Askari wa JWTZ aliyefariki Tanga Azikwa

Jamani tunazidi kuleta maelezo mepesi katika hoja nzito. Kumbuka hili tukio lilisimamisha nchi kwa masaa 48, ngoja tusubiri wadau watuwekee picha za msibani.
R.I.P Kajembe kwa kuipigania na kuifia nchi yako

unachekesha kwelikweli jamaa. yaani hizi drama za ccm zilisimamisha nchi! mimi hata sina habari na huu upuuzi wao.
achaneni na huo unaoitwa ugaidi. marekani na urusi pamoja na maguvu yao yote hapatoshi itakuwa tanzania. kafanye kazi ulishe watoto achana na upuuzi huu wa ccm.
 
Hizi ni sinema za ccm hata Jk hajaenda kumzika au kutoa salamu za rambi rambi kwa wafiwa amezikwa kimya kimya kama mgonjwa wa Ebola
 
Akili yako haikutoshi,suala la ulinzi si wa kova au kikwete ulinzi ni wa kila mtu,watu wanavamia US na kufanya uharifu sembuse tanga,sio kila jambo la kulaumu tuu ili mladi umelaumu na unalaum kwa sababu serikali ni ya ccm,foolish

Foolish Mama Yako.
 
Habari wakuu?

Nimesikia magazetini hasa majira, wanaelezea usiri mkubwa ulifanyija jana kumuaga mwanaukombozi huyu hapo Tanga, ili kupelekwa kwao kijiji kwa maziko.

Naomba kuuliza waliofika au waliopo kijijini kwao watujuze maziko yalikuwaje...

Pia naomba, mwenye picha au majina ya majeruhi pls atuweke hapa tuwajue na kuwasaidia ndugu zetu.

Asante sanaaa.
 
Na Kwa Taarifa Yako Tu Na Kwa Kukusaidia Hilo Tukio Zima La Tanga Ni Framing Tu Ya Situation Imefanyika Ili Kuwapumbaza Watu, Kufunika Masuala Fulani Fulani Ambayo Ni Nyeti Lakini Haswa Kuwafanyeni Muamishe Akili Zenu Ktk Kukazania Sijui Masuala Ya Katiba Pendekezwa Na Maudhui Yake Ili Muda Uende Na Siku Ifike Wafanye Yao. Akili Yangu Siyo Kama Yako Ya Ki BRN Hata Kufikiri Hujui Na Unakurupuka Tu. Siandiki Humu Jambo Kama Sijalichuja Na Kulitathmini Na Unavyo au Mnavyonichukulia Wala Sivyo Na Ipo Siku Mtanikubali Tu Na Kuficha Nyuso Zenu. Huna Ulijualo Na Acha Huruma Za KINAFIKI!
Mwenda wazimu siku zote anajitangaza kwamba ana akili sana, sijaona tofauti ya mwenda wazimu na wewe kwa kujisifia mwenyewe. Muungwana anaangalia mambo kwa nafasi nyingine na wala hajiangalii kwa kujipalilia au kujifagilia. Ulianza vizuri kujadili lakini ulipoanza kuponda mawazo ya wengine kwa dharau nikaanza kupoteza hamu ya kukutafakari kama mkomavu kwenye kujenga hoja. ni kwa sababu ya utoto wako kifikra, ukikua utajifunza namna ya kujadili hoja bila dharau lakini ukafikisha ujumbe kwa walengwa wako.
 
Hizo ni sinema za ccm kwani wamemzika kwa siri kama mgonjwa wa Ebola hata raisi hajaenda au kutuma salamu za rambi rambi inashangaza sana ccm mbinu zenu chafu zimeshajulikana andae lingine tena Amboni ni usanii tuu.
 
Habari wakuu?

Nimesikia magazetini hasa majira, wanaelezea usiri mkubwa ulifanyija jana kumuaga mwanaukombozi huyu hapo Tanga, ili kupelekwa kwao kijiji kwa maziko.

Naomba kuuliza waliofika au waliopo kijijini kwao watujuze maziko yalikuwaje...

Asante sanaaa.

sasa hapo usiri uko wapi kwani ulienda ukazuiliwa kushiriki mazishi.
 
Hizo ni sinema za ccm kwani wamemzika kwa siri kama mgonjwa wa Ebola hata raisi hajaenda au kutuma salamu za rambi rambi inashangaza sana ccm mbinu zenu chafu zimeshajulikana andae lingine tena Amboni ni usanii tuu.

bawacha viumbe wa ajabu sana sijui hata huko nyumbani mnaishi vipi na familia zenu hasa waume.
 
Usiri tena au msiba huu ni sawa na wa Balali kwenda kwa kadi? Kwa nini iwe siri wakati askari walikufa huko sudan walituonyesha live kuanzia mapokezi kuaga mpaka mazishi, na askari waliokufa DRC pia, sasa huyu wa hapa kwetu kwa nini iwe siri?!! mashaka makubwa haya !! Hata hivyo nilishangaa habari hii kutopewa coverage yoyote huku habari za chief mkwawa na kigwangara zikipewa uzito mkubwa , kwa nini? Serikali toeni ufafanuzi la sivyo watu wataamini mambo ya mitandaoni.
 
katika muvi ambayo chago chago ameshindwa kuimalizia ni hii, bora bwana kanda maalum anatoa na picha za watu feki, ni kiongozi gani aliyeudhuria huo msiba? mbona kwenye misiba ya wasanii wanajazana ila ya huyu shujaa aliyekuwa anatetea wananchi na magaidi hata mtendaji wa kata sidhani kama alienda.
 
Back
Top Bottom