Askari JWTZ mbaroni na mbao 600 za wizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askari JWTZ mbaroni na mbao 600 za wizi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bavaria, Sep 11, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,096
  Likes Received: 11,234
  Trophy Points: 280
  ASKARI wawili wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kambi ya Mirambo mkoani hapa ni miongoni mwa watu tisa waliokamatwa na kikosi cha kuzuia ujangili wakiwa na mbao 630 bila kibali.

  Wanajeshi hao Koplo Moshi Jumanne na Praiveti Mustapha Yusuf, walikamatwa wakiwa na gari kubwa la JWTZ aina ya Iveco likiwa limesheheni mbao ndani ya Pori la Akiba la Kigosi mkoani hapa.

  Walikamatwa Ijumaa saa mbili usiku wakiwa na gari hilo pamoja na mwanamke aitwaye Sophia Shigemela ndani ya pori hilo eneo la Ulyankulu wilayani Urambo.

  Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi ya Rasilimali Misitu (TFS), Vallentine Msusa aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa alipewa taarifa juu ya kukamatwa kwa watumishi hao wa Serikali wakiwa na maliasili hizo bila kuwa na kibali, kitendo ambacho ni cha aibu kwa Taifa. Msusa alisema gari lililokamatwa bado linashikiliwa katika kambi ya ndani ya pori hilo likiwa na mbao hizo.

  Alisema siku za karibuni watu wengi wamekuwa wakitumia magari ya Serikali kusafirisha maliasili za misitu kwa vile hayakaguliwi kwenye vizuizi na kusababisha kupakwa matope watumishi wa wizara hiyo kuwa wahusika wa uvunaji holela wa maliasili.

  Msusa alisema kitendo cha watendaji wa Serikali kutumia magari yao kusafirishia mazao ya maliasili, kimesaidia majangili kuingia ndani ya mapori na kuvuna mali zilizopo kwa kujiamini.

  "Tulitarajia taasisi za umma zingesaidia ulinzi wa misitu na raslimali zilizomo, lakini kumbe sivyo," alisema Msusa.

  Kwa mujibu wa Msusa, wanajeshi hao na watu wengine waliokamatwa na magari yakiwa na mbao hizo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

  Vitisho Katika hatua nyingine, Msusa alisema kumekuwa na matukio yasiyofurahisha kwani wiki mbili zilizopita, askari wa JWTZ wa kikosi cha Mirambo walimpiga mtumishi wa Idara ya Misitu huku wakimtishia kumuua.

  Habari zilizopatikana kutoka ya kambi Kikosi cha Kuzuia Ujangili katika pori hilo, zilidai kuwa magari ya JWTZ yamekuwa yakibeba mbao ndani ya pori hilo mara mbili kwa wiki, wakidai kuwa wanakwenda kutumia katika ofisi zao. Inadaiwa kuwa askari hao wawili baada ya kukamatwa wakiwa na Sophia, walidai kuwa wamekodishwa.

  Hata hivyo, kwa mujibu wa madai hayo, baada ya mahojiano, askari hao walidai kutoka Biharamulo na walikuwa wamesafirisha maiti lakini wakakosa mafuta ya kuwarudisha kwao, ndipo wakakubali kukodishwa ili wapate fedha za mafuta ya kurudia.

  Watu wengine waliokamatwa siku hiyo wakiwa na gari namba T 761 BCV aina ya Fuso likiwa na mbao zaidi ya 350, ni Kiwele William na Sultan Hamda dereva wa Fuso, Richard Samwel, Msina John, Bashiba Lugaka na Gaspar Kugatwa.

  SOURCE: HabariLeo
   
 2. peri

  peri JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  inakuaje watumishi wa umma tena wanaopaswa kulinda wanaenda kuiba?
  Watu kama hawa ni kuwapa adhabu kali ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi.
  Pia uchunguzi zaidi ufanyike manake mi naamini kutakuwa na wakubwa nyuma yao.
  Haiwezekani waondoke na gari la jeshi watu 2 tu bila kuwa na mkubwa nyuma yao.
   
 3. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa kuwa fani hii inanihusu kwa kiasi fulani, acha niwape wengine nafasi ya kuchangia.
   
 4. B

  Baba Matatizo JF-Expert Member

  #4
  Sep 11, 2012
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Dah kweli wameumbuka.hakuna gari zinazobeba magendo kwa kasi siku hizi kama gari za jwtz.ni wezi kuliko maelezo.dili zote haramu zinapigwa na gari za jwtz
   
 5. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #5
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Hii mbaya ndani ya Taifa letu!  Tanzania ni zaidi ya tujuavyo!
   
 6. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Eti hao ndiyo polisi wa kulinda mali na raia!!! Mijtu ya dili na wezi wa kutupwa!!! Imagine wa Dar wanashiriki wizi wa juzi kopa bandarini!!! Ninasema SSM ikiondoka vunja jesh lote, la posili na lile lngine!!! Wamepoteza credibility.
   
 7. kupe

  kupe JF-Expert Member

  #7
  Sep 11, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 1,025
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Na polisi pia wanatumia gari zao defender kusafirishia deal zao
   
 8. kupe

  kupe JF-Expert Member

  #8
  Sep 11, 2012
  Joined: Jul 26, 2012
  Messages: 1,025
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  defender, pikipiki (tigo) na magari mengi ya serikali yanatumika kwa uhalifu. Mfano yule mbunge songea aliyekamatwa na meno ya tembo........
   
 9. MK254

  MK254 JF-Expert Member

  #9
  Nov 12, 2014
  Joined: May 11, 2013
  Messages: 9,402
  Likes Received: 6,593
  Trophy Points: 280
  Yaani hata afadhali KDF wetu wanaiba dhahabu Westgate, hawa wanaiba mbao vijijini. CC: kadoda11
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. petermasele

  petermasele Member

  #10
  Nov 18, 2014
  Joined: Oct 22, 2014
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wameachiwa hao wajesh?
   
 11. H

  Hasadi JF-Expert Member

  #11
  Nov 18, 2014
  Joined: Jan 10, 2014
  Messages: 258
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  si wawachome moto tu pamoja na gari lao si wezi hao
   
 12. Kizzy Wizzy

  Kizzy Wizzy JF-Expert Member

  #12
  Nov 19, 2014
  Joined: Aug 2, 2013
  Messages: 1,729
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Kuwa na akili wewe hakuna cha uafadhali hapo wote mavi tu.Kwa vile walipata nafasi wakaiba dhahabu westgate na mkawaona, je unajua ni mambo mangapi ya kishenzi wanayafanya ambayo hamuyaoni?
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...