Askari mwingine auwawa Mkuranga!

mkonomtupu

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
441
118
Jana majira ya jioni, nikiwa naangalia mpira, mida ya saa moja usiku. Rafiki yangu ambaye ni askari ambaye yuko Mkuranga alinipigia simu akinitaarifu kuwa kuna askari mwenzao anayejulikana zaidi kama Tekamaji, amegongwa na Landcruiser wakati yupo doria, barrier eneo la mizani Mkuranga maarufu kama Magogo Matatu.

Alikuwa on duty na askari wenzake, ambapo marehemu alikuwa analisimamisha gari hilo kwa tochi kwa ishara ya kuichezesha ili dereva asimame.

Inaonekana dereva alikuwa mwendo kasi sana, hivyo basi badala ya kusimama, alimgonga askari huyo, na kukimbia baadae alilitelekeza gari na kukimbia kwa miguu.

Marehemu alichukuliwa na ambulance, na kupelekwa hospitali ya Wilaya. Lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya na kukimbizwa Muhimbili, na alipofika huko hali ilizidi kuwa mbaya na hatimaye alifariki.
 
duuuuu kazi kwelu hawa jamaa wanajitahidi sana kwa kazi lakini wanavyolipwa utacheka
 
Vizuizi vitumike baada ya askari kukaa kati ya barabara.Maana wehu wengi sana mabararani,nakumbuka kauli ile inayosema una po drive ona we ndio dereva timamu,madereva wengne n matahira,ukitembea na formula hiyo unakuwa na uhakika wa kuepuka ajali asilimia flani.R.I.P AFANDE TEKA MAJI
 
Utaratibu wa tochi sio sawa kabisa maana sidhani kama ni mojawapo ya alama za barabarani!!!
Mtu anaweza kudhani ni jambazi au mtu mwenye nia mbaya, hata mtu akisema alivaa koti na nini sijui reflekta, ntauliza hakuna wahalifu wenye mpaka sare za vyombo vya ulinzi???!!!

Wenzetu wawekewe mazingira mazuri ya kufanya majukumu yao ziwekwe barriers na nailed chains zikitanguliwa na road signs kama "check point ahead", "simama ukaguliwe" zikiwa wazi na za kusomeka hata kama movable kwa minajili ya kutozoeleka vituo lakini sio tochi, kama pale Dumila na wakati mwingine Gairo ni vile panajulikana tu ila hatari tupu! !!!!

Kabuku wanaweka machuma kabisa yaani ukiliingia au rejeta au taa unaacha hapohapo!!!!!!

Lakini afande naye mashine inayosimama na inayopitiliza kweli zina mlio mmoja????!!!!
Dereva kaacha gari au kaacha gari baada ya kutoa ambavyo vilimfanya asisimame kwa ukaguzi???!!

Mungu amlaze pema!!!!!!
 
Hizi kazi za ulinzi yani hata hazina uhakika wa kurudi nyumbani salama. R.i.p police
 
Huyu kauwawa au kafa kwa kugongwa na gari? Kichwa cha habari hakijakaa sawa.
Jana majira ya jioni, nikiwa naangalia mpira, mida ya saa moja usiku. Rafiki yangu ambaye ni askari ambaye yuko Mkuranga alinipigia simu akinitaarifu kuwa kuna askari mwenzao anayejulikana zaidi kama Tekamaji, amegongwa na Landcruiser wakati yupo doria, barrier eneo la mizani Mkuranga maarufu kama Magogo Matatu. Alikuwa on duty na askari wenzake, ambapo marehemu alikuwa analisimamisha gari hilo kwa tochi kwa ishara ya kuichezesha ili dereva asimame. Inaonekana dereva alikuwa mwendo kasi sana, hivyo basi badala ya kusimama, alimgonga askari huyo, na kukimbia baadae alilitelekeza gari na kukimbia kwa miguu. Marehemu alichukuliwa na ambulance, na kupelekwa hospitali ya Wilaya. Lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya na kukimbizwa Muhimbili, na alipofika huko hali ilizidi kuwa mbaya na hatimaye alifariki.
 
pole wafiwa msiba unauma kwa wafiwa hata angekuwa kafa vp kwao wamempoteza kipenzi
 
Utaratibu wa tochi sio sawa kabisa maana sidhani kama ni mojawapo ya alama za barabarani!!!
Mtu anaweza kudhani ni jambazi au mtu mwenye nia mbaya, hata mtu akisema alivaa koti na nini sijui reflekta, ntauliza hakuna wahalifu wenye mpaka sare za vyombo vya ulinzi???!!!

Wenzetu wawekewe mazingira mazuri ya kufanya majukumu yao ziwekwe barriers na nailed chains zikitanguliwa na road signs kama "check point ahead", "simama ukaguliwe" zikiwa wazi na za kusomeka hata kama movable kwa minajili ya kutozoeleka vituo lakini sio tochi, kama pale Dumila na wakati mwingine Gairo ni vile panajulikana tu ila hatari tupu! !!!!

Kabuku wanaweka machuma kabisa yaani ukiliingia au rejeta au taa unaacha hapohapo!!!!!!

Lakini afande naye mashine inayosimama na inayopitiliza kweli zina mlio mmoja????!!!!
Dereva kaacha gari au kaacha gari baada ya kutoa ambavyo vilimfanya asisimame kwa ukaguzi???!!

Mungu amlaze pema!!!!!!

Gairo na Dumila ipo siku nao itakuja jibu. Heri hao wa segera.
 
Mungu awaepushie na hilo.......ila ni wakati sasa hili liangaliwe!!!!

pole kwa jeshi la polisi ila jeshi la polisi linabidi kujirekebisha utendaji wao wa kazi hizi tabia za kusimamisha gari ghafla ndio madhara yake hayo kama mbunge wa musoma mjini alilisema hili bungeni askari huwa wananjificha halafu anatokea ghafla na kusimamaisha gari .hii tabia inabidi jeshi la plisi kitengo cha usalama barabarani wajirekebishe kama sehem ni official kwa ajili ya kukagua gari mida ya usiku kwanini isiwekwe beria na reflector ziwekwe manake usiku kuna mambo mengi wengine ni askari feki
 
Kuna siku tumewahi nusurika kupata ajali maeneo ya mikese.Dreva kaitungua mashine spidi kama 110 hivi.kumbe trafiki kajificha kwenye kibao cha shule ile tumefika karibu tu kachomoka mpaka katikati ya barabara kazi ikawa kwa dreva kumkwepa maana angepiga breki ya gafla angetumwaga.RIP AFANDE
 
Kuna kipindi kamanda Mpinga alilisemea hili sijui liliishia wapi kwa vitendo
 
Kuna siku tumewahi nusurika kupata ajali maeneo ya mikese.Dreva kaitungua mashine spidi kama 110 hivi.kumbe trafiki kajificha kwenye kibao cha shule ile tumefika karibu tu kachomoka mpaka katikati ya barabara kazi ikawa kwa dreva kumkwepa maana angepiga breki ya gafla angetumwaga.RIP AFANDE

Honi ya moja kwa moja na taa tu huwa wanatoka mbona, unasimamia mbali unapiga haja ndogo kabisa aje akitembea ili ajue gari ni chombo na muendeshaji ndio mtu..................wanafanya makusudi tu na utaratibu wanaujua vizuri sana au kusimamisha gari ye yuko upande wa pili wa barabara!!!!
 
Back
Top Bottom