Askari wa Bunge wapangiwa vituo vingine vya kazi kwa kusuasua kumnyakua Mnyika

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Askari walioagizwa kumtoa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika bungeni Ijumaa iliyopita, wamepangiwa vituo vingine vya kazi kwa kuchelewa kutekeleza agizo la Spika.

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema aliwashangaa askari hao kwa jinsi walivyokuwa wanambeleza mbunge huyo wa Kibamba kutoka nje.

"Askari hawa wataendelea kuhamishwa mpaka pale tutakapowapata wanaogaa," amesema Ndugai.

Mnyika alitolewa bungeni Ijumaa iliyopita baada ya mmoja wa wabunge kusema ‘Mnyika mwizi’ akimhusisha na wizi wa madini.

Kutokana na hali hiyo Mnyika alimtaka Spika kuchukua hatua dhidi ya mbunge aliyesema kuwa yeye ni mwizi lakini Spika alisema hajui hilo na haijaingia kwenye hansadi.

Hata hivyo Mnyika alisisitiza kuwa mambo hayawezi kwenda hivyo.

Baada ya majibizano kati yao Spika aliamuru walinzi wamtoe Mnyika nje ya Bunge

Chanzo: Mwananchi
 
Akumbuke kwamba hata yeye hatadumu kwenye uspika milele. Bora atekeleze majukumu yake kwa haki.

Kuna wakati anafanya maamuzi vizuri kabisa, nashindwa kuelewa huu ubaguzi, jazba na kiburi huwa vinatoka wapi?
 
Askari walioagizwa kumtoa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika bungeni Ijumaa iliyopita, wamepangiwa vituo vingine vya kazi kwa kuchelewa kutekeleza agizo la Spika.

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema aliwashangaa askari hao kwa jinsi walivyokuwa wanambeleza mbunge huyo wa Kibamba kutoka nje.

"Askari hawa wataendelea kuhamishwa mpaka pale tutakapowapata wanaogaa," amesema Ndugai.

Mnyika alitolewa bungeni Ijumaa iliyopita baada ya mmoja wa wabunge kusema ‘Mnyika mwizi’ akimhusisha na wizi wa madini.

Kutokana na hali hiyo Mnyika alimtaka Spika kuchukua hatua dhidi ya mbunge aliyesema kuwa yeye ni mwizi lakini Spika alisema hajui hilo na haijaingia kwenye hansadi.

Hata hivyo Mnyika alisisitiza kuwa mambo hayawezi kwenda hivyo.

Baada ya majibizano kati yao Spika aliamuru walinzi wamtoe Mnyika nje ya Bunge

Chanzo: Mwananchi
Askari hawa wataendelea kuhamishwa mpaka pale tutakapowapata wanaogaa," amesema Ndugai.
Jini la Ndugai linataka damu bungeni. Alipokuwa mgonjwa, alitutia sana huruma tukafunga na kusali kumwombea, naona sasa afya imeimarika anatamani, kufanya yale aliyomfanyia yule mgombea mwenzake kule Mpwapwa. Hebu wekeni picha wale mlionazo tujikumbushe.
 
Lazima hawa waliotusaliti na kuanza kutetea mafisadi wa madini wakomeshwe

Unasahau kuwa wewe pamoja na mafisadi wenzako ndio mliotufikisha hapa kwa kupitisha mikataba kwa hati za dharura.

Wakati huo wakina mnyika walikua wanawaonya bado mlitumia mbinu hii hii ya kuwatoa nje. Sasa mnaleta ujinga wenu mnaonywa bado mnatumia mbinu ileile ya kuwatoa nje ili mkihalibikiwa mpate sehemu kulilia.

Aibu yenu imewakamata wazee wa ndiooooo
 
Now the end is near so near. Magufuli chunga sana narudia chunga sana. Watu wanahasira mioyoni kamwe usijaribu kuziamsha hakika ziliamka Tanzania haitakuwa salama
 
Sijui lakini nawaza mfano Mh. Ndugai wewe ukifanyiwa hivi utafurahi? Wakristo sisi ujue....Jiulize mara ngapi umekosea hadharani au sirini hukuhukumiwa japo ulistahili huku pengine kali kuliko hiyo unayowapa vijana wenzio?

Badilika hao polisi hawakukosea kumbembeleza Mh. Mnyika ni kama vile ungefanyiwa wewe iwapo umeingia katika mazingira yale. Pia Polisi sio kupiga tu au kudhalilisha tu acheni pia watumie busara hasa kwenu ninyi waheshimiwa maana tumewachagua na tunawaheshimu sana ukipigwa mbele yangu sitafurahi kabisa hata kama umekosa.

Pia maamuzi yako yaongozwe na afya ya bunge katika kusimamia serikali maana hao unaowatoa nje wanamichango yakuokoa taifa hili pia jaribu kiti chako kiwe na falsafa ya utaifa kuliko kumpendeza mtu au chama chako huo ndio uongozi.
 
Ndiyo maana kazi ya uaskari siipendi kabisa, kuna amri za kijinga kabisa na huna uwezo wa kuzikataa bila kuhatarisha kibarua chako. Hata hivyo Ndugai atambue kuwa siku zake za kuwa spika zinahesabika. Spika wa JPM ni Tulia Ackson. Maandalizi ya kukwaa jimbo yamekamilika kwa asilimia 100. Sasa yeye aendelee na ubabe wake bila kujua una mwisho.
 
Ilitakiwa waswekwe ndani kwanza kwenye magereza ya kijeshi na adhabu kali ili iwe fundisho kwa askari wengine watakaobadili kwao.
 
Back
Top Bottom