Askari ajiua kwa kujipiga Risasi Mdomoni

Askari ajiua kwa kujipiga Risasi Mdomoni

MstahikiMeya

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2014
Posts
1,633
Reaction score
561
Amejiua copy.png

TAARIFA YA KIFO:Mnamo tarehe 02/02/2015 majira ya saa 10.35hrs askari no.G.4228PC. ALOYCE ambaye alikuwa dereva wa OCD-MANYONI alifika kwa armoury keeper na kumuomba amkabidhi silaha kwani anasafari na OCD,alikabidhiwa silaha aina ya SAR NO.10065077ikiwa na risasi kumi.

Aliondoka na silaha hiyo na kuingia ndani kwake ambapo ni karibu sana na armoury na kuingia ndani ambapo aliingiza mtutu wa silaha hiyo mdomoni na kujipiga risasi huku akiwa amelala kitandani na kufariki hapo hapo.

Marehemu ameacha ujumbe kuwa ameamua kujiua mwenyewe kwa ridhaa yake na asilaimiwe mtu yeyote kuhusiana na kifo chake.mwili wa marehemu umehifadhiwa mortuary manyoni gvt hospital kwa ajili ya uchunguzi.

Pia katika ujumbe wake amedai mwili wake upelekwe kwao na S/SGT.MARWA NA SGT.MTAKI wa Polisi Singida.
 
RIP, munyandughu ww ni ----, kama ulienda shule bc kwa sababu fedha za kukusomesha zilikuwepo, other wise hiyo hela bora babako angehonga malaya wake, maiti haitaniwi popote pale duniani,ikiwa hujui kufa, tazama kaburi. Foolish lady
 
Mweeee!!!! mbona bado kijana mdogo ivo, alipatwa nalipi lililo gumu kiasi cha kushindwa kuzuia roho ya mauti???? rip
 
Kama ni police acha aende tu,ukiuwa kwa Risasi nawewe utakufa kwa Risasi.Hakuna tulichopoteza!
 
Pole sana IGP kwa kupoteza nguvu kazi. Kijana wako alikuwa bado saana yaani, ila ujiulize IGP ni nini kilimfikisha hapo? Angeweza kuondoka na askari 9 na yeye awe wa 10 ujue! Sasa ni nini hii kitu?

Je tusiwape tena bunduki?

Je tusiwaruhusu wakae na silaha karibu na wakuu wao?

je, ni maanyanyaso ya mkuu wake?

Angalia IGP leo wanajitoa uhai wao, kesho watafyeka kikosi ndo wajilipue. WAPIGWE TUUU.
 
Je ni uhamisho wa kukomolewa au mapenzi mpaka ameamua maamuzi magumu hivyo ? Kama kazi ndiyo sababu ya kujiua basi polisi wengine wapokee ujumbe wangu kuwa siyo lazima uwe polisi ndiyo maisha yaende maana kama vikwazo kazini vipo nje ya uwezo wako kazi zipo nyingi za kufanya si mpaka ujiue.
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Inawezekana kauawa manake ndio zao hizo, polisi wanaua wenzao kisha wanasingizia wamejiua.
 
Bado RPC Mihayo wa Ruvuma, naye ana damu inayomilia. Anaweza kuishia hatua kama hiyo
 
Back
Top Bottom