Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,325
- 11,193
Katika hali ya kuzimwa data na umeme Gaza kuna mengi tunayokosa kuyaona.Hata hivyo machache yanayovuja kwa shida inaonesha vita huko ni kali kuliko ule ukali uliotarajiwa na jeshi la IDF.
Mara kadhaa jeshi hilo limeshatangaza kuingia katikati ya Gaza lakini baadae ikaonesha kuwa bado wako pembeni kabisa wakitumia makombora ya kutoka kwenye ndege zao za kisasa.
Katika moja ya vidio zilizotolewa kwa shida na wapiganaji wa Hamas imeonesha kifaru cha Israel kikiripuka baada ya kupigwa na silaha hafifu.
Baada ya hapo mmoja wa waendeshaji kifaru hicho akachomoka kwa nyuma huku akivua magwanda yake na kukimbia akiwaacha waenzake waungue ndani ya kifaru hicho.
Pembeni ya kifaru hicho vipo vyengine kadhaa vilivyotelekezwa baada ya ama kuharibiwa au askari wake kuamua kuviacha tu na kukimbia.