jaffari odhiambo
JF-Expert Member
- Jan 1, 2014
- 526
- 13
Kwa taarifa zilizothibitishwa zinasema kuwa askari polisi aliyekuwa lindo katika BENKI YA TWIGA ilioko katikati ya UKEREWE ROAD na BOMA ROAD ampiga dereva bodaboda kichwani kwa fimbo na kuzimia. Chanzo cha tukio hilo ni kwamba, huyo bodaboda alikuwa anadaiwa sh.1000 tu na jamaa mmoja aitwaye NYIREMBE ambaye aliwatumia mgambo kwenda kumkamata mhusika. Baada ya mgambo kufika hapo bodaboda akakataa ndipo huyo askari akamfuata huyo bodaboda wanakopaki eneo la Round About na kumshika na kumfunga pingu. Baada ya kumfunga pingu ndo askari huyo akampiga kichwani na kuzimia. Baada ya hapo, traffic police aitwaye JOHN akawa anapita na kumbeba mpaka hospitali ya D.D.H BUNDA. Kwa hali aliyonayo ni kwamba sio nzuri maana hata haongei na huyo bodaboda anaitwa SAMWEL anapaki round abaout barabara iendayo Bomani.