Askari wa jeshi la polisi wanaruhusiwa kuvaa hivi?

Askari wa jeshi la polisi wanaruhusiwa kuvaa hivi?

b191

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
742
Reaction score
1,032
Nawasalimu wote,

Tangu nikiwa mdogo niliamini kuwa Askari yeyote hasa wa hapa Tanzania ambao nilikuwa nikiwaona hawaruhusiwi kufanya vitu hivi;

1. Kuvaa (modal) suruali au shati lililobana akiwa kwenye sare za kazi

2. Kusuka nywele kwa WP

3. Kuweka nywele dawa

4. Kuvaa nguo fupi kwa WP

5. Kufuga ndevu

Kwa miaka ya hivi karibuni nimekuwa nikiwaona baadhi ya Askari wakifanya vitu hivi. Sasa nimekuwa nikijiuliza;
JE WANARUHUSIWA KUFANYA VITU HIVYO?

Nawasilisha..
 
Wasubiri wanamalizia mazoezi ya kupambana na UKUTA tarehe 1 watakuja kukujibu.
 
Jeshi siku hizi nalo limeanza kukumbatia mambo ya kidotCOM.

Siku hizi kuna baadi ya askari wanavaa mpaka milegezo, yaani ni aibu sana aiseeee.
 
1. Ukishakuwa kwenye sare za kazi hiyo "modo" unavaaje sasa!!! Ukishakibidhiwa sare za kazi labda itokee zikubane tu lakini siyo uzifanye ziwe modo

2. Kusuka ni utaratibu kwa wanawake / na kuweka nywele dawa (siyo zile zinazobadilisha rangi ya nywele )

4. Ufupi wa nguo ni kipimo ,so inategemea tu ila isiwe imevuka magoti (uniform )

5. Ndevu ni uchafu katika kanuni za jeshi. Ila yapo mazingira (MF: Askari anaumwa ,anakuwa off duty let's say miezi kadhaa, huyu anaweza kufuga ndevu).
 
Hawana kazi za kufanya, vita hamna waasi Hamna vurugu hamna
Wanakula ela tu, wanaota na vitambi nyumba bure usafiri bure chakula bure,
 
Ujue ifikie hatua muli heshimu jeshi letu jifunzeni kwenye mataifa mengine jeshi halitaniwi taniwi hovyo kwenye mitandao hivi una taka kujua nini kuhusu jeshi nenda makao makuu watakwambia kama kufuga ndevu ni sawa au sio sawa jifunzeni kuheshimu vyombo vyetu vya usalama musipende kuvichunguza na kuvishambulia kwenye mitandao over
 
Dah...ngoja Sept 1 tutawaona kwa karibu [emoji12]
 
Kufuga ndevu kwa askari wa CID ruksa, wapo wanovaa heleni kwa wanaum, kufuga rasta, hao ndio undercover policee ukifika pale msimbazi police ukiwaona huwezi amini kama ni askari, lakini kwa kufanya hivyo inawawezesha sana kukabiliana na uhalifu, mazingira ya kazi yamebadilika sana
 
Hawana kazi za kufanya, vita hamna waasi Hamna vurugu hamna
Wanakula ela tu, wanaota na vitambi nyumba bure usafiri bure chakula bure,
Tumia uhuru wako wa maoni vizuri. Jeshi ni zaidi ya vita na waasi, siasa zenu pelekeni huko.
 
Ujue ifikie hatua muli heshimu jeshi letu jifunzeni kwenye mataifa mengine jeshi halitaniwi taniwi hovyo kwenye mitandao hivi una taka kujua nini kuhusu jeshi nenda makao makuu watakwambia kama kufuga ndevu ni sawa au sio sawa jifunzeni kuheshimu vyombo vyetu vya usalama musipende kuvichunguza na kuvishambulia kwenye mitandao over
[emoji15] Real?
 
Mkuu mbona hivyo?Jeshi ni letu watanzania na kila mtanzania anayo haki ya kuhoji miendendo isiyofaa ndani ya jeshi pale anapoiona na hilo ni jambo jema.
Mleta mada kauliza vizuri hajalivunjia heshima jeshi letu ni kumjibu kwa hekima tu kwa kuwa majeshi yetu sio untouchable ni ndg zetu wanapokengeuka lazima warekebishwe kistaarabu.
 
Mbona mimi nawaona smart sijawaona na ndevu .we jali kasheshe zao wanapomfuma jambazi achana na ndevu.
 
Kuna vingi vya kuzungumzia kwa hapa ni majungu tu.......
 
Ujue ifikie hatua muli heshimu jeshi letu jifunzeni kwenye mataifa mengine jeshi halitaniwi taniwi hovyo kwenye mitandao hivi una taka kujua nini kuhusu jeshi nenda makao makuu watakwambia kama kufuga ndevu ni sawa au sio sawa jifunzeni kuheshimu vyombo vyetu vya usalama musipende kuvichunguza na kuvishambulia kwenye mitandao over
Hapana usiwe mnafiki hakuna sheria inayo zuia kujadili mwenendo wa jeshi hasa katika swala la maadili na usilifanye jeshi kuwa exceptional kiasi hicho kwa sababu wao sio mungu hata majesh ya nchi za nje yanajadiliwa vyema kwenye mitandao huenda wewe hufuatilii forum za wenzetu unatumia wazo la mazoea.
Na kwakuongeza tu kulijadili jeshi haina maana kwamba haliheshimiwi mbona katika mema huwa hamleti maneno kama haya?
 
Back
Top Bottom