Askari aliyepiga picha na Lema atokomea

Askari aliyepiga picha na Lema atokomea

Sabung'ori

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2011
Posts
2,166
Reaction score
1,248
Nape tunaomba utueleze kadi za hao maafisa wa jeshi waliomaliza kufanya kazi( U-DC na RC) za chama(CCM) na kurudi jeshini ziko wapi?

Monday, December 31, 2012



Na : Nuzulack Dausen



JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limesema askari anayedaiwa kuwa jeshi hilo aliyepiga picha na Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ametoroka.

Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe alisema jana kwamba pamoja na hatua yake ya kutoroka, jeshi litaendelea kumsaka kwa udi na uvumba ili kumhoji na kujiridhisha kama kweli ni mwanajeshi wake kabla ya kumchukulia hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Kifungu cha 147 cha Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya 1977.

“Huyu kijana inasemekana alishawahi kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), lakini wakati tunaendelea na uchunguzi alitoroka katika nyumba aliyokuwa amepanga bila ya taarifa kwa baba mwenye nyumba,” alisema Kanali Mgawe na kuongeza:

“Askari huyo alikuwa anaishi katika nyumba ya kupanga mita chache karibu na Kituo cha Polisi cha Simanjiro, Arusha na alikuwa akijishirikisha na ulinzi shirikishi.”

Alipoulizwa jina la askari huyo, Kanali Mgawe alijibu: “Yeye alikuwa anafahamika mtaani hapo kwa jina la kamanda.”

Hata hivyo, Kanali Mgawe alisema jeshi hilo litahakikisha linatoa ripoti kamili kwa umma baada ya kumkamata na uchunguzi kukamilika ili kuondoa utata uliogubika suala hilo.

Alipoulizwa kama kuna tofauti gani kati ya mwanajeshi kuingia kwenye mikutano ya wanasiasa na wale wanaofanya kazi za kisiasa kama wakuu wa wilaya na mikoa, Kanali Mgawe alijibu:” Wanajeshi wanaofanya kazi za U-DC au RC, wanaruhusiwa kisheria.”

Alifafanua kuwa iwapo mwanajeshi atateuliwa kufanya kazi katika taasisi yeyote ya Serikali nje ya jeshi, atatakiwa kuvua magwanda ya jeshi na kufanya kazi hiyo mpaka atakapomaliza muda wake na baada ya hapo ataruhusiwa kurejea jeshini.

“Kuna kitu kinaitwa ‘secondment.’ Mwanajeshi anaruhusiwa kufanya shughuli zozote nje ya jeshi iwapo atahitajika kufanya hivyo. Ila kwa masharti ya kuvua magwanda, hivyo wananchi wasishangae kuwaona baadhi ya askari wetu ni wakuu wa wilaya na mikoa na baadaye kurudi jeshini kuendelea na majukumu yao,” alisema Kanali Mgawe na kuongeza:

“Askari akiwa katika majukumu yake mapya, atafanya kazi zote atakazopewa zikiwamo za kisiasa kama ilivyo kwa wakuu wa wilaya na mikoa, lakini akirudi jeshini, anarudi kuwa askari mwenye utii na kufuata kanuni za jeshi zisizofungamana na siasa.”

Chanzo: Mwananchi
 
Kwa maelezo ya huyo msemaji wa jeshi,tanzania tuna matatizo. Mungu atuepushie mbali,inakuwaje dc-mwanajeshi ashiriki siasa? Halooo.......ccm ni zaidi ya uijuavyo!
 
"Huyu kijana inasemekana alishawahi kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), lakini wakati
tunaendelea na uchunguzi alitoroka katika nyumba aliyokuwa amepanga bila ya taarifa kwa baba mwenye nyumba," alisema Kanali Mgawe na kuongeza:


hizi sarakasi mpaka lini?
 
Anajichanganya, mara hawamjui, mara katoroka, tutamtafuta huu ni ubabaishaji ambao nadhani kwa iteligensia ya jeshi haiingii akilini, labda itelijensia ya wale wa wema wa ccp
 
Huyo soja, imeshakula kwake!!!!! atokomee na asionekane kabisa, la sivyo watam-Kolimba!!!!!
 
hii kali kamanda kumbe alikuwa sahii, hata hivyo siku ya tukio nilimwona kamanda akiwa mwenye furaha kweli hawa mabwana wanaipenda chadema kweli kwani wamegundua wao ndio watakuwa mabosi 2015 mabosi wao wa sasa ni mafisadi wakati huo watakuwa jela
 
Aisee Kamanda anazidi kuibua mjadala mzito mkubwa zaidi
Nahitaji kujua iyo sheria ya secondment tu-construe.

...utata uko hapo Kanali anaposema kwamba wanajeshi anapotakiwa kufanya kazi za serikali na za-kisiasa(U-DC na RC) wanavua kombati na kufanya hizo kazi,lakini hajatuambia wanapomaliza hizo kazi za kisiasa kama wanajivua uanachama wa CCM na kurudisha kadi ya chama!...
 
Kuwa mwanajeshi c sababu kuwa huna haki ya kushirki kama mtu mwingine kawaida lah! Suala tunalotakiwa kuelewa hapa ni wakat gan unatakiwa kushirk kama taratibu za nchi zinavyoeleza ndilo suala kamanda mgawe analolieleza, tuache ushabk kabla ya kujua taratib za sehem husika (nchi)
 
  • Thanks
Reactions: GDM
Wanamtafura wa nini? Kwa kuwa alivaa sare? Kama wao wako makini, hizo sare alizipata wapi na kwa nini hawakuchukua hatua kabla ya hapo? Au siku hizi hizo sare zinapatikana sokoni? Kwa maswali kama hayo na mengine mengi ni ishara tosha kuwa ulinzi wa nchi uko mashakani.
 
Hahahahaha si walisema hawa mtambui? Sasa kwa ninii wamtafute?
 
Kweli nimeamini jeshi letu halina kazi ya kufanya,kwanini wanakomaa na jambo dogo kama hilo?
 
ubabaishaji tu.... huyo msemaji kajichanganya kwenye statement yake.
 
  • Thanks
Reactions: JGG
Hahahahaha si walisema hawa mtambui? Sasa kwa ninii wamtafute?

Anatafutwa kwa kuvaa sare za jeshi na kupiga nazo picha, tena na mbunge wa chama cha Upinzani. Hili ni kosa sana bora hata angekuwa amepiga na mbunge wa chama Tawala.. Duh, siasa za Bongo hizi....!!! nashauri JWTZ waache huu ijinga waendelee na kazi zao.. hii ni siasa tu!!!
 
Kwa hiyo hawa wanajeshi waliowahi kwenda kuwa wenyeviti wa kamati za siasa za CCM mkoa na wilaya watakuwa credible kuendelea kuitumikia serikali siku CCM ikiwa haipo madarakani?
Na je, wakati CCM ikitoka madaraki mwaka 2015, wanajeshi ambao kwa wakati huo watakuwa maDC na maRC, wataomba kurubi jeshini?

CDM itakuwa na kazi ngumu sana 'kusafisha' serikali na vyombo vyake, pindi watakapoichukua...
 
Back
Top Bottom