Askari ''Cornell Kufahaizuru' aliyezuia wizi bandarini Dar atekwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askari ''Cornell Kufahaizuru' aliyezuia wizi bandarini Dar atekwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by R.B, Sep 11, 2012.

 1. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 6,163
  Likes Received: 1,098
  Trophy Points: 280
  MMOJA wa askari wa bandari, Cornell Kufahaizuru aliyeshiriki operesheni ya kuzuia jaribio la wizi wa shaba na mafuta Bandari ya Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita, juzi ametekwa na watu wanaodaiwa ni wahusika wa jaribio hilo.

  Taarifa zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe zilieleza kuwa juhudi za kumtafuta zinafanywa na vyombo vya dola nchini.
  Licha ya Dk Mwakyembe,chanzo kingine cha habari cha kuaminika kutoka Kitengo cha Ulinzi na Usalama katika bandari hiyo, kimethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

  Waziri Mwakyembe alisema Kufahaizuru alitoweka siku moja baada ya kupambana na katika zoezi la wizi huo, hajulikani alipo.

  “Juhudi za kumtafuta huyo kijana na waliomteka zinaendelea, lakini mpaka sasa hajapatikana ingawa kuna taarifa zisizo rasmi zinazoeleza kuwa kuna maeneo huwa anaonekana,” alisema Dk Mwakyembe na kuongeza:
  “Uhalifu wa aina hii ni mpya kabisa, huu ni ukurasa mpya wa uhalifu nchini lazima tupambane nao, unaweza kuufananisha na zile filamu za nchini Nigeria.”
  Awali, askari mmoja katika kitengo cha ulinzi bandarini hapo kwa sharti la kutotajwa, alidaiKufahaizuru alitekwa na watu wasiojulikana juzi.

  Alisema jana kuanzia saa 7:00 mchana walianza kupokea ujumbe mfupi wa maneno kutoka simu ya askari huyo, ukitoa masharti ya kuachiwa kwa wahusika wote waliokamatwa kwa tuhuma za kuhusika na jaribio la wizihuo.
  Chanzo hicho kinadai kuwa, watekaji hao wametoa saa 24 kutimizwa kwa sharti hilo na iwapo halitatekelezwa kwa wakati, wametishia kumuua askari huyo.

  Kuhusu hatua zilizochukuliwa mpaka sasa za kumwokoa askari huyo, chanzo kingine cha habari kutoka ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama, kimedai kuwa wanafanya kila linalowezekana na wameshaanza rasmi msako mkubwa wa kuwasaka wale wote wanaohusika na utekekaji huo na wanatarajia kuwanasa muda wowote.
  Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama wa Bandari, Mranda hakukanusha wala kukubali na kudai kuwa yuko safarini akirejea Dar es Salaam.

  Jumamosi iliyopita, watu 10 wakiwamo polisi wawili walikamatwa kwa tuhuma za kutaka kuiba shaba katika bandari hiyo.Shaba hiyo iliyokuwa katika kontena, inakadiriwa kuwa na thamani ya Sh1 bilioni na ilikuwa iibwe saa 9:00 usiku wa kuamkia juzi.

  Tukio hilo linadaiwa lilikuwa likiratibiwa na polisi kadhaa wakiwamo wa Kikosi cha Mamlaka Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), walioingiza bandarini kichwa cha treni pamoja na watu wengine wanane kwa ajili ya kutekeleza wizi huo.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa juzi, askari wa bandari walipata taarifa za kuwapo kwa uhalifu huo na kwenda eneo hilo na walikuta watuhumiwa hao wakipakia shaba hiyo.
   
 2. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Hii kali now! Kweli Huo mtandao wa wizi Bandarini ni mkubwa na una wakubwa wengi hasa katika Jeshi la Policcm na wana Usalama. Dr. Mwakyembe katu hautashinda vita hii, labda CCM itoke madarakani
   
 3. Msolopagazi

  Msolopagazi JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 659
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Mmmmh hatari naona Tanzania kisiwa cha amani sasa imekuwa nchi ya kimafia hawa policcm nao kazi ni kuua watu wasio na hatia na kupiga deals
   
 4. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #4
  Sep 11, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,160
  Likes Received: 1,162
  Trophy Points: 280
  Polis! Wauwaji wako humo, wezi wako huko, wafanya magendo huko, wauza madawa ya kulevya huko, rushwa ni wao, kunyanyasa na kubambikia watu kesi ni wao, sasa wameanza na utekaji!.
   
