kwa upande wa majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo, wanaendelea na matibabu huku madaktari na wauguzi wakitakiwa kutoa taarifa za kila anayefikishwa hapo akiwa majeruhi.

"Tumepewa maelekezo kwamba kila raia anayefikishwa hapa akiwa na majeraha tutoe taarifa haraka kwa uongozi kwani kuna uwezekano wa kuletwa waliofanya mashambulizi kwenye mapango," alisema mmoja wa wauguzi kwa sharti la kutotajwa jina.

Wakazi wa Kijiji cha Kiomoni kilicho jirani na mapango ya Amboni, walisema baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikipotosha taarifa juu ya eneo yalikofanyika mapambano, kwamba ni mapango ambayo hutembelewa na watalii na wageni wengine, wakati si kweli.

"Katika eneo la Amboni kuna jumla ya mapango 13 yaliyogunduliwa lakini yanayotumika ni mawili, kwa hiyo kunakoendeshwa mapambano ni pango la mbali kabisa na sehemu inayotembelewa na wageni," alisema Hussein ambaye hufanya kazi ya kupiga picha katika eneo hilo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Frasser Kashai alisema jeshi hilo lisingeweza kuzungumza na vyombo vya habari jana kwa sababu hakukuwa na mtu yeyote aliyekamatwa na operesheni ilikuwa inaendelea. "Sisi sote tuko huku kwenye operesheni na Kamishna (Paul Chagonja wa Operesheni na Mafunzo) hataweza kuzungumza na waandishi wa habari leo (jana) kwa sababu taarifa ni zilezile za jana (juzi)," alisema Kamanda Kashai.

Kaimu Kamanda wa Makosa ya Jinai nchini, DCI Diwani Athumani alisema matukio ya uhalifu yanayotokea nchini ni mapya na yanayochochewa na ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano.

"Haya ni mambo mapya kwa hapa nchini, lakini ninachoweza kusema ni kuwa, hawa ni wahalifu na ni wachache kiasi kwamba nina uhakika Jeshi la Polisi lina uwezo wa kuwadhibiti," alisema.

Akizungumzia hali hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mathias Chikawe alisema polisi wanafahamu kuwa kuna hali ya hatari na wameshaongeza ulinzi katika maeneo yote.

"Sisi tunafahamu, ndiyo maana askari wetu tumeshawaambia kuwa sasa hakuna kuning'iniza silaha begani… sasa silaha iwe mkononi wakati wowote kwa mapambano," alisema Waziri Chikawe na kuongeza kuwa juhudi zaidi zinaendelea kufanyika ili kulinda usalama wa raia na kuifanya Tanzania ibaki kuwa kisiwa cha amani.

"Umakini unaendelea, tunahimiza doria na ninakuhakikishia tunapambana nao," alisema Waziri Chikawe huku akisisitiza kuwa ni uhalifu wa kawaida.

Wakati Chikawe akisema hayo, kumekuwapo na taarifa katika vyombo vya habari na wachambuzi wa masuala ya kiusalama zikihusisha uhalifu huo na matukio ya kigaidi yenye lengo la ama kulipiza kisasi cha polisi kupambana na uhalifu au kuteka silaha za kufanyia uhalifu.

Jana, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja, alikaririwa akisema mapigano hayo yalifanyika katika msako wa majambazi walioiba silaha kwenye kituo cha polisi mkoani Tanga.

Aliyeuawa azikwa

Mwili wa askari wa JWTZ, Said Kajembe aliyefariki dunia katika Hospitali ya Bombo baada ya kujeruhiwa katika mapambano hayo uliagwa jana katika kikosi cha JWTZ Pande na baadaye kusafirishwa kwenda kijijini kwake, Kwashemshi, Korogwe kwa mazishi.

Wahalifu kulipiza kisasi

Kaimu DCI Diwani alisema uvamizi huo wakati mwingine husababishwa na wahalifu kutaka kulipiza kisasi kwa polisi hali ambayo alisema inatishia usalama wa nchi kwa ujumla. "Wapo watu wamewekeza kwenye uhalifu, sasa wanapoona polisi wamefanya kazi yao wanaamua kuwaharibia kwa kulipiza kisasi. Kwa kawaida, mhalifu hapendi polisi lakini hawa hawaangalii mbali kuwa vitendo vyao vinaweza kusababisha majanga zaidi ya haya," alisema.

Aliwataka Watanzania kuwa na sauti moja ili kukomesha vitendo vya uhalifu vinavyoendelea nchini ili kuirudisha Tanzania yenye amani.

