Askari wa JWTZ aliyefariki Tanga Azikwa

MASWALI YA MSINGI KWA HILI TUKIO LA TANGA

Kwanza nitoe Pole kwa Familia ya marehemu askari (R.I.P Said Kajembe) kama ni kweli.

(1) Nakubaliana na mambo ya usalama kutooneshwa picha za tukio likiwa linaendelea ili kuwalinda walio kwenye operation hiyo, sasa je, ni ugumu gani kutoa taarifa sahihi na picha za majeruhi na huyo askari aliyefariki?

(2) Je, vyombo vya ulinzi havioni ni shida kwa wananchi kuwa na sintofahamu ya ukweli kwa kutoweka taarifa sahihi? Je, ukimya wao hawaoni kama ni kweli watu wanavyooneza kuwa hiyo ni movie itawaingia wananchi na kuwachukia vyombo vya usalama?

(3) Aliyekufa ni shujaa akipigania nchi, je, haikufaa kuenziwa na kudhaminiwa mchango wake katika mazishi yake? Mfano; tujikumbushe yule Askari Shujaa wa Dodoma (R.I.P Soja) aliyekuwa anamuokoa mtoto mchanga asiuawe, taarifa sahihi na kwa wakati zilitoka na kila mtu alimuona ni shujaa wa kweli.

(4) Je, ikibainika si kweli vyombo vya usalama vitaficha wapi sura na je, vitaaminika tena na jamii?

(5) Je, wapi TISS, nini majukumu yao? Kweli hawajui kinachoendelea? Mbona zamani walikuwa fit hata kuaminishwa kuwa kwa afrika TZ wana-mashushushu wa ukweli na uhakika?

Ningependa mwenye kuyajua hayo yanayonitatiza akanisaidia kunielewesha
 
Haya Mimi bado nasubiri part two ya hii sinema,yaani askari anakufa akiwa on line of duty alafu mnamzika kimya kimya!!!?
Let's wait and see Kama vyombo vya habari vilikuepo mazishini,Kama sio kweli then wakuu wa vyombo vya usalama kuanzia COD hadi karagosi wa mwisho walio plan this bloody shit wote wajiuzulu haraka iwezekanavyo.
They cant play with our brains kirahisi hivi nasisi tukawaitikia eti,Bwana ametoa Bwana ametwaa .noneses
 
yani mijitu ya humu kila kitu utasikia PICHA TAFADHALI naamini hata ukiambiwa mkeo ANALIWA GEST utasema hivo hivo PICHA TAFADHALI

Acheni udanganyifu na hizo movie zenu. Zikeni migomba na msichukulie watu ni wajinga kiasi hicho.
"you can fool the people but you can't fool all the people all the Time"
 
Its true Balali party two.
kama kuna ndugu au rafiki yeyote mwenye picha ya kajembe aiweke mtandaoni watu tumwone..amezaliwa lini? wapi? ndg,rafiki yake wa karibu ni nani? TZ KWA COMED KWENYE MAMBO YA MSINGI HATUJAMBO
 
Jamani tunazidi kuleta maelezo mepesi katika hoja nzito. Kumbuka hili tukio lilisimamisha nchi kwa masaa 48, ngoja tusubiri wadau watuwekee picha za msibani.
R.I.P Kajembe kwa kuipigania na kuifia nchi yako



Acha uongo, sie mjin kwetu tulikuwa tunaendelea na movement za hapa na pale kama ilivyo ada, za kutafuta mkate wa kinywa.Mpaka sasa wengne hawaelew kama kuna tukio kama hili ndan ya tz; na kaz inaendelea kuchapwa kama kawa kama dawa.
 
wakugalagaza wenzao kwenye matope, kila nguo yao,kosa dogo adhabu kubwa,wazee wa nauli bure wazee wenye haraka barabarani kuliko wenzao wote,kuwa wajeshi wamejiona kama wamekuwa miungu ya duniani muda wa kuonesha kwnn walikuwa wanalipwa mishahara isiyojadiliwa bungeni na kutaka utukufu duniani ndo huu musituambie habari za wananchi kutoa ushirikiano kwani wakati unakula mshahara wako wa mara 2 kwa mwezi ulikuwa tunagawana
 
Kwanza nilivyomuna tu Changonja nikajua hapa movie. Kuna watu wawili nikiwaona tu hao kwenye issue yoyote najua akina Kanumba cha mtoto hao ni Chagonja na mwenziwe Kova mtoto wa Dar, hao wazee wa karata 3. Wazee waongo hao hata macho hawapepesi. Huwa wanachomekewa huko kusiko na jina bali wenyewe huwa wanaita ngazi za juu. Wanakujaga na hekaya za kizamani sana bila kujua huko wanakolala ndio sisi tumeamkia. Bado wanaishi dunia ya gazezi la mzalendo na vichekesho vya kina chakubanga, bila kujua siku hizi dunia ni digital. Wanaongea mambo mpaka unajiuliza hawa wazee wako sawa kweli. Ukikutana na vijana wao wa jeshi la polisi mpaka wanapata hasira jinsi wazee wanavyowapeleka kizamani. Ila ndio hivyo huko jeshini wanasema hakuna kuhoji ni kutekeleza kwanza longolongo baadae. Wenyewe wanajua mambo mawili tu nchi hii chadema na magaidi mwisho wa habari. Haya mambo mengine sijui mbinu za kisasa unawachanganya maana hata kugoogle kwenye internet kwao ni janga.