 5. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #5
  Sep 11, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Tunategemea ufanisi wa taarif za kiitelijensia kwenye hili zaidi ya mambo ya siasa kama tulivyozoea, niwakati wa kuvipima ufanisi vyombo vyetu vya usalama.
   
 6. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,567
  Likes Received: 1,930
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo unamshauri aache wizi uendelee? Hii ni vita ya watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi yao.
   
 7. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #7
  Sep 11, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Intelijensia ya jeshi la polisi inatakiwa kujidhihirisha katika tukio hili. Kufahaizuru ni lazima apatikane haraka iwezekanavyo vinginevyo hii aibu sijui wataificha wapi...
   
 8. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #8
  Sep 11, 2012
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hii ndiyo tanzania, Zuia wizi, Penda Haki au ungana na jamii ya kimasikini kulinda maslahi yao uingie kwenye vita na wenye nchi, cha ajabu sijamuona kamanda Kova kuitisha press kuzungumzia hili, naona keshachoka kuongopa!!! I wonder why that alienda Hijja!!!
   
 9. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #9
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Kama Rais doesn't care, Unadhani nita thubutu kuingiza pua yangu, waniteke? Lakini CCM ikitoka madarakani wote hao watafirisiwa tuu kabla ya kwenda Jela
   
 10. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #10
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,245
  Trophy Points: 280
  Haitakuwa aibuya kwanza wala ya mwisho. Wana ukomavu wa aibu hawa. Wenyewe wahusika tu
   
 11. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #11
  Sep 11, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,788
  Likes Received: 3,877
  Trophy Points: 280
  ya Ulimboka yako wapi si upepo tu umeshapita!!
   
 12. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #12
  Sep 11, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  hii kitu sasa inakua balaaaaaaaa
   
 13. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #13
  Sep 11, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ujuha sio amani. Wajinga ndio waliwao. Yote haya ni sababu ya watu kukata tamaa ya maisha. Ikiwa polisi nao wamo kwenye dill hiyo na wanaua mtu yeyote anayetaka mabadiliko kwa kutumiwa na waliopewa dhamana ya kutunza amani na usalama, wapi tukimbilie? Ndo maana watu hujichukulia amri mikononi. Hata mahakamani ukienda kuna mkono wa mafisadi. Tunaongopeana, hakuna amani ila woga tu Tanzania. Labda useme kisiwa cha waoga.
   
 14. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #14
  Sep 11, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Anabaka kuku?
   
 15. G

  Gilly Member

  #15
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kwani Kamanda Kova ni Alhaji??
   
 16. M

  MR.KUMEKUCHA Senior Member

  #16
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 30, 2012
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Police wanafanya wizi baadhi yao ni kutokana na maslahi yao ni madogo wanashindwa kuandamana2.na huyu inawezekana ametekwa na wao wenyewe polisi ili kupoteza ushaidi.uaminifu kwa polisi jamii wakakamavu umeshuka kwa kiasi kikubwa sana sasa tufanyaje wadau wa tz?
   
 17. o

  obwato JF-Expert Member

  #17
  Sep 11, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Tatizo sio udogo wa mshahara,mbona mabosi wao wana mishahara mizuri lkn ndio waratibu wa ujambazi na madawa ya kulevya? Tatizo ni kuchoshwa na vitendo vya mabosi wao ndio maana nao wanaamua kuchukua chao mapema na sera zao za kulindana ndio zinawapa kichwa ila siku zao zinahesabika.
   
 18. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #18
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nchi nyingine sehemu nyeti kama bandari, airport, ikulu wanalinda wanajeshi ama polisi maalumu. Sasa sisi polisi wetu tunatumia kuzuia maandamano tu.
   
 19. T

  Toshack Kibala Member

  #19
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huo wizi wale walikuwa wafanyakazi wao ila wezi wenyewe wapo tena ni wakubwa na wana nguvu kuliko hata waziri tusubili tuone ila sina imani na jeshi la polisi kuhusu wezi hawa,ingawa baadhi yao kama huyo aliyezuia wizi huo hatuna budi kumpongeza.
   
 20. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #20
  Sep 11, 2012
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  KApatikana IRINGA-MAFINGA yuko salama!!
  source KOVA
   
Loading...