"Tuwe na sauti moja, wimbo mmoja kama Watanzania, waandishi wa habari ni wadau wakubwa na viongozi wa dini pia watusaidie katika hili. Tunaapa kufanya kazi usiku na mchana kupambana na hili."

Uvamizi vituo vya polisi

Juni mwaka jana, majambazi wanaokisiwa kuwa sita, wakiwa na pikipiki tatu, walivamia Kituo Kidogo cha Polisi Mkamba kilichopo Kimanzichana, Wilaya ya Mkuranga, Pwani na kuua askari mmoja na kupora bunduki tano na risasi 60.

Polisi aliyeuawa ni Konstebo Joseph Ngonyani na majeruhi Venance Francis na Mariamu Mkamba ambao walipelekwa katika Hospitali ya Wilaya Mkuranga kwa matibabu.

Tukio la pili

Septemba mwaka jana, majambazi yalivamia Kituo Kikuu cha Polisi Ushirombo, Wilaya ya Bukombe mkoani Geita na kuua polisi wawili na kujeruhi wengine wawili na kupora bunduki 10 ambazo hata hivyo zilipatikana zote.

Walioawa ni G.2615 PC Dastan Kimati na WP 7106 PC Uria Mwandiga na waliojeruhiwa ni E.5831 CPL David na H627 PC Mohamed. Majambazi hao walivamia kituoni hapo kwa kurusha bomu la mkono.

Tukio la tatu


Januari 15, watu 15 wanaosadikiwa kuwa majambazi wakiwa na silaha za kivita na mabomu ya kurushwa kwa mkono walivamia Kituo cha Polisi Ikwiriri, Rufiji mkoani Pwani na kuua polisi wawili na kupora silaha tano za SMG na mbili za kufyatulia mabomu ya machozi zilizokuwapo kituo hapo na kutokomea kusikojulikana. Katika tukio hilo, polisi wawili Koplo Edga na WP Judith waliuawa.

Tukio la nne

Februari 3, Kituo cha Polisi cha Mngeta, Wilaya ya Kilombero kilivamiwa na majambazi ambao waliiba bunduki aina ya SMG yenye risasi 30.

Matukio mengine


Mbali na matukio ya uvamizi wa vituo vya polisi, kumekuwa na matukio mengine ya uhalifu mkubwa yanayoashiria kuwa hali nchini si shwari, likiwamo la Aprili mwaka jana la majambazi kuvamia Benki ya Barclays, Tawi la Kinondoni, Dar es Salaam na kupora kiasi kikubwa cha fedha.

Katika kipindi hichohicho, majambazi saba wakiwa na silaha waliivamia Benki ya I&M na kupora fedha zinazokadiriwa kuwa ni zaidi ya Sh150 milioni na kutoweka.

Novemba 2013, majambazi wanane walipora zaidi ya Sh900 milioni katika Tawi la Benki ya Habib, Kariakoo, Dar es Salaam. Sh700 milioni na Dola za Marekani 181,885 (Sh285, 444,000).

Mji wa Geita kutekwa kwa dakika 15


Itakumbukwa kuwa Juni mwaka jana, majambazi yaliuteka mji wa Geita kwa takribani dakika 15 na kupora fedha kwenye kampuni ya Blue Coast Inv. na kwa wakala wa usambazaji wa bia wilayani hapo. Kadhalika, majambazi hao walimuua kwa risasi, wakala wa huduma za fedha kwa njia ya simu.

Pia, kumekuwapo na matukio kadhaa ya utekaji mabasi. Januari 20, zaidi ya watu 40 waliteka mabasi sita ya abiria yanayofanya safari kati ya Jiji la Arusha na Nairobi, Kenya.

Viongozi wa dini

Katibu Mkuu wa Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, Sheikh Khamis Mataka aliwataka wananchi kutekeleza majukumu yao badala ya kuwaachia polisi.

"Vyombo vya kisheria na polisi havina watu wa kutosha. Wananchi wanatakiwa kuilinda amani iliyopo. Hili si jukumu la polisi peke yao. Kama tungekuwa na moyo wa kutoa taarifa ya mienendo ya shaka, ingekuwa rahisi kutatua matatizo kwa haraka. Ni muhimu kurudisha ari ya kushirikiana na vyombo vya usalama."

Mchungaji John Mbata wa Kanisa la Njia ya Yesu, Mbagala alisema hashangazwi na matukio hayo kwani ni dalili ya siku za mwisho... "zamani vituo vya polisi viliogopewa hata kwa kupita tu, leo ndivyo vinavamiwa, hii ni hatari."

