Taarifa yako siyo sahihi, mambo hayaendagi hivyo hata Siku moja, labda KWA kuwa hujui ukweli wa jambo lenyewe. Mara nyingi hao wahifadhi huruhusu MIFUGO kuingia kwnye mapori baada ya kupewa rushwa.Nchi hii haikomi maajabu! Kuna taarifa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa Mkuu wa Pori la Burigi mkoani Kagera, kwa kosa la mkuu huyo kukamata ng’ombe 400 walioingizwa na raia wa Tanzania na Rwanda porini humo.
Pamoja na mifugo, wenye ng’ombe hao wamekamatwa wakiwa na nyara (wanyamapori waliouawa).
Kusimamishwa kwake kumetokana na shinikizo la Wabunge wa Kamati ya Utalii, Maliasili na Mazingira wakiongozwa na Mbunge Musukuma, waliotaka mifugo hiyo iachiwe mara moja bila masharti.
Inaelezwa kuwa Mkuu wa Pori anayeitwa Bigilamungu, alihoji uhalali wa kuachiwa kwa ng’ombe pamoja na watuhumiwa hao waliokamatwa wakiwa na nyara za Serikali. Kitendo cha kusita kutekeleza amri hiyo, kumegharimu kazi yake!
Sasa wabunge wanashinikiza hata Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Profesa Songorwa naye asimamishwe kazi!
My take: Sitaki kuhukumu, lakini ndugu zangu mtambue kuwa Uhifadhi nchi hii unauawa na wanasiasa. Tatizo la mifugo katika Mapori na Hifadhi zetu nchini ni kubwa mno kuliko hata ujangili.
-Naomba niwe mchochezi kwa kutoa mwito kwa Wakuu wa Mapori wote nchini kusimama imara kumtetea mwenzao, na hilo litawezekana tu endapo wataamua kuacha mifugo iingie kwenye Mapori na Hifadhi bila kizuizi! Hatuwezi kuendelea kuwachekea wanasiasa ambao utajiri wao unatokana na mifugo- maelfu kwa maelfu- wanayoingiza katika Mapori na Hifadhi zetu.