Askari jambazi auawa na raiya

Askari jambazi auawa na raiya

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
62,190
Reaction score
128,272
Ilikua ni juzi mishale ya saa kumi na mbili jioni maeneo ya mbauda ktk mji wa Arusha ambapo mfanyabiashara wa vifaa vya ujenzi mwenye asili ya kabila la maasai alikua akijongea kwake kwa gari aina ya canter lililokua likiendeshwa na mke wake.
Gafla wakikaribia geti la kuingia nyumbani, ilitokea pikipiki iliyokuwa na watu watatu(mshkaki) ambapo alishuka kijana mmoja na kuwaonyesha bastola mzee yule na mkewe na kuwataka wampatie fedha.
Mama yule alikabithi pochi kwa jambazi lile na baba akaambiwa na yeye atoe fedha zote za mauzo, mzee yule akaingiza mkono mfukoni kuashiria kuwa anatoa fedha lakini kinyume chake mzee yule akatoa bastola yake na kumlenga jambazi ambapo palepale akapoteza maisha na wenzake wawili wakakimbia na pikipiki.
Baada ya kukagua bastola aliyokua nayo jambazi yule ikagundulika kuwa bastola ile ni mali ya jeshi la polisi na jambazi aliyeuwawa ni askari polisi wa hapa mjini arusha.
Mpaka sasa habari hii inafichwa na swala hili linaendeshwa kwa usiri mkubwa kwa nia ya kuhifadhi reputation ya jeshi la polisi.

My take:
Hawa askari wanapewa silaha nzito while wanalipwa mshahara kiduchu sasa matokeo yake wameamua kuwa majambazi na kuacha kazi ya ulinzi wa raiya na mali zake. Hakika watatumaliza.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
hahaha kila mtu apewe bastola ili kuwe na heshima hapa
Arusha na sehemu nyingine za tz
 
Asilimia kubwa y ujambazi wa kutumia silaha nchini utatendwa na polisi na wana jeshi.
 
Ndiyo faida ya serikali tawala na jeshi lake la kuaminika!
 
Hata kama mishahara kidogo kufanya hivyo ni mbaya sana, ona sasa huyu kapoteza maisha kipumbavu hivyo, pia kaliaibisha vibaya sana jeshi la polisi.
 
Naona umetueleza kabila la huyo mfanya biashara tu, hujatueleza na kabila la huyo jambazi. Naomba lisiwe lile kabila al maaruf kwa shughuli hizo.
 
lo huyo mzee anastahili pongezi
nakumbuka enzi za nyuma majambazi walikuwa wanatuma kinote kuwa watakuja usiku. mzee moja aliwaachia mlango wazi kabisa ili wakija wasipate tabu. alipowaona alisimama kando ya mlango huku akiwa amechomoa bulb ya sebuleni ili wakiingia wanapowasha taa wasimwone. alipoingia jambazi mmoja ile anapapasa switch mzee alimkata panga la kichwa akaanguka hapo hapo kimya.wenzie walipoona kimya mwingine aliingia nae alikatwa bega kwa nguvu zote wa tatu alikimbia.
mwanae na yule mzee alizunguka uwani akaenda kutoa upepo matairi yote la gari la majambazi.alipewa fedha na jeshi la polis ilikuwa mwaka 1992.
je kwa sie wa leo ujasiri huu twauweza?
 
Dah jamaa aliazima bastola polisi ili apigie dili
 
Kaka kweli kuishi kwingi ni kuona mengi!, nilikuwa mtoto sana hii story ningeisikia wala nisingeweza kuelewa
 
Kwa nn stori hiyo iwe siri ? Na wasi wasi na ukwel wa taarifa hii ebu lete facts kama jina la askar huyo na kituo chake cha kazi na pengine hata picha za tukio ili walau tuamin stor yako !!! Kwa vyombo vya habar vilivyo vingi nchini story hiyo wawe hawajaipata !!!? Sio kweli
 
lete vielelezo vya kutosha tumbananishe kamanda wa polisi mkoa wa arusha atoe tamko
 
mwaka 1992 niko la 6 kijana
umejiandika babu wa loliondo ilhali u kinda kwanini
zamani ndio ikuwa hivo.
KIna mtambuzi asprin watanishukia hapa kuwa nami mtoto manake miaka hiyo watu tayari wako kazini
Kaka kweli kuishi kwingi ni kuona mengi!, nilikuwa mtoto sana hii story ningeisikia wala nisingeweza kuelewa
 
Kwa nn stori hiyo iwe siri ? Na wasi wasi na ukwel wa taarifa hii ebu lete facts kama jina la askar huyo na kituo chake cha kazi na pengine hata picha za tukio ili walau tuamin stor yako !!! Kwa vyombo vya habar vilivyo vingi nchini story hiyo wawe hawajaipata !!!? Sio kweli
Sina sababu ya kutunga au kumsingizia askari jambo lolote, kama nilivyosema awali kuwa jeshi la polisi linaficha habari hii for the purpose of reputation, kupata baadhi ya detail inakua ngumu ila ukweli ndo uwo kitenge shaban
 
hayo yapo sana. masiha magumu, majuku mengi. kujikimu watu wanaenda front. imekuwa siri lakini JF, haiwezi kuwa siri hata kidogogo. wataumbuka tu.
 
vipi wameshazika?.r.i.p jambazi.
 
Back
Top Bottom