Alisema hayo yote ni matokeo ya kumuacha Mungu, hivyo Taifa halina budi kuomba ili uchaguzi ujao uwe na amani.

Chanzo: Mwananchi
 
Hakuna hata picha ya tukio la mazishi?ili niamini tajeni hapa namba yake na picha nione.lkn ngoja niendelee kutafuta ukweli,maana moja ya msema kweli jeshini kuna kitu kinaitwa Part one order,kama imesoma basi nitakubali,lkn mpaka isome na chazo cha kifo.
Nitarudi baadae.
 
Aliyeuawa azikwa

Mwili wa askari wa JWTZ, Said Kajembe aliyefariki dunia katika Hospitali ya Bombo baada ya kujeruhiwa katika mapambano hayo uliagwa jana katika kikosi cha JWTZ Pande na baadaye kusafirishwa kwenda kijijini kwake, Kwashemshi, Korogwe kwa mazishi.

Source : Mwananchi

Ina aminika silaha zilizoibwa Polisi na kutumiwa na magaidi feki wa CCM pale Tanga zilijibadilisha kutoka silaha nyepesi kuwa nzito na kulazimu kuita Jeshi la Wananchi lije na silaha nzito!! ha ha ha ha !! CCM bwana~!
 
Aliyeuawa azikwa

Mwili wa askari wa JWTZ, Said Kajembe aliyefariki dunia katika Hospitali ya Bombo baada ya kujeruhiwa katika mapambano hayo uliagwa jana katika kikosi cha JWTZ Pande na baadaye kusafirishwa kwenda kijijini kwake, Kwashemshi, Korogwe kwa mazishi.

Source : Mwananchi

Nilivyooona huu uzi wako nikaja mbio nikiamini hatimae ninaweza kuona kaushahidi kadogo tu ili moyo wangu uanze kupungua shaka.. Lakini nimekutana na yale yale.. Habari zisizo na hata chembe cha ushahidi..

Bado ninasubiri ushahidi..
 
Mzee, u mzima wewe huko kichwani? Ni binadamu yule ujue. Acha lugha za dharau kwenye uhai wa wenzio. Usipojali wewe wapo wengi wanaomjali. HAkuuwawa kwa kushikwa ugoni, ni katika kukulinda wewe fyatu. Mungu atakulipa kwa ukilaza wako.

Mimi Silindwi Na Wanajeshi Wenu Bali Nalindwa Na Malaika Wa Mwenyezi Mungu Na Najilinda Mwenyewe Pia Sawa? Mbwiga Mkubwa Weye! Wao Ni Nani Wasife? Tena Nawalaumu Mno Hao Sijui Majangili au Magaidi Kwa Kuua Tu Huyo Mmoja Kwani Mimi Nilitaka Wawaue Wote Ili Wakome. Battle Ndogo Tu Hiyo Tunahanya hanya Na Kuhangaika Je Zingine Zitakuwaje? Mr. Misifa Wenu Mwakibolwa Mbona Hajaenda Sasa Huko Amboni Tanga? Mnadhani Magaidi Ni Sawa Na M23? Hivi Kama Wewe Una Akili Na Unajifanya Unayajua Masuala Ya Medani Za Kivita Ambaoni Tanga Ni Kwa Kuwapeleka Wanajeshi? Kulikuwa Na Ugumu Gani? Ndiyo Maana Na Wao WAMETUSAMBAZIA UPENDO Kwa Ku Mdedisha Huyo Mjeda Kwani Na Wao Walikurupuka Na Wakome Siku Nyingine.
 
Nilivyooona huu uzi wako nikaja mbio nikiamini hatimae ninaweza kuona kaushahidi kadogo tu ili moyo wangu uanze kupungua shaka.. Lakini nimekutana na yale yale.. Habari zisizo na hata chembe cha ushahidi..

Bado ninasubiri ushahidi..

Mkuu kuna chembe fulani ya Ukweli katika hoja yako. Lakini tuvute Subra.....japo nimejaribu kumsearch Said Kajembe wamekuja wakenya wengiii ngoja niendelee
 
Mzee, u mzima wewe huko kichwani? Ni binadamu yule ujue. Acha lugha za dharau kwenye uhai wa wenzio. Usipojali wewe wapo wengi wanaomjali. HAkuuwawa kwa kushikwa ugoni, ni katika kukulinda wewe fyatu. Mungu atakulipa kwa ukilaza wako.

