Askari shupavu akifa, mapambano hayakomi

Askari shupavu akifa, mapambano hayakomi

Na. Julius Mtatiro,
Mapambano yaendee, askari amekufa mstari wa mbele wakati vita inakaribia kuisha, ni bahati mbaya, chukueni mwili wake, upeni heshima zote za mwisho kisha uhifadhini na kukumbuka mchango wa askari huyo.

Si muda wa kumbeza na kumsimanga, si muda wa kumuombea mabaya.
Wanaweza kufa askari wengi sana dakika za mwisho za mapigano lakini kusaka ushindi vitani ni jukumu la askari waliobakia, hata wakibaki wachache ni lazima washikamane na vita iendelee, huu siyo wakati wa kujiuliza kama sababu za kuingia vitani zilikuwa sahihi au la, huu siyo muda wa kuacha vita na kuanza mjadala juu ya askari shupavu aliyeuawa mstari wa mbele, huu ni muda wa kupigana vita, vitani hakuna msalie mtume na ukitaka salamu ya upande wa adui umeshakaribisha kifo chako. Vita haina macho, yeyote yule anaweza kuuawa.
juliusmtatiri@yaho

Unafiki wa Lipumba wamtoa Mtariro alipo
 
mnafiki wewe usiyejitambua lipumba kujiuzulu ni haki yake kwani lazima awe mwenyekiti??? si ndio nyinyi mhuwa mnasema hapa prof ni sultani nyinyi vipi??/
 
Nimeipenda hiyo mpo vijana wengi na wazee wengi tu wenye busara wanaoweza kuziba pengo mshikamano unatakiwa huyo nahodha kajitosa kwa kuogopa mawimbi sie tuendelee na safari
 
askari aliyekatisha mapambano mbele ya mstari hatari
11248254_1474474542874256_5288858298985108461_n.jpg
 
😡Na vita ya safari hii ni ngumu mno, tuko busy kupambana na adui, kama askari shupavu akifa mstari wa mbele hatuziki tunamuacha msituni baada ya kuupata ushindi tunaopigania tutarudi kwa ajili yake.
 
😡Na vita ya safari hii ni ngumu mno, tuko busy kupambana na adui, kama askari shupavu akifa mstari wa mbele hatuziki tunamuacha msituni baada ya kuupata ushindi tunaopigania tutarudi kwa ajili yake.

Naam, baada ya vita na hasa baada ya ushindi tutarudi kufuata mwili wa askari aliyeuawa, kama kajeruhiwa tu tutamfuata kwa ajili ya kumpeleka hospital ya jeshi kutoa mabaki ya risasi za rushwa alizopigwa nazo katikati ya vita.
 
Tutatumia silaha yoyote haijarishi maadui zetu wanaiona ni sahihi au la! chamsingi mfumo wote ubadilishwe. Vita hii si mchezo....nikubaliane na mtoa mada kuwa yawezakana askari wengine mashuri wakafuata....ilo halikatishi maamuzi magumu ya askari shupavu waliobakia kusonga mbele....tunaitaji ushindi....mjadara wa nani kafanya nini utakuja baadae....

Niwaambie....watanzania tuna bahati sana...timing ya askari huyu ilikuwa ukawa wasipate mgombea kupitia vyama hivyo...na ndivyo ilivyokuwa iwe....alitaka askari huyo yeye ndiye awe.....na mchzezo huo ungefanyika dakika za mwisho. Askari wenzake shujaa zaidi wakiliona hilo....wote waliotaka wawe wakawekwa pembeni.....tunasubilia maamuzi ya askari mwingine....ahukumiwe na historia yake mwenyewe!

Tunakoelekea ni ushindi....tena mapema asubuhi
 
Back
Top Bottom