Kwa hiyo usishangae ukiona wanaleta mambo ya namna hiyo, ila ni sisi wenyewe ndio tumeruhusu viongozi wasanii wakakaa madarakani hivyo hawataki weledi bali mazoea ili wapige deal, na huwa wanaamini sisi waafrika hatujui kitu bali wazungu. Ngoja wamuone mzungu hata kama hajui kusoma na kuandika nakwambia kwenye kiti watampisha. Na wazungu si unajua wanatujua kwamba tunawatetemekea wanapiga deal wanavyopenda nchi hii. Ole wako sasa umguse mzungu akipiga simu tu wanamuuliza nani anakusumbua, akikohoa tu utaona PT zimeshehena maaskari tayari kwa kipigo.

Acha basiiiiii! Ha ha ha ha ha ha ................haaaaa aaaah!
Yaani mwanangu we ukishika maiki 'MWALIMU' chamtoto, ila tu LONGOLONGO na ushabiki wa vyama umezidi kidogo!
 
Drama zinaendelea, wanajeshi wetu waliofia DRC walizikwa kwa heshima zote za kitaifa tulionyeshwa picha zao na majeneza yalifunikwa kwa bendera za taifa, inakuwaje askari aliyefia nchini anazikwa kimya kimya?

Feedback;
Jua kitu moja tu. Uongo wa kutunga una matobo ka ya pakacha. Halisitiri maji. Hakuna mahali ambapo JWTZ wange jionesha ka hapa. Kutuaminisha kuwa, kama ni magaidi au panya road wajue jeshi liko tayari.
Askari wetu 1 tu kufia kwenye uanja wa vita, ni sikitiko kwa kila Mtanzania. Iweje leo mmzike shujaa wetu, aliyekuwa anapigania Taifa lake kama alifumaniwa?
Tungeni muvi zenye mshiko. Mnalichafua hata jeshi, jamani mnataka kutupeleka wapi?? Hao wanajeshi mnawafanya si Watanzania?? Hawajafika kiwango cha chini hivyo kuwa akifia kwenye uanja wa mapambano basi mnamsahau haraka hivyo.
Hakuna jinsi ambavyo Serekali hii ya ccm itaacha kulaumiwa endapo machafuko yatatoke nchini. Msibuni mambo ya hatari namna hiyo. Ongezeni ujanja kwenye hizo mashine za kuandikisha wapiga kura lakini msiliingize tena jeshi tafadhali. Mmeshawapata polisi hao, mmeshawapata majaji hao mpaka Jaji mkuu mstaafu kumbe alikuwa ccm. Sasa mnatuambia naye Mh. Mamunyange ni ccm??? Kwa nini mlilete jeshi kwenye sinema hii?
Ondokeni kwa amani Magogoni jamani. Waje tena wengine nao waje kula hayo makombo kama mmebakiza. Nawaza tuuu kupu.uziiii nisamehewe. Sitaki makomenti yaso na kichwa kutoka maccm hapa. Tumefunguka macho
 
-- Tukumbushane, kama mnakumbuka miaka ile ya mwanzo ya utawala wa JK yalikuwepo mambo kama haya kuibiwa kwa mabank, ile sinema ya pale Ubungo mataa kuibiwa kwa hela za benk zilizokua zinapelekwa NMB Wami Moro.
-- Kile kikosi cha Wajaluo wa Sarungi kule kule Shirati, na mengine mengi. Naamini magogoni wana episode zote za movie hii.
-- Ukiona hivi juo ndo Mkwere anaondoka Ikulu, anatoka kama alivyoingia
 
mkuu wa mkoa wa tanga ataongea ksho na waandishi wa habar labda tutajua hii movie inaendaje
 
....mimi ainiingii akilini; pamoja na Askari wetu kuuawa na Baadhi kujeruiwa lakini pia na ushirikiano wote huo unaotajwa wa Jeshi la Polisi na JWTZ bado tu hao ,majambazi/magaidi yameshindwa kunaswa ama kujeruiwa!!!!!!!!

Nina pata wasiwasi na Uwezo wa Majeshi yetu.
 
mkuu wa mkoa wa tanga ataongea ksho na waandishi wa habar labda tutajua hii movie inaendaje
Ameshaongea kasema watu waendelee na kazi zao kama kawaida kwa vile wameshadhibiti eneo la tukio, cha ajabu hakuzungumzia lolote kuhusu mazishi ya askari aliyefia kwenye mapambano hayo.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom