Askari wa barabarani akabana koo na bodaboda

Askari wa barabarani akabana koo na bodaboda

Pharm D

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2017
Posts
1,238
Reaction score
3,020


Hawa jamaa wamezid mno kuonea watumiaji wa vyombo vya moto...
Tunajua mko kulinda usalama wa maisha yetu lkn pale mnapovuka mipaka na kugeuka kero ndio hapo tunashindwa kuwaelewa.

Hili jambo la jamaa kujivunia kukusanya mapato kupitia makosa ya barabaran its like mnafurahia watu kukosea ili muweze kufikia malengo ya makusanyo yenu na kule kuongeza tozo za fain ni kichocheo kikuu cha rushwa za barabaran mwenye nchi amezihalalisha kuziita ruzuku ya kufutia viatu.

Acha mpigwe tu maana hamna namna sasa
 
hawa jamaa wamezid mno kuonea watumiaji wa vyombo vya moto...
Tunajua mko kulinda usalama wa maisha yetu lkn pale mnapovuka mipaka na kugeuka kero ndio hapo tunashindwa kuwaelewa...
.
Hili jambo la jamaa kujivunia kukusanya mapato kupitia makosa ya barabaran its like mnafurahia watu kukosea ili muweze kufikia malengo ya makusanyo yenu na kule kuongeza tozo za fain ni kichocheo kikuu cha rushwa za barabaran mwenye nchi amezihalalisha kuziita ruzuku ya kufutia viatu...
.
Acha mpigwe tu maana hamna namna sasa

Wapigwe tu maana hamna namna in Pinda voice.
 
hawa jamaa wamezidi wallah kama mkuu hatoliangalia hili tutafika sehemu mbaya wamezidi uwonevu ,inamana wao wako juu ya sheria ?
Ni nani wa kuwasimamia hawa Askar kuhakikisha wanatenda haki
 
Huyo traffic ni kama ana hasira na maisha yake.. hii kitu haitakiwi kutendwa kihivyo kabisa. Kingine haionyeshi makosa na hakuna ngumi zaidi ya kukabana mashati na dereva. Inatia aibu traffic kutenda hilo hata baada ya mwemzake na raia kumsihi akaendelea tu. Hata kama dereva ana kosa.. inabidi watafute mbinu za kuwabana hao madereva wasiotii sheria za barabarani ikiwa wanaogopa kukimbiwa nao
 
Tena siku hizi traffic ni wengi barabarani katika kituo kimoja waweza kuta hadi 10 sijui huko ofisini huwaacha wengine au ni ugumu wa kazi barabarani
 
Ugomvi mwingine ni wa kijinga! Kujifanya jasiri,.

Sasa huyo trafic angekuwa na bastola hajakutoa utumbo tu hapo?

......
 
Kunasiku nilikutana na bodaboda mmoja ,anasema kunamwenzao alishikwa na trafic akamtishatisha kisha kamuandikia akalipe elf60.bodaboda akamwambia nalipa lakini utailrudisha hiyo.

Jamaa akatafuta wenzie wachache wameenda hadi nyumbani kwa traffic wakagonga mlango ,ile anatoka wakamuweka chini wamwambia alipe hela yao aliewalipisha mchana,traffic hakua na namna kaingia ndani katoa hela na ya usumbufu ,bodaboda wakaondoka.

UKWELI KUNA MAKOSA MENGINE UNEWEZA KUMKUMBUSHA TU DEREVA NA KUACHANA NAE,

TATIZO WANA DILIAZAIDI NA BODABODA ,BAJAJI, DARADARA ,NA VILUKUU,

HUKU NI KUWAPANDIKUZA WATU HASIRA,MAANA UNAKUTA MTU CHOMBO SIO CHAKE NA ANATAFUTA RIZIKI YA WATOTO. IKIFIKA JIONI ANAJIPA MOYO NIMEPATS HESABU YA MWENYE CHOMBO NA RIZKI YAKE YA FAMILIA WEWE UNAKUJA BILA YA HULUMA TENA KWA KOSA LA MTU KUKUMBUSHWA TU.

ASKARI ANATAKIWA AJUE DHAMANA ALIYOPEWA SERKALI NA NGUO ALIZOPEWA AVAE ,ISIWE KIGEZO CHA KUJIONA KUWA UKO TOFAUTI NA WATU WENGINE,UTU NI MUHIMU.
 
Kupiga askari sio ujanja ni ujinga
Kweli kabisa.

Katika dunia askari hasa wa kiwango cha taifa ,anatakiwa kuwa smati katika hali zote ,hasa kwa askari anaedili na raia ,
Kwasababu amejifunza mambo mengi kuliko RAIA wa kawaida,mfano kumsoma mtu yupo ktk halo gani ,mbinu,ujasiri,uvumilivu nk ,

Kwahiyo sio vyema unapomuona RAIA kafanya kosa na wewe uanze kumbuluta makonde na makofi heti kwasabu wewe ni askali,mambo haya yapo kwa waafrica tu.

Msome mtu yupo ktk hali gani.
Hutakiwi kutumia ubabe pasipohitaji ubabe.
 
Huyo traffic ni kama ana hasira na maisha yake.. hii kitu haitakiwi kutendwa kihivyo kabisa. Kingine haionyeshi makosa na hakuna ngumi zaidi ya kukabana mashati na dereva. Inatia aibu traffic kutenda hilo hata baada ya mwemzake na raia kumsihi akaendelea tu. Hata kama dereva ana kosa.. inabidi watafute mbinu za kuwabana hao madereva wasiotii sheria za barabarani ikiwa wanaogopa kukimbiwa nao
Asante comrade leo sijui nan ka hack account yako maana nmekuelewa haswa
 
Back
Top Bottom