Na Kwa Taarifa Yako Tu Na Kwa Kukusaidia Hilo Tukio Zima La Tanga Ni Framing Tu Ya Situation Imefanyika Ili Kuwapumbaza Watu, Kufunika Masuala Fulani Fulani Ambayo Ni Nyeti Lakini Haswa Kuwafanyeni Muamishe Akili Zenu Ktk Kukazania Sijui Masuala Ya Katiba Pendekezwa Na Maudhui Yake Ili Muda Uende Na Siku Ifike Wafanye Yao. Akili Yangu Siyo Kama Yako Ya Ki BRN Hata Kufikiri Hujui Na Unakurupuka Tu. Siandiki Humu Jambo Kama Sijalichuja Na Kulitathmini Na Unavyo au Mnavyonichukulia Wala Sivyo Na Ipo Siku Mtanikubali Tu Na Kuficha Nyuso Zenu. Huna Ulijualo Na Acha Huruma Za KINAFIKI!
 
Aliyeuawa azikwa

Mwili wa askari wa JWTZ, Said Kajembe aliyefariki dunia katika Hospitali ya Bombo baada ya kujeruhiwa katika mapambano hayo uliagwa jana katika kikosi cha JWTZ Pande na baadaye kusafirishwa kwenda kijijini kwake, Kwashemshi, Korogwe kwa mazishi.

Source : Mwananchi

Kuna mwenye Picha yake tujue anafananaje? Ngoja tusubiri jioni kwenye Taarifa za Habari!!
 
We na magaidi wenzenu siku zenu zinahesabika.

Pamoja Na Kwenda Na Makombora Yenu Ya Msaada Kutoka China Na Marekani, Magari Sijui VX Na Misafara Ya Askari Wa Kila Aina Kuna Jangili Hata Mmoja Wamemkamata? Ninavyowadharau Hawa Watu Usifikiri Kuwa Nakosea Bali Namaanisha Kuwa Uimara Wa Vikosi Vyetu Vya Ulinzi Na Usalama Kwa Sasa Nchini Tanzania Unatia Mashaka Na Kuna Upuuzi Na Uzembe Mkubwa Unaofanyika Humo ILA Nyie Kwakuwa Mmekuzwa Ki BRN Hamwezi Kutambua Kitu. Ingekuwa Ni Nchi Zenye Ueledi Na Nidhamu Ya Kazi Kwa Tukio Hili Tu Mkuu Wa TISS Na Hata Wa Jeshi La Polisi Wangewajibika Kwa Uzembe Ambao Kama Idara Zao Zingekuwa Makini Yaliyotokea Amboni Kamwe Yasingejiri Na Bado Wanapeta Tu Huku Watanzania Wakitaabika Huko Tanga.
 
sinema kama ya balali. Hakuna mwili, hakuna kaburi lakini amekufa na kuzikwa. Only in Tz
Jamani tunazidi kuleta maelezo mepesi katika hoja nzito. Kumbuka hili tukio lilisimamisha nchi kwa masaa 48, ngoja tusubiri wadau watuwekee picha za msibani.
R.I.P Kajembe kwa kuipigania na kuifia nchi yako

 
Mbona hizi taarifa sijasikia kutoka kwa Msemaji wa JWTZ? Kuna amtu anajua Email au Namba ya Simu ya Msemaji (Meja Erick Komba)? Naomba ani PM pls!
 
Na Kwa Taarifa Yako Tu Na Kwa Kukusaidia Hilo Tukio Zima La Tanga Ni Framing Tu Ya Situation Imefanyika Ili Kuwapumbaza Watu, Kufunika Masuala Fulani Fulani Ambayo Ni Nyeti Lakini Haswa Kuwafanyeni Muamishe Akili Zenu Ktk Kukazania Sijui Masuala Ya Katiba Pendekezwa Na Maudhui Yake Ili Muda Uende Na Siku Ifike Wafanye Yao. Akili Yangu Siyo Kama Yako Ya Ki BRN Hata Kufikiri Hujui Na Unakurupuka Tu. Siandiki Humu Jambo Kama Sijalichuja Na Kulitathmini Na Unavyo au Mnavyonichukulia Wala Sivyo Na Ipo Siku Mtanikubali Tu Na Kuficha Nyuso Zenu. Huna Ulijualo Na Acha Huruma Za KINAFIKI!
Thatz true boy hiyo ni epsod mpya kati ya tamthilia inayoendelea..Watanzania amkeni kumekucha
 
Drama zinaendelea, wanajeshi wetu waliofia DRC walizikwa kwa heshima zote za kitaifa tulionyeshwa picha zao na majeneza yalifunikwa kwa bendera za taifa, inakuwaje askari aliyefia nchini anazikwa kimya kimya?
 
Back
Top Bottom